Dereva makini, fanya yafuatayo

Dereva makini, fanya yafuatayo

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Dereva makini unatakiwa kabla ya kuliondosha au kuwasha gari lako ufanye mambo haya:-

Ufanye ukaguzi wa nje ya gari
  • Matairi kama yote ni mazima, hakuna sehemu iliyotuna​
  • Taa zote kama zinawaka(taa kubwa, indicator, reverse, hazard, break)​
Ukaguzi wa boneti
  • Maji ya radiator​
  • Maji ya wiper​
  • Oil (injini, breki, clutch, usukani)​
  • Betri​
Ukaguzi wa ndani ya gari
  • Dashboard, kama kuna ujumbe wowote ufanyie kazi, iwe mafuta, joto n.k​
  • Clutch kama inafanya kazi​
  • Breki kama inafanya kazi​
  • Gear kama inafanya kazi​
  • Accelerator kama inafanya kazi​
  • Usukani kama unafanya kazi vizuri​

Baada ya kukamilisha hayo yote na ukaona viko sawa, unaweza kuondosha gari.​
 
Hahaa! Hii daily routine (tena sio daily, ni kila unapotaka kuiondosha) kama ulinunua gari mkononi au dalali lazima zikuhusu tu 😆
Ata kama ni mpya lazima ufanye hivyo, kwa sehemu unayopaki inaweza kuwa na changamoto; nyoka anaweza kuingia kwenye radiator kwa ajili ya kutafuta joto n.k kwa hiyo ukaguzi ni muhimu.
 
unanunua galon la Lita 5 kwa elfu kumi unatumia mpaka unachoka. shida watu mpaka leo wanaweka maji ya mfereji, au maji ya chupa , makosa
Huwa natumia coolant kwenye ford, nikipiga safari ndefu huwa inapungua; ila ni muhimu kukagua kabla tatizo halijatokea; maji/ coolant ikiisha injini inapata moto na kuunguza mifumo ya umeme na hatimaye gari itazima.

Ukaguzi hauepukiki.​
 
Back
Top Bottom