Dereva aliyetajwa na Makonda kufanya uhalifu afikishwe kwenye vyombo vya sheria

Dereva aliyetajwa na Makonda kufanya uhalifu afikishwe kwenye vyombo vya sheria

MGOGOHALISI

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2011
Posts
3,294
Reaction score
4,920
Nimeona clip ikisambaa mitandaoni inayomwonyesha aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam mheshimiwa Paul Makonda akimtuhumu mmoja wa aliyewahi kuwa msaidizi wake kuwa alikua akichukua gari na kwenda kupora kwenye biashara za watu. Kwa kuwa uporaji ni jinai na jinai haifi ni wakati muafaka kwa jamhuri kuchukua hatua stahiki. Ifunguliwe kesi aitwe makonda ili mtu huyo ajulikane na haki itendeke.

Pia soma: Makonda: Dereva wangu alikuwa anafunga namba za RC DSM na kutapeli watu

Ikumbukwe kuwa Paul Makonda amekua akihusishwa na vitendo vya kihalifu kipindi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na inaaminika hata kuwekwa pembeni ilikua ni mkakati wa kuwatuliza walalamikaji. Kwa kutoka kwake Paul Makonda na kutamka hadharani kuwa ni msaidizi wake alikua akifanya vitendo hivyo nitashangaa kama jamhuri kupitia mwendesha mashtaka watakaa kimya.
 
Dereva hawezi kutafutwa kama hakuna mlalamikaji alieenda kufungua kesi
 
Back
Top Bottom