Mngeanza kwa kupata ushauri wa kisheria.
1. Kikundi hicho kimesajiliwa?
Kama hakijasajiliwa pia siyo kosa mnaweza KUNUNUA ardhi kwa pamoja, lakini makubaliano ya umiliki yawe kimaandishi.
Kama kimesajiliwa, basi kwenye kumiliki ardhi mngekuwa mmeshaanza mchakato wa bodi ya udhamini ili mpewe ruhusa ya kumiliki ardhi na RITA.
Pia, serikali ya mtaa siyo chombo chenye mamlaka ya kiutendaji, ni chombo cha serikali ya kata katika mamlaka za miji, siyo body corporate. It's actually a toothless dog.
Serikali ya Kijiji ndiyo inayoidhinisha uuzwaji wa ardhi. Kama Hakuna serikali ya Kijiji, basi usinunue shambani hapo, nunua ardhi iliyopimwa tu.
2. Mngepata ushauri wa kitaalam.
Hekari 10 za ardhi ukizipima utapata hekari 7 mpaka 8. Kwa sababu 20% to 30% ya ardhi hiyo itakuwa ni barabara.
Kwa hiyo hesabu ya kila mtu atapata 800sqm ilikosa ujuzi wa Mambo ya ardhi na haikufikiria upimaji.
Pia, mngepata mpimaji (surveyor) afanye reconnaissance ili apate coordinates halafu aangalie kama Kuna upimaji wowote uliowahi kufanywa eneo hilo, na kama Kuna umiliki. Mngehakikisha akimaliza tu kupima anawarushia excel file la vipimo, huwa haichukui dakika mbili hapo hapo shambani ili upate second opinion. Hii ni must kwa sababu usimuamini mtu yeyote. Asipokupa excel file shambani, usimpe hela.
Kwa hiyo ununuzi wenu ndiyo uliotoa mwanya wa kutapeliwa.