Mawaziri wa Afya wa East Africa na SADC wakubaliane kuwa kila dereva wa gari, meli au ndege ya mizigo, kabla hajaondoka nchini kwake awe amepimwa. Ripoti ya vipimo itumwe kwenye nchi anakoenda. Taarifa iwe mpakani. Pale mpakani apimwe tena ili kujithibitishia kuwa hajapata maambukizi akiwa njiani.
Wizara za afya za mataifa haya, ziwe na hoteli maalum ambako madereva hawa wanaweza kula na kulala. Na hoteli hizo ziwe ni zile tu ambazo wahudumu wake wote wamepimwa, na zipo kwenye karantini, kwa maana ya kuwa wafanyakazi wake wote wanaishi hapo hapo hotelini na wanaofanyiwa vipimo vya mara kwa mara, na hakuna watu wengine wanaohudumiwa kwenye hoteli hizo. Zinahitajika kuwa hoteli ndogo ambazo wateja hawa wa vyombo vya usafirishaji mizigo, watatosha kuzifanya zijiendeshe.
Siyo jambo jema, wagonjwa wa nchi moja wakawa wanapeleka ugonjwa nchi nyingine. Kila nchi ibakie na wagonjwa na maambukizi yake.