Kwa sasa, jiji la Dar es salaam linakabiliwa na foleni za magari. Kutoka pembeni mwa mji mji kuja katikati yanatumika masaa kama 3 kwa wastani, ambapo ni sawa na muda wa kutoka Dar kwenda Morogoro.
Katika hali kama hii, tulitegemea serikali kufanya kila linalowezekana katika kukabiliana na foleni hizi ambazo zina athari kubwa sana kwetu kiuchumi. Mfano tulitegemea kwa wakati wa Peak hours service road zitumike ili kupunguza foleni.
Cha ajabu ni pale tunaposhuhudia pale barabara zinapofunga kabisa traffic wanasambaa kwenye service roda kuzuia watu wasitumie njia hizi.
Yawezekana wengine wakadai uwezo wa service road ni mdogo lakini inakuwaje barabara hizi zinatumika kama parking za malori ya mizigo yenye uzito mkubwa na zisitumike kwa kupitisha vi saloon car.
Nashindwa kuelewa kama kweli ndani ya serikali wote wanashirikiana kukabiliana na changamoto inayotokea? Au kila mmoja ana mambo yake na tatizo likiwa la huyu basi wengine wanalitumia kutafuta mapato na kufanya tatizo kuwa kubwa zaidi.
Swala la foleni limeachiwa wizara moja tu lakini halmashauri hazionekani kulipa kipaumbele swala la foleni ili na wao kwenye mipango yao barabara za kusaidia kuondoa foleni ndio na wao wanazipa kipaumbele katika bajeti zao, wanaosimamia usalama barabarani kunapotokea foleni wao ndio wawe mstari wa mbele kuwaonyesha watumiaji wa barabara njia zipi zinaweza kutumika kwa dharura.