Denmark wanasema wanataka kuhakikisha watu wao wako SALAMA kwenye Dunia inayozidi kupoteza muelekeo wa kidemokrasia na HAKI za Binadamu

Denmark wanasema wanataka kuhakikisha watu wao wako SALAMA kwenye Dunia inayozidi kupoteza muelekeo wa kidemokrasia na HAKI za Binadamu

Behaviourist

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2016
Posts
39,926
Reaction score
95,626
Mdau mkubwa wa maendeleo wa Tanzania Denmark anasema kuwa wanataka kuhakikisha watu wao wako salama kwenye Dunia inayozidi kupoteza muelekeo wa kidemokrasia na HAKI za Binadamu.

Wameyasema haya baada ya kutoa tangazo kuwa watafunga balozi zao Tanzania.

Ikumbukwe kuwa Denmark imekuwa mdau mkubwa sana wa maendeleo ya Tanzania tokea uhuru kwa kutoa fedha nyingi za maendeleo katika maeneo ya haki za binadamu, ukuzaji demokrasia, utawala bora,usalama, vita dhidi ya ugaidi,mapambano dhidi ya ukimwi na kadhalika.

Pia Denmark imekuwa ikitoa ufadhili wa Masoma kwa wanafunzi wa Tanzania.

Wameamua kufunga ubalozi wao Tanzania kutokana na mambo ya hovyo tunayoyashuhudia Tanzania sasa hivi kama vile uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia, kukosekana kwa utawala bora, kukosekana kwa utulivu na usalama,ugaidi(fake) na kadhalika.

Hii maana yake ni kwamba misaada ambayo Denmark ilikuwa inaipa Tanzania kama nilivyoainisha hapo juu haitakuwepo tena.

Wa kulaumiwa katika hili ni hii serikali fake ya CCM ambayo haina kibali cha wananchi ambayo imefikia hadi hatua ya kutengeneza ugaidi fake ili tu kutengeneza uhalali wa kuendelea kubakia madarakani kwa mabavu.

Source: Denmark yatangaza kufunga ubalozi wake Tanzania

im76543age12.png

20210828_060218_temp.jpg
 
Haki za binadamu na utawala bora ndio misingi ya utawala wa kidemokrasia popote duniani, sio kusema tu midomoni, matendo yanayoendelea Tanzania leo hii, kama Mbowe kubambikiwa kesi, wengine kukimbia nchi kwa usalama wao, ni kielelezo tosha nchi yetu haipo kwenye mstari sahihi unaotakiwa kufuatwa, asitafutwe mchawi.

Historia hii ya matendo maovu yanayofanywa na watawala nchini, yanawaondolea legitimacy yakujitetea na kuaminika kwa wananchi kwa tukio lolote, kwasababu wamekuwa wakionesha mfano mbaya kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuwakandamiza raia na vyama vya siasa, ili kulinda maslahi yao, wakidhani wenye haki ya kuitawala hii nchi ni wao pekee, sasa wastaarabu wameanza kutukimbia.
 
Denmark katika lugha ngumu isiyokuwa ya kidiplomasia wanatuma ujumbe kuwa wanapata mashaka juu ya usalama wa watu wao katika nchi hii ambayo kila kukicha inazidi kupoteza muelekeo sahihi wa kidemokrasia na haki za binadamu.

Huu ni ujumbe tosha ya kuwa hawaridhishwi na mwenendo wa serikali ya CCM. Kionekancho mbele yao ni kwamba serikali inafanya kiini macho tu ili ionekane kuwa inajali masuala ya kidemokrasia na utu wa binadamu wakati katika uhalisia wake ni hadaa tupu mbele ya dunia.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Mulamula aliwabipu kwa mkwara eti wasifike mahakamani kufuatilia kesi ya Mbowe. Jamaa sasa wanaanza kupiga
 
Serikali iliyoko madarakani siyo halali. Siyo halali kuanzia huko serikali za mitaa hadi serikali kuu. Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 ulikuwa feki na uchaguzi mkuu wa 2020 ulikuwa wizi mtupu. Serikali inaigiza tu kwamba ni halali
 
Sasa itakuaje? Zile NGO zao Danida etc.

CRDB kama nawaona vle....[emoji112]
 
Toka JPM aingie madarakani, haikutokea hata mara moja kufanya ziara ya kikazi katika mojawapo wa nchi za Ulaya kama Denmark licha ya wao kuwa ndiyo wadau wakubwa wa maendeleo ya nchi hii. Kidiplomasia hii inatoa picha kuwa serikali ni "maskini jeuri" yaani misaada yao tunaihitaji kwa udi na uvumba lakini vipaumbele vyao hatujali.

Wito kwa Madam President SSH, aanze kufanya ziara chache katika nchi kama Denmark kwa ajili ya kuimarisha masuala ya kidiplomasia na kimataifa. Achane na ziara za nchi kama Burundi, Rwanda na Visiwa vya Komoro. Huko anaweza kumtuma Makamu wa Rais ili naye awe "busy" kidogo kuliko kumwacha siku zote kukaa kama "figurehead"
 
Back
Top Bottom