Depression Itaniua

Depression Itaniua

Tuseme tu pole.

Mikopo ya benki inatesa sana, kwa hii miezi ambayo hujapeleka rejesho riba ya adhabu itakuwa imeshapaa.

Ungeweza uza hiyo nyumba ulipe deni la watu, kiasi kinachobaki kikusogeze, pole
ushauri wa hovyo mkopo wa mshahara hauuzi dhamana yoyote bwana GT relax wambie benki ulichokuwa unakitegemea niu mshahara ambao huna ...usiuze nyumba kwa ajili ya kulipa mkopo pia usiogope kuwekwa kwenye blacklist relax brother
 
Pole sana mkuu, endelea kutafuta kazi sehemu mbalimbali, cha msingi usiuze nyumbani bora ukaze hivyo hivyo tu mtaan mambo yatabadlika mbele kwa mbele.
 
Habari za leo wana GT.

Niende kwenye hoja ya msingi.
Kwa utambulisho huu mimi si mgeni humu ila ID nliyotumia ni mpya niliona nifungue hii ili nisiwezekujulikana na wanaoifahamu ID yangu iliyozoeleka hasa mke wangu.

Kwa hakika hapa nilipo nina msongo wa mawazo unanisumbua na ninahisi ninapoelekea sio pazuri, Miaka mitano nyuma nilichukua mkopo kwenye bank moja hivi hapa nchini. Huu mkopo nilichukua kwa udhamini wa mshahara wangu wa kipindi kile.

Kuna jambo lilitokea ofisini hivyo ilinibidi ni resign ndani ya 24hrs hivyo sikupata chochote pale ofisni, (hii nitakuja kuisimulia siku nyingine) lakini nilijipa moyo kuwa maisha hayatonisumbua kwa vile ile pesa nilianzsiha miradi mbalimbali.

Lakini bila kujua kuwa sina uzoefu na usimamizi wa hii miradi yangu niliingia kichwa kichwa mambo yalianza kwenda mrama. Miradi iliyumba mingine niliifunga ilinibidi niuzie gari yangu niweze kusimama tena , lakini bado kama vile nilijiongezea dhiki tu.

Sasa nina miezi 10 sijapeleka rejesho la bank, na bank wanapiga simu sana mpaka waliniambia nijitahidi niweke chochote kile ili nisiwekwe kwenye blacklist. Watoto wangu nimewarudisha shule za Kayumba, hela ya kula imekuwa changamoto kiasi kwamba natamani hata kufa ili nisione hawa watoto wangu wanavyoteseka.

Nafikiri niuze nyumba hii moja niliyobaki nayo ili tu nijaribu tena bahati yangu kwenye biashara zingine lakini nahofia hiyo biashara ikifilisika hawa watoto nitawaweka wapi.

Hofu kubwa niliyonayo ni hawa watu wa hii taasisi ya bank nao wasije wakaniuzia nyumba yangu maana nimeshavurugwa mpaka kila ninalowaza naona haliwezekani.

Kwa upande mwingine naendelea kutafuta kazi nimeshafanya interview sehemu nyingi tu lakini sijabahatika kuitwa, miezi mitatu iliyopita interview yangu ya mwisho niliambiwa nitaitwa kwa ajili ya kuanza kazi mwezi wa saba au wa nane. Lakini mpaka sasa hivi sioni faraja yoyote ile ya kuitwa kwenye hiyo taasisi ya kimataifa.

Wana GT naomba neno la faraja kutoka kwenu nifanyaje ili niweze kumudu hizi heka heka za maisha na hasira za watu wa bank wasije kunipeleka mahakamani na kunifilisi.
Kwanza pole lakini kwa mtazamo wa baadhi ya thinkers kuwa nyumba yako haipo kwenye risk naona kuna ukakasi, hivi ofisi yako ilijulishwa kuwa salary yako ndio dhamana ya huo mkopo ? Na endapo ungepunguziwa mshahara hadi kiwango cha robo hiyo bank wangekusanya vp marejesho yao na wewe ungeishije ...inaonesha uliachishwa kazi na bilashaka ulifanya makosa makubwa tuache hilo lakini ushauri wa kuuza hiyo nyumba upo positive zaidi ila kabla ya jaribio la kuiuza Waone wanasheria wa mambo ya fedha wakupe ushauri mzuri pia tubia hilo kosa lililosababisha ukaachishwa kazi Mungu ni wa msamaha usiwe na shingo ngumu .
 
Umejificha kwa codes ila tumeshakujua .

Si uliacha kazi kwa mbwembwe na kiburi sasa unakuja kulialia humu nini? Ngoja sasa watu waanze kukugongea mkeo ndo utajua hujui halafu ule mpango wa kujifanya kushindana na majirani zako kimaisha ni ubwege wa kittoto psmbana fwala wewe na bado utaomba poooh.
Dah mkuu utamfanya mtu ajiue jamani.
Kwa Leo mpunguzie maneno makali ni binadam mwenzetu
 
Dah mkuu utamfanya mtu ajiue jamani.
Kwa Leo mpunguzie maneno makali ni binadam mwenzetu
Jinga hilo acha likufe tu mimi nshaligundua japo linajificha unaacha aje kazi kwa sabqbu ya mwajiri kukuhamisha kituo? Hiyo ni akili ngoja mkeo aanze uliwa na wajanja ndo utajuahujui fwala wewe unaenda uwatesa watoto bure kwa sababu ya ubwege wKo .
 
Pole sana mkuu, ninayo picha ya unayoyapitia.
Ninayo mawili tu la kukushauri;
1. USIUZE NYUMBA. Hii usiifanye kwa ajili ya kulipia mkopo wala kuanzishia viashara, najua familia inakuangalia wewe lakini Mungu yupo utapata mlango wa kutokea katika hili zito.
2. Endapo benki watakupeleka mahakamani na wakataka kuuza nyumba yako nipigie ama nicheki PM nitakusaidia kukupa mbinu za kuwasumbua hadi watakata tamaa wenyewe kuipata hiyo nyumba. Ni mbinu za kisheria tu hawataambulia chochote.
So usije ukauza nyumba ukiogopa kuwa itachukuliwa na benki, relax waache familia yako waendelew kuishi na wewe endelea kukomaa.
 
Mkuu naomba kuku uliza,kwasasa hauna kazi unayofanya najua unatamani kufanya kazi

upate chochote kitu ili maisha yaende,naomba kujua hapo ulipo unatamani kupata kazi

ya kukupa kiasi gani kwa mwezi (ikitokea mtu anakuajiri),hebu niambie nijue unatamani

malipo ya kiasi gani kwa mwezi,huwezi jua kuna mtu yupo humu anatafuta Mfanyakazi ila

anashindwa kukwambia maana anahofia labda unataka malipo makubwa,be free kuwa muwazi

sema posho unayoifikiria itakutosha, isiwe chini ya kiasi gani kwa siku au kwa mwezi.
 
Back
Top Bottom