Dereva anayepita service road anavunja sheria gani?

Dereva anayepita service road anavunja sheria gani?

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Kwa sasa, jiji la Dar es salaam linakabiliwa na foleni za magari. Kutoka pembeni mwa mji mji kuja katikati yanatumika masaa kama 3 kwa wastani, ambapo ni sawa na muda wa kutoka Dar kwenda Morogoro.

Katika hali kama hii, tulitegemea serikali kufanya kila linalowezekana katika kukabiliana na foleni hizi ambazo zina athari kubwa sana kwetu kiuchumi. Mfano tulitegemea kwa wakati wa Peak hours service road zitumike ili kupunguza foleni.

Cha ajabu ni pale tunaposhuhudia pale barabara zinapofunga kabisa traffic wanasambaa kwenye service roda kuzuia watu wasitumie njia hizi.

Yawezekana wengine wakadai uwezo wa service road ni mdogo lakini inakuwaje barabara hizi zinatumika kama parking za malori ya mizigo yenye uzito mkubwa na zisitumike kwa kupitisha vi saloon car.

Nashindwa kuelewa kama kweli ndani ya serikali wote wanashirikiana kukabiliana na changamoto inayotokea? Au kila mmoja ana mambo yake na tatizo likiwa la huyu basi wengine wanalitumia kutafuta mapato na kufanya tatizo kuwa kubwa zaidi.

Swala la foleni limeachiwa wizara moja tu lakini halmashauri hazionekani kulipa kipaumbele swala la foleni ili na wao kwenye mipango yao barabara za kusaidia kuondoa foleni ndio na wao wanazipa kipaumbele katika bajeti zao, wanaosimamia usalama barabarani kunapotokea foleni wao ndio wawe mstari wa mbele kuwaonyesha watumiaji wa barabara njia zipi zinaweza kutumika kwa dharura.
 
Labda kwanza tafuta maana ya 'service road' kisha rudi tena hapa
 
Mtoa thread hii unatakiwa kujua kwanza tofauti ya barabara kubwa,za kati na service road,kisha tuanze mjadala
 
nashangaa the way we are judging things kwa maana katika dharura hata pori linaweza kuwa barabara haijalishi definition ya pori inasemaje.

tunaongelea tatizo la foleni za dar, sijui kama kuna logic kustick kwenye definition.

hapa tunachohitaji ni logic je kwa foleni za dar barabara zinapofunga service load zitumike kama njia kuu au la na anayechangia atoe logic behind kwa sababu swala la definition halina logic.

Labda kwanza tafuta maana ya 'service road' kisha rudi tena hapa
 
Sasa magari yakipita service road waenda kwa miguu na walemavu watapita wapi?
 
nadhani hatujaelewana maana ukipita mfano barabara ya nyerere, mandela, morogoro pembeni ya barabara kuna kuna barabara ndogo ambazo zinatumika kwa magari ambazo ni kama barabara za kutoa huduma katika maeneo hayo.

unataka kuingia mtaa au sehemu fulani unatoka barabara kuu unaingia barabara hizi ndogo na sio njia za watembea kwa miguu bali ni barabara za kuhudumia maeneo husika.

lakini lipo tatizo kuwa barabara kuu wakati fulani zinazidiwa na magari au wakati mwingine kukitokea tatizo katika barabara fulani na magari mengi yanayoelekea huko yanakuwa hayaendi hivyo kuleta adha kubwa kwa magari kusiamama kwa mda kadhaa kwenye foleni kusubiri tatizo lililotokea huko litatuliwe.

lakini mfano barabara ya mandela kama magari ya kuelekea tazara yanakuwa hayaendi basi magari yanayoelekea mjini yanaweza kupita barabara ya huduma kwa maeneo ya buguruni na kuingia barabara ya uhuru na kuelekea mjini lakini askari wanasimama maeneo ya buguruni na kupiga mkwara magari yaliyopita barabara hii ndogo yarudi yalikotokea.

pale karume barabara ile huwa inafunga sana lakini kuna barabara zenye service raod pembeni ambazo kunapotokea tatizo kama hilo basi traffic wanajificha pembeni.

najiuliza hawa wanaosimama pembeni kuzuia magari kupita barabara hizi ndogo zenye lami je wanasukumwa na kulitumikia taifa au wanasukumwa na ambition zao binafsi?

lakini tujiulize kama taifa tunadhani ni mwiko kupita service road wakati kumetokea jam barabara kuu? wakati service road hizi ni barabara tulizozitengeneza wenyewe kwa rami.

je ni sahihi kuegesha malori ya mizigo kwenye barabara hizi lakini zisitumike kupunguza foleni?

Sasa magari yakipita service road waenda kwa miguu na walemavu watapita wapi?
 
nashangaa the way we are judging things kwa maana katika dharura hata pori linaweza kuwa barabara haijalishi definition ya pori inasemaje.

tunaongelea tatizo la foleni za dar, sijui kama kuna logic kustick kwenye definition.

hapa tunachohitaji ni logic je kwa foleni za dar barabara zinapofunga service load zitumike kama njia kuu au la na anayechangia atoe logic behind kwa sababu swala la definition halina logic.

Sijasema definition, nimesema maana (meaning)... kwa hiyo maana ya kitu inabeba kila kitu isipokua kisichomaanishwa... service road sio kwamba zitasaidia kupunguza foleni kama zikitumika maana sio suluhu ya foleni na kwa taarifa sehemu ya makutano lazima mtu urudi barabara kuu kitu ambacho kinaongeza tatizo kwa wlioko barabara kuu na huko service road pia
 
unatumia theory zaidi ya practical kwa maana si kweli kwamba kwenye junction lazima wote wakutane bali zipo sehemu ambazo kama barabara kuu magari yamesimama magari ambayo hayanyooshi na njia yanaweza kutumia service road na kuingia kwenye njia yao baada ya makutano wakaonda mfano ni barabara ya mandela eneo la junction ya kuelekea tabata na hapo traffic wanaruhusu jambo hilo linafanyika wanaoelekea tabata kutokea buguruni hawana haja ya kusubiri foleni ya kuelekea ubungo.

barabara hiyo hiyo ya mandela wanaotoka ubungo kama wanataka kuelekea karume pale buguruni service road inatoka hawana haja ya kusubiri katika foleni na hapa sizungumzii katika nyakati za kawaida kusubiri dakika tano mpaka kumi.

leo hii asubuhi palepale buguni KCB traffic kasimamisha magari yaliyokuwa yakipita service road anawaambia warudi huko huko wakati wa mbele wanaanza kugeuza mtu mmoja aliyekuwa nyuma kidogo aliovertake tena kwa kupita nje ya barabara na akaja mbele akasalimia na yule traffic akampa mkono akapita na wale waliokuwa wakianza kugeuza sasa wakabaki wamemwangalia traffic na yeye akabadili mawazo hapo akawaambia waingie barabara kubwa.

mambo kama haya ni mengi yanafanyika wazi na sote tunayaona, hivi kweli kupita service road mpaka ufahamiane na askari au mridhishe?

kama hakuna jam barabarani hawa huwaoni kwenye service road sasa hivi kweli kunapotokea jam wanaenda kukamata wahalifu au kutega mitego yao?

maisha yanakuwa magumu pale tu tunaporuhusu mtu mmoja aliyekabidhiwa rungu fulani kulitumia kwa matakwa yake binafsi kwa maana kama atapata faida yeye binafsi na matatizo mtu huyo anaweza kujifanya yuko bize na kazi kumbe anapalilia matatizo ili yamfaidishe.

ni vema wale waliojuu watazame jambo hili na walitolee mwongozo na sio kuwaacha hawa wanaosimama barabarani kujifanya wako serious na kazi kumbe wanachelewesha kazi za wengine na kuathiri uchumi wetu.

Sijasema definition, nimesema maana (meaning)... kwa hiyo maana ya kitu inabeba kila kitu isipokua kisichomaanishwa... service road sio kwamba zitasaidia kupunguza foleni kama zikitumika maana sio suluhu ya foleni na kwa taarifa sehemu ya makutano lazima mtu urudi barabara kuu kitu ambacho kinaongeza tatizo kwa wlioko barabara kuu na huko service road pia
 
mkuu pole na yaliyokukuta nadhani pia umepigwa faini mkuu.

Mie yalinikuta sana barabara ya morogoro ila huwa wakinikamata nawaambia nini maana ya hii barabara na pia waeleze kwa nini hujapita njia kuu ukapita service road.

Mie walinidaka asubuhi niko na wife wakaniambia mbona unapita huku nikawaaambia unaona kile kibao mbele cha lodge ndo naelekea pale sasa nielekeze njia ya kufika pale bila kupita huku wakacheka wakaniachia kumbe wananifuata niliwaona nikaingia kwa hicho kilodge then nikatoka wakaniambia mbona unatoka tena nikawaambia vyumba vimejaa wakaniruhusu kuendelea na service road.
 
kimsingi haya unayoyasema kweli mtu anaweza kujitetea lakini hapa tujadili kuwa wanachokifanya kweli ni sahihi?

barabara kuu magari hayaendi kama kuna magari yanaelekea njia ambazo kwa service road zinafikika kwa nini wasitoke wakaenda?

barabara hizi nyingi zinageuzwa masoko kwa watu kupanga chini nyanya viatu wanauza.

sioni mantiki kwa nini tukae kujitetea kwa askari bali wao wangekuwa wakiona barabara zimefunga wanawaelekeza wananchi njia gani mbadala kupunguza jam barabarani.

na je kwa mtizamo wako hawa wanaozuia kweli wako serious kuzuia wahalifu au wanatafuta rushwa au kutengeneza mazingira ya wao kutenda uhalifu kwa kupokea rushwa.

ni vigumu kuimaliza rushwa lakini hata rushwa za waziwazi ambazo kila mwanajamii anaona ?

mkuu pole na yaliyokukuta nadhani pia umepigwa faini mkuu.Mie yalinikuta sana barabara ya morogoro ila huwa wakinikamata nawaambia nini maana ya hii barabara na pia waeleze kwa nini hujapita njia kuu ukapita service road.Mie walinidaka asubuhi niko na wife wakaniambia mbona unapita huku nikawaaambia unaona kile kibao mbele cha lodge ndo naelekea pale sasa nielekeze njia ya kufika pale bila kupita huku wakacheka wakaniachia kumbe wananifuata niliwaona nikaingia kwa hicho kilodge then nikatoka wakaniambia mbona unatoka tena nikawaambia vyumba vimejaa wakaniruhusu kuendelea na service road.
 
mkuu kwenye hizi barabara kiuhalisia ni kuwa wana haki za kuzuia kwa kuwa hakuna trafiki anayejua lengo la mtu kwenda huko mbele.ila cha msingi mkuu ni kujipanga na kuwaeleza nia yako na wao ni binadamu wanaelewaga sometimes. Ila linapokuja swala la rushwa ni kila mtu anachukua kwa upande wake mathalani kuna njia(service) road kutoka kimara corner/kona hadi ubungo maji ile njia pale kwa mbele iko kama imezibwa ila ukweli haijazibwa ukifika pale wanakuja vijana wanakuambia toa kitu kidogo then wao wenyewe wanatoa lile jiwe unapita na wanalirudisha na imekuwa ndo utaratibu.
kimsingi haya unayoyasema kweli mtu anaweza kujitetea lakini hapa tujadili kuwa wanachokifanya kweli ni sahihi?

barabara kuu magari hayaendi kama kuna magari yanaelekea njia ambazo kwa service road zinafikika kwa nini wasitoke wakaenda?

barabara hizi nyingi zinageuzwa masoko kwa watu kupanga chini nyanya viatu wanauza.

sioni mantiki kwa nini tukae kujitetea kwa askari bali wao wangekuwa wakiona barabara zimefunga wanawaelekeza wananchi njia gani mbadala kupunguza jam barabarani.

na je kwa mtizamo wako hawa wanaozuia kweli wako serious kuzuia wahalifu au wanatafuta rushwa au kutengeneza mazingira ya wao kutenda uhalifu kwa kupokea rushwa.

ni vigumu kuimaliza rushwa lakini hata rushwa za waziwazi ambazo kila mwanajamii anaona ?
 
unajua lipo tatizo nchi hii uchumi tumeugeuza ni uchumi wa ujanja ujanja. ili mtu afanikiwe lazima kufanya utapeli, kupata dili au kutumia madaraka vibaya.

na hili limekuwa ni jambo la kawaida na wale wanaoijifanya kutaka kutafuta kwa kutumia uchapa kazi mifumo ya kuwalinda inawashughulikia na kuwafilisi.

ni lazima tuanzie sehemu tubadili jamii yetu kwani huko tuendako watoto wetu watafilisika maana mataifa makubwa yanaweza kupiga hatua zaidi kwa kutumia ujanja kwetu lakini kwa nchi masikini mkilea ujanja wageni wa nje watakuja na kutumia ujanja huo kuwafilisi ninyi. hakuna future katika ujanja hasa kijamii mfano angalia mtu mmoja anaweza kununua vidaladala vitatu kwa kuwabana watu wanaopitia pembeni wampe rushwa lakini adha anazozileta kwenye jamii kwa kuwabana watu wakae barabarani masaa sita kila siku kwenda kazini na kurudi anasababisha wangapi kufanya kazi chini ya kiwango huku ukitazama athari za kiuchumi kijamii?

mkuu kwenye hizi barabara kiuhalisia ni kuwa wana haki za kuzuia kwa kuwa hakuna trafiki anayejua lengo la mtu kwenda huko mbele.ila cha msingi mkuu ni kujipanga na kuwaeleza nia yako na wao ni binadamu wanaelewaga sometimes. Ila linapokuja swala la rushwa ni kila mtu anachukua kwa upande wake mathalani kuna njia(service) road kutoka kimara corner/kona hadi ubungo maji ile njia pale kwa mbele iko kama imezibwa ila ukweli haijazibwa ukifika pale wanakuja vijana wanakuambia toa kitu kidogo then wao wenyewe wanatoa lile jiwe unapita na wanalirudisha na imekuwa ndo utaratibu.
 
mabadiliko yanaanza mimi na wewe.
unajua lipo tatizo nchi hii uchumi tumeugeuza ni uchumi wa ujanja ujanja. ili mtu afanikiwe lazima kufanya utapeli, kupata dili au kutumia madaraka vibaya.

na hili limekuwa ni jambo la kawaida na wale wanaoijifanya kutaka kutafuta kwa kutumia uchapa kazi mifumo ya kuwalinda inawashughulikia na kuwafilisi.

ni lazima tuanzie sehemu tubadili jamii yetu kwani huko tuendako watoto wetu watafilisika maana mataifa makubwa yanaweza kupiga hatua zaidi kwa kutumia ujanja kwetu lakini kwa nchi masikini mkilea ujanja wageni wa nje watakuja na kutumia ujanja huo kuwafilisi ninyi. hakuna future katika ujanja hasa kijamii mfano angalia mtu mmoja anaweza kununua vidaladala vitatu kwa kuwabana watu wanaopitia pembeni wampe rushwa lakini adha anazozileta kwenye jamii kwa kuwabana watu wakae barabarani masaa sita kila siku kwenda kazini na kurudi anasababisha wangapi kufanya kazi chini ya kiwango huku ukitazama athari za kiuchumi kijamii?
 
hilo ni kweli lakini msemo huu unahitaji kueleweka.

mimi na wewe mamlaka yetu yanaishia kwenye kuongea mambo haya ili viongozi wetu wachukue hatua.

wapo walioko serikalini wenye kutakiwa kushughulikia mambo haya moja kwa moja.

wapo tuliowapa majukumu ya kusimamia serikali ambao ni mhimili wa bunge au chini yake madiwani nao wanatakiwa kufuatilia.

sasa hao wasipochukua hatua ndio mpira utarudi kwetu tena.

Leo wamenibania kupita service road wanaruhusu STK
 
elimu kwa wananchi kujitambua ndio mkombozi pekee.

watumishi wa umma wote wameajiriwa na wanalipwa kwa fedha ya wananchi.

ni sawa umemuajiri mtu katika shamba lako siku unaenda shambani anakuomba rushwa ili akuruhusu uchume nyanya.

hayo yanaweza kutokea iwapo mwenye shamba hajitambui na huyu aliyewekwa shambani hajui wote hawana elimu.

kuelimisha jamii ndio njia pekee ya kuwa huru.

Leo wamenibania kupita service road wanaruhusu STK
 
Sasa nimekupata...nimejuwa nia yako kubwa..unataka sheria ifuate unayotaka wewe..sioni chamsingi unacho lialia.
 
kutokukiona kunakutambulisha wewe ni mtu gani, maelezo yangu yako wazi na argument yako iko wazi only tanzanian wanaosoma mada hii wanaweza kuchambua nani ni nani kati yetu.

Sasa nimekupata...nimejuwa nia yako kubwa..unataka sheria ifuate unayotaka wewe..sioni chamsingi unacho lialia.
 
Back
Top Bottom