Depression Itaniua

Depression Itaniua

Habari za leo wana GT.

Niende kwenye hoja ya msingi.
Kwa utambulisho huu mimi si mgeni humu ila ID nliyotumia ni mpya niliona nifungue hii ili nisiwezekujulikana na wanaoifahamu ID yangu iliyozoeleka hasa mke wangu.

Kwa hakika hapa nilipo nina msongo wa mawazo unanisumbua na ninahisi ninapoelekea sio pazuri, Miaka mitano nyuma nilichukua mkopo kwenye bank moja hivi hapa nchini. Huu mkopo nilichukua kwa udhamini wa mshahara wangu wa kipindi kile.

Kuna jambo lilitokea ofisini hivyo ilinibidi ni resign ndani ya 24hrs hivyo sikupata chochote pale ofisni, (hii nitakuja kuisimulia siku nyingine) lakini nilijipa moyo kuwa maisha hayatonisumbua kwa vile ile pesa nilianzsiha miradi mbalimbali.

Lakini bila kujua kuwa sina uzoefu na usimamizi wa hii miradi yangu niliingia kichwa kichwa mambo yalianza kwenda mrama. Miradi iliyumba mingine niliifunga ilinibidi niuzie gari yangu niweze kusimama tena , lakini bado kama vile nilijiongezea dhiki tu.

Sasa nina miezi 10 sijapeleka rejesho la bank, na bank wanapiga simu sana mpaka waliniambia nijitahidi niweke chochote kile ili nisiwekwe kwenye blacklist. Watoto wangu nimewarudisha shule za Kayumba, hela ya kula imekuwa changamoto kiasi kwamba natamani hata kufa ili nisione hawa watoto wangu wanavyoteseka.

Nafikiri niuze nyumba hii moja niliyobaki nayo ili tu nijaribu tena bahati yangu kwenye biashara zingine lakini nahofia hiyo biashara ikifilisika hawa watoto nitawaweka wapi.

Hofu kubwa niliyonayo ni hawa watu wa hii taasisi ya bank nao wasije wakaniuzia nyumba yangu maana nimeshavurugwa mpaka kila ninalowaza naona haliwezekani.

Kwa upande mwingine naendelea kutafuta kazi nimeshafanya interview sehemu nyingi tu lakini sijabahatika kuitwa, miezi mitatu iliyopita interview yangu ya mwisho niliambiwa nitaitwa kwa ajili ya kuanza kazi mwezi wa saba au wa nane. Lakini mpaka sasa hivi sioni faraja yoyote ile ya kuitwa kwenye hiyo taasisi ya kimataifa.

Wana GT naomba neno la faraja kutoka kwenu nifanyaje ili niweze kumudu hizi heka heka za maisha na hasira za watu wa bank wasije kunipeleka mahakamani na kunifilisi.
If it is serious mkopo wa mfanyakaz hauwez uza nyumba dhamana yake ni ajira
 
Stay Strong....

When You I start feeling sick of it all,
It helps you remember your a brick in a wall, who runs down from the hillside to the sea, when you start feeling that it's gone too far, lie on your back and stare up at the stars, Wonder if they're staring back at You.
 
Yaani mkuu una mke na bado unakuwa depressed?
Sasa mkuu kama hujamshirikisha mkeo nashauri umshirikishe na umwambie kila kitu, mke ndio mtu pekee anayekujua vizuri na ndio mtu pekee atakayekupa faraja ya kweli kwenye nyakati ngumu za maisha ili upambane zaidi na hilo ndio dhumuni kuu la ndoa. na hapo ndipo nguvu ya mwanamke inapoonekana na hilo ndio lengo kuu la uwepo wa mwanamke duniani.

Lakini kwa kuwa umekuja huku kwa wanaume wenzako basi tambua tu utapata ukweli na uhalisia mchungu wa maisha, trust me niliwahi kuwa na matatizo makubwa tena ya kutisha ambayo yangekukuta wewe mkuu bila shaka ungekuwa kichaa. hayo yako ni madogo sana. tena mimi hakuna aliyenionea huruma wala kunisadia chochote hata pole na ikawa kama mimi ndio mwenye makosa wakati ni innocent lakini sikukaa chini kulialia na kuomba faraja NO. nilipigana kwa hasira na uchungu. I fought back even harder.

Naona unaomba neno la faraja, binafsi sikuonei huruma wala kukupa pole kama kila mtu anavyofanya au kukupa moyo kwamba mungu atakusaidia ili upate nguvu ya kupambana, sababu nguvu ya kupambana inatakiwa kutoka ndani ya mtu binafsi yeye mwenyewe na sio kwa watu wengine. wewe ulizaliwa peke yako na utakufa peke yako sasa vipi hawa watu wanaokupa pole na kukufariji sasa hivi wakiwa hawapo? utafanya nini? je utajiua? au utalia?

Sikuonei huruma sababu najua matatizo ni sehemu ya maisha na uchungu wa maisha ndio maana ya maisha na najua jinsi gani dunia ilivyo mbaya na katili na watu walivyo wabaya na wanafiki wenye dhuruma isiyoelezeka. ni Survival of the fittest, dhaifu watakanyagwa na wenye nguvu, na wenye nguvu pekee ndio watakaobaki.

Sasa nakwambia ukweli na uhalisa wa maisha man to man.
Ni kwamba mwanaume hakimbii matatizo wala kulialia na kujiua alafu kuacha familia yake iteketee peke yake.
Ni muoga, mpumbavu na mjinga pekee anayeweza kuchukua mtoto wa watu kutoka kwao kwenye maisha ambayo labda yalikuwa mazuri alafu kumzalisha watoto na kumpa mzigo mzito na yeye mwenyewe kujiua au kufa kwa depression na kuacha huyo mwanamke na maumivu makali na majuto juu yako, kitu kichungu zaidi ni kwamba bila shaka mkeo ataolewa tena na mwanaume mwingine ambaye atalea familia yako. je uko tayari kuona watoto wako na mkeo wakilelewa na mwanaume mwengine? mwanaume mwenzako?
Mimi sijui.

Kama ulikuwa unaona wewe hauna uwezo wa kujipambania na kumpambania huyo mwanamke basi usingemuoa ungesubiri kufa peke yako, lakini hapana, ulioa sababu uliamnini ungeweza kumuhudumia.
Sasa thibitisha hilo au kila nilichokiandika mimi hapa kitakuja kutokea kweli, na kwakua hatujuani basi tambua wala sikutanii mkuu.

Mwanaume anatakiwa kutokata tamaa na sio kulialia kwa kuomba faraja na kutaka huruma, anatakiwa kusimamia misimamo yake na kamwe isiyumbishwe wala kuvunjwa na yoyote yule. atapambana na kupigana mpaka tone la jasho la mwisho la ushindi.

Kaa chini fikiria kwa makini na ufanye unachoona kinafaa kwako na familia yako na kuwa tayari kupokea matokeo mabaya yasiyofurahisha. baba ndio tegemo la familia wewe ukiwa dhaifu je mkeo na wanao wawe vipi na wafanye nini?
Siku zote tambua maisha hayako fair na hakuna atakayekuonea huruma, matatizo yapo ili yatatuliwe na sio kuyakimbia au yatakukimbiza na kukumaliza wewe.

Binafsi sipendi kuomba ushauri wala sijawahi kuomba ushauri sababu ninakuwa na uhakika na maamuzi yangu siku zote na sitokubali mtu yoyote aniamulie au aniambie nini cha kufanya japo nitamsikiliza mama na mke wangu pekee kwa asilimia 1%, namaanisha 1% kama ilivyo.

Kuna Mwanaume anaitwa Horatius, yeye alisimama katikati ya daraja peke yake dhidi ya jeshi zima.
Namaliza na alichokisema.
"To every man upon this earth Death cometh soon or late. And how can a man die better Than facing fearful odds, For the ashes of his fathers, And the temples of his Gods.”
Huu sasa ndo ushauri wa mwanamume na sio mwanaume. Kabisa kwenye misukosuko ni muhimu kuusikiliza moyo wako na Mungu tu na sio kuwayawaya na ushauri,utapotea. Situation hiyo mm ni witness.
 
Pole Sana tofauti yako na Mimi ni namna ulivopata mkopo dhamana yako ni ajira Mimi niliweka nyumba Kama dhamana ya mkopo kilichofata niliangukia pua mkopo wa tatu madalali wa bank walinisumbua mnoo ikafika hatua nakoswakoswa kugongwa na gari barabarani nawaza marejesho,wife akarudi kwao na mwanangu mzuri mmoja binti yangu nikabaki mwenyewe ilikuwa ijumaa saa kumi na nusu nikasikia gari la matangazo wanatangaza nyumba yangu nilitetemeka nilipokuwa maana nilikuwa najua Kila kitu usiku huo huo liliandaliwa zuio la mahakama jumamosi saa tatu washaweka meza wanataka kuuza nyumba na majirani wamezunguka kushangaa mnada madalali wakaambiwa branch manager nmb kasaini wito wa mahakama tayari hakuna kuuza nyumba inazuio la mahakama kuanzia siku hiyo sikusumbuliwa na simu wala vitisho vya madalali wa bank kesi ikaenda mahakama ya ardhi mwanasheria akasimamia Mimi nikapata chance ya kuja dar kutuliza ubongo nikapata gepu mda huu nalipa kidogo kidogo wife nishamrudisha na binti yangu napambana wao wapo kwenye nyumba yetu yenye zuio la mahakama napambana tuu japo haikuwa rahisi
Ombi, usiuze nyumba yako kizembe
 
Hajafukuzwa kazi ameresign 24hrs
Whether ume resign ama umefukuzwa kazi ni wajibu wa insurance kulipa.

Kwani wakati anachukua mkopo kuna mahala walikubaliana asiache kazi ama kufukuzwa ndani ya muda flani?

Insurance kazi yake ni kumlinda mtoa mkopo dhidi ya hali yoyote itakayojitokeza hapo mbele.

Ndio maana kabla bank hawajakupa mkopo kwanza wanafanya credit profiling and credit worth ness yako kuona kama they can take the risk of lending you their money.

Hakuna bank inakupa mkopo kwa kuamini kwamba hutaacha kazi ama. Hakuna imani hapo.

So ni wajibu wa bank kujilinda ama kulinda pesa yao kwa hali yoyote itakayojitokeza huko mbele.

Kusema kwamba bima haikingi kuacha kazi ni sawa na useme unakata bima ya gari lakini unakinga dhidi ya ajali ya kugongwa na fuso ila ajali nyingine sawa tu.
 
Kama ulichukua Mkopo Bank kwa Udhamini wa Mshahara wako iweje Bank waje wauze Nyumba yako??Dhamana yako wewe ni Ofisi ndio iliyokudhamini hivyo Bank hawawezi kuwa na Hati ya Nyumba yako
Mikopo ya hivyo ipo inaitwa personal loan unaweka collateral Nyumba Yako lakn mshahara wako ndo marejesho.Kwa kifupi Ofisi Yao haikuzamini hyo mikopo .

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Kama ulichukua Mkopo Bank kwa Udhamini wa Mshahara wako iweje Bank waje wauze Nyumba yako??Dhamana yako wewe ni Ofisi ndio iliyokudhamini hivyo Bank hawawezi kuwa na Hati ya Nyumba yako

Muwe mnasoma na kuelewa kwanza acha mihemko.
 
Umejificha kwa codes ila tumeshakujua .

Si uliacha kazi kwa mbwembwe na kiburi sasa unakuja kulialia humu nini? Ngoja sasa watu waanze kukugongea mkeo ndo utajua hujui halafu ule mpango wa kujifanya kushindana na majirani zako kimaisha ni ubwege wa kittoto psmbana fwala wewe na bado utaomba poooh.
 
Habari za leo wana GT.

Niende kwenye hoja ya msingi.
Kwa utambulisho huu mimi si mgeni humu ila ID nliyotumia ni mpya niliona nifungue hii ili nisiwezekujulikana na wanaoifahamu ID yangu iliyozoeleka hasa mke wangu.

Kwa hakika hapa nilipo nina msongo wa mawazo unanisumbua na ninahisi ninapoelekea sio pazuri, Miaka mitano nyuma nilichukua mkopo kwenye bank moja hivi hapa nchini. Huu mkopo nilichukua kwa udhamini wa mshahara wangu wa kipindi kile.

Kuna jambo lilitokea ofisini hivyo ilinibidi ni resign ndani ya 24hrs hivyo sikupata chochote pale ofisni, (hii nitakuja kuisimulia siku nyingine) lakini nilijipa moyo kuwa maisha hayatonisumbua kwa vile ile pesa nilianzsiha miradi mbalimbali.

Lakini bila kujua kuwa sina uzoefu na usimamizi wa hii miradi yangu niliingia kichwa kichwa mambo yalianza kwenda mrama. Miradi iliyumba mingine niliifunga ilinibidi niuzie gari yangu niweze kusimama tena , lakini bado kama vile nilijiongezea dhiki tu.

Sasa nina miezi 10 sijapeleka rejesho la bank, na bank wanapiga simu sana mpaka waliniambia nijitahidi niweke chochote kile ili nisiwekwe kwenye blacklist. Watoto wangu nimewarudisha shule za Kayumba, hela ya kula imekuwa changamoto kiasi kwamba natamani hata kufa ili nisione hawa watoto wangu wanavyoteseka.

Nafikiri niuze nyumba hii moja niliyobaki nayo ili tu nijaribu tena bahati yangu kwenye biashara zingine lakini nahofia hiyo biashara ikifilisika hawa watoto nitawaweka wapi.

Hofu kubwa niliyonayo ni hawa watu wa hii taasisi ya bank nao wasije wakaniuzia nyumba yangu maana nimeshavurugwa mpaka kila ninalowaza naona haliwezekani.

Kwa upande mwingine naendelea kutafuta kazi nimeshafanya interview sehemu nyingi tu lakini sijabahatika kuitwa, miezi mitatu iliyopita interview yangu ya mwisho niliambiwa nitaitwa kwa ajili ya kuanza kazi mwezi wa saba au wa nane. Lakini mpaka sasa hivi sioni faraja yoyote ile ya kuitwa kwenye hiyo taasisi ya kimataifa.

Wana GT naomba neno la faraja kutoka kwenu nifanyaje ili niweze kumudu hizi heka heka za maisha na hasira za watu wa bank wasije kunipeleka mahakamani na kunifilisi.
Wewe hao bank achana nao ofisi yako ndio mdhamini watamalizana wenyewe wewe focus kwenye mambo ya msingi sasa
 
Ulikopa Kwa dhamana ya mshahara na sasa ile kazi umeipoteza hivyo huwez kurejesha mkopo aidha hiyo bank Haina Cha kukufanya maana ile dhamana haipo tena.wewe huna tofauti na walotumbuliwa vyeti feki.wew jutuluze waeleze huna uwezo wa kulipia..watakusumbua tu ila hawana Cha kukufanya so tulia jipange vizuri ndo maana mikopo hukatiwa bima ni hasara yao
 
Habari za leo wana GT.

Niende kwenye hoja ya msingi.
Kwa utambulisho huu mimi si mgeni humu ila ID nliyotumia ni mpya niliona nifungue hii ili nisiwezekujulikana na wanaoifahamu ID yangu iliyozoeleka hasa mke wangu.

Kwa hakika hapa nilipo nina msongo wa mawazo unanisumbua na ninahisi ninapoelekea sio pazuri, Miaka mitano nyuma nilichukua mkopo kwenye bank moja hivi hapa nchini. Huu mkopo nilichukua kwa udhamini wa mshahara wangu wa kipindi kile.

Kuna jambo lilitokea ofisini hivyo ilinibidi ni resign ndani ya 24hrs hivyo sikupata chochote pale ofisni, (hii nitakuja kuisimulia siku nyingine) lakini nilijipa moyo kuwa maisha hayatonisumbua kwa vile ile pesa nilianzsiha miradi mbalimbali.

Lakini bila kujua kuwa sina uzoefu na usimamizi wa hii miradi yangu niliingia kichwa kichwa mambo yalianza kwenda mrama. Miradi iliyumba mingine niliifunga ilinibidi niuzie gari yangu niweze kusimama tena , lakini bado kama vile nilijiongezea dhiki tu.

Sasa nina miezi 10 sijapeleka rejesho la bank, na bank wanapiga simu sana mpaka waliniambia nijitahidi niweke chochote kile ili nisiwekwe kwenye blacklist. Watoto wangu nimewarudisha shule za Kayumba, hela ya kula imekuwa changamoto kiasi kwamba natamani hata kufa ili nisione hawa watoto wangu wanavyoteseka.

Nafikiri niuze nyumba hii moja niliyobaki nayo ili tu nijaribu tena bahati yangu kwenye biashara zingine lakini nahofia hiyo biashara ikifilisika hawa watoto nitawaweka wapi.

Hofu kubwa niliyonayo ni hawa watu wa hii taasisi ya bank nao wasije wakaniuzia nyumba yangu maana nimeshavurugwa mpaka kila ninalowaza naona haliwezekani.

Kwa upande mwingine naendelea kutafuta kazi nimeshafanya interview sehemu nyingi tu lakini sijabahatika kuitwa, miezi mitatu iliyopita interview yangu ya mwisho niliambiwa nitaitwa kwa ajili ya kuanza kazi mwezi wa saba au wa nane. Lakini mpaka sasa hivi sioni faraja yoyote ile ya kuitwa kwenye hiyo taasisi ya kimataifa.

Wana GT naomba neno la faraja kutoka kwenu nifanyaje ili niweze kumudu hizi heka heka za maisha na hasira za watu wa bank wasije kunipeleka mahakamani na kunifilisi.
Kwa nini u resign bila kufukuzwa Kazi? Hukujua yajayo kuwa hayafurahishi?

Mkuu jiajiri tuu na pole Sana.
 
Back
Top Bottom