Yaani mkuu una mke na bado unakuwa depressed?
Sasa mkuu kama hujamshirikisha mkeo nashauri umshirikishe na umwambie kila kitu, mke ndio mtu pekee anayekujua vizuri na ndio mtu pekee atakayekupa faraja ya kweli kwenye nyakati ngumu za maisha ili upambane zaidi na hilo ndio dhumuni kuu la ndoa. na hapo ndipo nguvu ya mwanamke inapoonekana na hilo ndio lengo kuu la uwepo wa mwanamke duniani.
Lakini kwa kuwa umekuja huku kwa wanaume wenzako basi tambua tu utapata ukweli na uhalisia mchungu wa maisha, trust me niliwahi kuwa na matatizo makubwa tena ya kutisha ambayo yangekukuta wewe mkuu bila shaka ungekuwa kichaa. hayo yako ni madogo sana. tena mimi hakuna aliyenionea huruma wala kunisadia chochote hata pole na ikawa kama mimi ndio mwenye makosa wakati ni innocent lakini sikukaa chini kulialia na kuomba faraja NO. nilipigana kwa hasira na uchungu. I fought back even harder.
Naona unaomba neno la faraja, binafsi sikuonei huruma wala kukupa pole kama kila mtu anavyofanya au kukupa moyo kwamba mungu atakusaidia ili upate nguvu ya kupambana, sababu nguvu ya kupambana inatakiwa kutoka ndani ya mtu binafsi yeye mwenyewe na sio kwa watu wengine. wewe ulizaliwa peke yako na utakufa peke yako sasa vipi hawa watu wanaokupa pole na kukufariji sasa hivi wakiwa hawapo? utafanya nini? je utajiua? au utalia?
Sikuonei huruma sababu najua matatizo ni sehemu ya maisha na uchungu wa maisha ndio maana ya maisha na najua jinsi gani dunia ilivyo mbaya na katili na watu walivyo wabaya na wanafiki wenye dhuruma isiyoelezeka. ni Survival of the fittest, dhaifu watakanyagwa na wenye nguvu, na wenye nguvu pekee ndio watakaobaki.
Sasa nakwambia ukweli na uhalisa wa maisha man to man.
Ni kwamba mwanaume hakimbii matatizo wala kulialia na kujiua alafu kuacha familia yake iteketee peke yake.
Ni muoga, mpumbavu na mjinga pekee anayeweza kuchukua mtoto wa watu kutoka kwao kwenye maisha ambayo labda yalikuwa mazuri alafu kumzalisha watoto na kumpa mzigo mzito na yeye mwenyewe kujiua au kufa kwa depression na kuacha huyo mwanamke na maumivu makali na majuto juu yako, kitu kichungu zaidi ni kwamba bila shaka mkeo ataolewa tena na mwanaume mwingine ambaye atalea familia yako. je uko tayari kuona watoto wako na mkeo wakilelewa na mwanaume mwengine? mwanaume mwenzako?
Mimi sijui.
Kama ulikuwa unaona wewe hauna uwezo wa kujipambania na kumpambania huyo mwanamke basi usingemuoa ungesubiri kufa peke yako, lakini hapana, ulioa sababu uliamnini ungeweza kumuhudumia.
Sasa thibitisha hilo au kila nilichokiandika mimi hapa kitakuja kutokea kweli, na kwakua hatujuani basi tambua wala sikutanii mkuu.
Mwanaume anatakiwa kutokata tamaa na sio kulialia kwa kuomba faraja na kutaka huruma, anatakiwa kusimamia misimamo yake na kamwe isiyumbishwe wala kuvunjwa na yoyote yule. atapambana na kupigana mpaka tone la jasho la mwisho la ushindi.
Kaa chini fikiria kwa makini na ufanye unachoona kinafaa kwako na familia yako na kuwa tayari kupokea matokeo mabaya yasiyofurahisha. baba ndio tegemo la familia wewe ukiwa dhaifu je mkeo na wanao wawe vipi na wafanye nini?
Siku zote tambua maisha hayako fair na hakuna atakayekuonea huruma, matatizo yapo ili yatatuliwe na sio kuyakimbia au yatakukimbiza na kukumaliza wewe.
Binafsi sipendi kuomba ushauri wala sijawahi kuomba ushauri sababu ninakuwa na uhakika na maamuzi yangu siku zote na sitokubali mtu yoyote aniamulie au aniambie nini cha kufanya japo nitamsikiliza mama na mke wangu pekee kwa asilimia 1%, namaanisha 1% kama ilivyo.
Kuna Mwanaume anaitwa Horatius, yeye alisimama katikati ya daraja peke yake dhidi ya jeshi zima.
Namaliza na alichokisema.
"To every man upon this earth Death cometh soon or late. And how can a man die better Than facing fearful odds, For the ashes of his fathers, And the temples of his Gods.”