Dereva bodaboda auawa akidaiwa kuiba mayai matatu

Dereva bodaboda auawa akidaiwa kuiba mayai matatu

Hizi issue za uswahilini pasipo uchunguzi wa kina mnaweza kupotezwa pasipostahili kupotezwa. Kiufupi profile ya kijana ijulikane na hali ya wizi kwa huo mtaa ijulikane.

Sihalalishi chochote kilichotokea lakini mara nyingine, wizi ukiwa mwingi maani pasipo kukamata yoyote, siku akijichanganya mtu hata kwa bahati mbaya lazma afanywe wa mfano
 
Dereva bodaboda anayefahamika kwa jina la Dickson Chacha(24), aliyekuwa mkazi wa Mtaa wa Machimbo kata ya Kipunguni jijini Dar es Salaam, amefariki dunia kwa kupigwa akidaiwa kuiba mayai matatu kwenye moja ya nyumba inayofuga kuku wa mayai kwenye mtaa huo.

Mama wa kijana huyo ameomba vyombo vya sheria kuingilia kati ili haki ya mtoto wake iweze kupatikana kwani waliotekeleza tukio hilo wanawaona mtaani wakitamba kuwa hawawezi kushindana na watu wenye pesa.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Machimbo, Evana Isaya amekiri tukio hilo kutokea mtaani kwake, akidai kuwa kijana huyo aliingia kwenye nyumba ya watu usiku hivyo akashambuliwa hadi kufikia umauti wake, huku akiomba wananchi kutojichukulia sheria mkononi kwa matukio hayo.
View attachment 3227774
Daah, mayai tu na unaua mtu na wapo watu wanatembea kwenye viyoyozi vya V8 na wameiba mabilioni na mabilioni
 
Hata kama ni mwizi mayai3!
  • Inawezekana angetenda maasi zaidi ya hayo, mwizi kuingia sehemu usiku anaweza kukuua.​
  • Tusiangalie alichochukua kwa sababu aliwaiwa, kama yeye (mwizi) angewawai si ajabu angeangamiza hiyo familia.​
  • Kwa kifupi wizi/ujambazi si kitu kizuri; asiyefunzwa na mamaye ufunzwa na ulimwengu.​
 
Maeneo yenye uchawi na ushirikina bei ya mayai viza ni Sawa na bei ya mayai ya kawaida.
Dunia ina mambo hii bado kuyajua.
 
Back
Top Bottom