DOKEZO Dereva Bodaboda tulionunua ardhi Boko Mnemela tumetapeliwa, tunaomba msaada wa Serikali Kuu

DOKEZO Dereva Bodaboda tulionunua ardhi Boko Mnemela tumetapeliwa, tunaomba msaada wa Serikali Kuu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Matajari wanaungana kumkabili masikini, ila masikini wanashindwa kuungana kumkabili tajiri.

Ili kushinda hii case endeleeni kuwa wamoja, nyie Bodaboda mlivyo na vurugu hivyo mnashindwa kwenda kupack boda zenu kwenye maofisi yao? Uzuri mpo 50
 
Poleni sana.

Binafsi nimenunua eneo kiwanja huko Boko Mnemela, Kijiji cha Mpiji Station.

Mimi nimenunua kutoka moja ya kampuni zile zinazopina na kuuza viwanja, ambapo ninadhani kuna usalama zaidi maana wao wana mikataba ambapo moja ya kipengele kinaeleza kwamba iwapo kiwanja kitabainika kuwa na mgogoro basi kampuni itawajibika kukupa eneo lingine, ila usiporidhika watakurudishia fedha ulizolipa.

Kwa upande wenu, mmejitahidi kufanya utafiti lakini, kuna mahali mlikosea kidogo tu ila pana madhara makubwa.

Mlitakiwa kwanza, kumdodosa Muuzaji kwamba alipataje lile eneo? Jibu mara nyingi lingekuja kwamba kapewa, basi mngehoji kapewa na nani? Kama kanunua, mkataba upo wapi?

Akishamaliza kujibu, basi mnaenda kwa majirani kupeleleza.

By the way shamba la Mo huko Boko Mnemela ni maarufu sana, kwa hiyo msingekosa taarifa.

Kuna shamba kama la Maboto, Mwarabu na pia Serikali ina shamba eka 4000 huko Kibaha.

Ila Mkuu wa Mkoa wa Pwani juzi kaagiza kwamba Watendaji wote waliohusika kitapeli watu huko kwenye ardhi washughulikiwe.
 
Sasa Mwenyekiti wa serekali ya mtaa anakuwaje wa mchongo!? Inamaana serekali kuu haijui hilo!!??
Ngoja nikupe mwanga. Anakwenda MTU pale maeneo ya serikali za mitaa anamuhuri wa michongo, wakati muuzaji anskupeleka pale ofisini yule mtumishi feki anajitokeza , wanasalimiana fresh halafu wanakuambia wanaokoa muda, muhuri anao mfukoni haina haja ya kuingia ofisini, anatokea mzee mwingine wa michongo Kama shahidi, hao wote watatu sio watu wa Kibaha Ni watu wa Dar, unakwenda kuonyeshwa shamba la MTU mwingine, kule shambani unakuta Kuna mtu na mkewe wa michongo wanakuhakikishia kwamba wanapakana na muuzaji na Ni ndugu Yao. Kumbuka wote hao Ni watu wa Dar, wamekwenda ili ujiridhishe. Unauziwa eka kwa milioni , mkataba feki na mihuri mingi unapewa, kibaya zaidi unaambiwa ulipe 10 percent ya Bei kwenye ofisi ya serikali ya mtaa lkn kwa kua wote wako pale shambani wanakuambia mmalize kila kitu kule kule shambani. Unatoa pesa na kila mtu anayeyuka.
Kesho yake ukirudi majirani huwakuti, ukienda serikali za mitaa unaonyeshwa watumishi halali ambao hiyo transaction hawaijui.
Ogopa matapeli.
 
Basi mmepigwa na middle men wenu mlie mpaa kazi ya kutafuta Aridhi, yeye ndiyo chanzo cha nyininyi kupigwa na mchongo wote alikua anaujua,sema nyinyi mnamuamini sana! Katumia trust kuwapiga!!
 
Mmekosea,nyie endeleeni na mchakato wenu.jengeni kabisa uzuri ofisi ya ardhi mlifika,pia Serikali za mitaa na 10%mlitoa.
So,nyie endeleeni eneo lenu.
Huyo sijui mmiliki ambaye hata idara ya ardhi haijui ndo yeye aende Mahakamani.
Hapo mlipofikia hamtaambulia hata sent.
Mlijuaje Kama ni eneo la Mo.
 
Kufika ofisi ya ardhi hakutasaidia kama hamkufanya search. Search inalipiwa na control number na unapata report yenye muhuri wa registrar of titles kuonyesha kuwa eneo halina hatimiliki.

Halafu Hakuna kitu kinaitwa 10% ya serikali ya mtaa. Hiyo ni dalili mojawapo ya utapeli.
 
Back
Top Bottom