John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Dereva ambaye alisababisha ajali ya Basi la Kampuni ya Kilimanjaro Express iliyotokea jana Machi 14, 2022 Mkoani Songwe na kusababisha vifo vya watu wanne, Mjahid Waziri mwenye umri wa miaka 39, amefutiwa leseni ya udereva.
Ajali hiyo ilitokea wakati basi likitoka Tunduma kuelekea Dar es Salaam ambapo lililopindukia korongoni eneo la Senjele wilayani Mbozi sababu ikiwa ni mwendokasi alipokuwa akitaka kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake likiwemo lori.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Rashid Ngonyani amesema wanamfutia leseni dereva huyo mkazi wa Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kwanza wakiwa wanamshikilia na baadaye watamfikisha Mahakamani.
Source: Clouds TV
Pia soma > Songwe: Basi la Kampuni ya Kilimanjaro Express lapata ajali, watu wanne wafariki dunia