Dereva Mtanzania akutwa na maambukizi ya COVID 19 kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda

Dereva Mtanzania akutwa na maambukizi ya COVID 19 kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda

G Sam,
Huyu dereva kila mizani alitoa kadi ya gari wakati wa kupima, huyu dereva kila alipokutana na trafik aliombwa leseni na kadi ya gari, huyu dereva kila check point alitoa document za mzigo, njiani alikula chakula alilala gesti, the chain iz horrible
 
Interior cabinet secretary Kenya, Fred Matiangi hapo jana ametangaza hatua za ziada zitatekelezwa mipakani Kenya hasa Namanga kuzuia kuenea virusi vya corona kupitia mipakani. Uzembe wetu kukabiliana na corana tunatengwa.
 
Dreva wa gari la mzigo aliekua akitokea Dar kwenda Kampala amekutwa na virusi vya corona baada ya kupimwa mpaka wa mtukula kati ya Tanzania na Uganda.

Dreva huyo ambae aliendelea na safari yake baada ya vipimo, alitafutwa na kurudishwa Tanzania baada ya majibu yake kuonyesha ana virusi vya corona, imesema wizara ya afya ya Uganda.

COVID-19: Tanzanian Truck Driver Tests Positive in Uganda

Tuendelee kuliombea Taifa huku tukichukua tahadhari ndugu zangu, hali ni mbaya, we fikiria kaambukiza wangapi toka bandarini, njiani alikopita mpaka kufika mpakani.

Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania
 
Duuh so vipimo vyetu na Uganda ni tofauti?Vyetu viliona yuko poaa,hahaha
 
Kwani Uganda wakimhesabia huyo mgonjwa kwao wanapungukiwa nini?.Mbona Tanzania wanataja idadi kwa ujumla huku wakibainisha uraia wao!

Na sisi tukianza kuwarudisha wagonjwa wa mataifa mengine badala ya kuwashikilia na kuwatibu tutakuwa tunapunguza au tunaongeza tatizo?

Sijawaelewa kabisa.
Unawalamu bure tu wakati ni makosa yetu badala ya kufunga mipaka tunajali uchumi wa nchi kwanza badala ya kuchukua hatua za kisayansi tunahimiza watu wa sali sana....bora arudishwe tu tumuombee ndo sera ya Raisi wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sifungi mipaka kuna nchi zinanitegemea nyooooo...hizo nchi zenyewe saiv zinakunanga na wagonjwa wako wanakurudishia upambane nao!

Hapa wanachojaribu kukuonesha ww ndie supplier mkubwa wa corona EA sbabu ya maamuzi yako mabovu mabovu na utai cost dunia!
 
Sifungi mipaka kuna nchi zinanitegemea nyooooo...hizo nchi zenyewe saiv zinakunanga na wagonjwa wako wanakurudishia upambane nao!Hapa wanachojaribu kukuonesha ww ndie supplier mkubwa wa corona EA sbabu ya maamuzi yako mabovu mabovu na utai cost dunia!
Very Shameful.
 
[emoji16][emoji16].ukitaka uwachanganye uanze kukimbia.
Wakati wanakujua una corona.
Kwahio Data za Tanzania zina Plus One? Na wanamrudisha ili iweje si wamtibu ili apone alafu ndio arudi? Au tunaanza kuwa-treat binadamu kama commodities.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
....
Dreva huyo ambae aliendelea na safari yake baada ya vipimo, alitafutwa na kurudishwa Tanzania baada ya majibu yake kuonyesha ana virusi vya corona, imesema wizara ya afya ya Uganda....

Mbona hiyo habari inaonyesha Dereva bado anatafutwa ili harudishwe Tanzania
 
Back
Top Bottom