Yes mkuu alicho fanya Papa Yohana ni kitu cha kupendeza sana. Ina furahisha pale mtu anapo kiri makosa na kuomba msamaha. Hakuna dhambi kubwa kama kutenda dhambi na kutetea dhambi hiyo. Na pia ina pendeza wana JF wakiongea kwa ustarabu bila jaziba na kutoa hoja badala ya hisia tu.
Nakubaliana na usemi wako kuwa ni jambo zuri kujadili mambo haya na kwamba mengine yaliyotokea kwa makundi mengine hayo ni mambo mengine au tofauti. Lakini sisi waafrika tunatakiwa tuwe tunayaangalia mambo yaliyowasibu Babu zetu na Bara zima la Afrika kwanza kabla ya kukubali haya ya juzi. Babu zetu zaidi ya milioni mia sita walichukuliwa utumwa na wengi sana waliuwawa kikatili na miili yao kutupwa baharini. Dada zetu walifanyiwa vitu vya kishenzi kama wanyama. Waarabu walichukua watumwa wengi sana lakini hawaonekani hata mmoja aliyesalia arabuni, je waienda wapi? Nani lini ataomba msamaha? Ingebidi tuanzie hilo la siku nyingi zaidi na lilillohusu watu wengi zaidi ndipo turejee kwa milini sita ya juzi.