DOKEZO Dereva Mtanzania anashikiliwa Sudan Kusini baada ya kugonga mtu, inadaiwa Polisi wagoma kumuachia wanataka hela

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
WhatsApp Image 2025-02-21 at 06.22.21_45162f04.jpg
Kuna Mtanzania mwenzetu anaitwa Juma Ally Maganga ambaye ni dereva wa magari makubwa, inadaiwa anashikiliwa na Watu ambao wanadai wao ni Askari Polisi Nchini Sudan Kusini, sababu ya kumshika ni kwamba wanamtuhumua amemgonga mtu na kusababisha kifo wakati alipokuwa katika safari zake akipita nchini humo.

Vyanzo vya taarifa zinaeleza kuwa bosi wa Mtanzania huyo anaitwa Gabriel John Kiliki ni bosi wa Kampuni inaitwa Kiliki Company.

Juma akiwa anaendesha gari lenye namba za usajili T 931 CWS alisafiri kwenda Sudan Kusini eneo la Juba ambapo ndipo ajali ilitokea, akapalekwa Kituo cha Polisi cha Nimule.

Baadaye akahamishwa na kupelekwa Kituo cha Polisi Malikia Police Station.

Siku ya tukio la ajali ilikuwa Februari 14, 2025, baada ya kushikiliwa, akapewa nafasi ya kutoa taarifa kwa ndugu zake ambapo inadaiwa Polisi waliomshikilia walianza kutoa maelekezo kuwa watumiwe fedha.

Taarifa zaidi zitafuata kujua kinachoendelea…

==========================

JamiiForums imefanya jitihada za kuwasiliana na mmiliki wa gari alilokuwa akiendesha Juma Ally Maganga, mke wa dereva huyo na pamoja na upande wa Wizara ya Mambo ya Nje

Mmiliki wa gari, Gabriel John Kiliki
Ni kweli dereva wangu Juma Ally Maganga ameshikiliwa tangu Februari 14, 2025, tumeshatuma hela zaidi ya Tsh. Milioni 1 kwa Askari waliomshikilia ili wamuachie lakini mpaka sasa bado kashikiliwa.

Kila tunapowasiliana na hao Askari Polisi wa huko wanakuwa wanataka hela lakini hawakamilishi tunachokubaliana, baadaye wakataka tuwatumie Dola 3,500 ambazo lakini hatujatuma mpaka sasa.

Pia, tunaendelea kuwasiliana na Mwenyekiti wa Madereva wa Malori wa Afrika Mashariki anaitwa Sudi, anasaidia kuwasiliana na Polisi wa hapo.

Wakati huohuo, kuna madereva wangu wengine wa nne ambao nao wapo huko wanashughulikia, gari pia alilopata nalo hiyo ajali wamelizuia mpaka sasa na nimejulishwa dereva wangu huyo hali yake kiafya siyo nzuri kwa kuwa anaumwa, alipigwa sana na Wananchi baada ya tukio kutokea.

Mke wa dereva, Rehema Godfrey Mongi
Wakati mume wangu anasafiri alikuwa na msaidizi wake ambaye ni mtoto wangu pia, anaitwa Hassan Juma Maganga, baada ya tukio waliwapiga sana, walipofika Polisi wakawapeleka kwenye kituo cha Afya baadaye wakawapeleka gerezani.

Walimuachia mwanangu ili apate nafasi ya kutoa taarifa kwetu, wamekuwa wakitaka hela huko, tunatuma lakini hawamtoi.

Hela inapotumwa mwanangu akienda Kituo cha Polisi waliposhikiliwa awali, wanaambiwa Askari aliyepokea fedha hayupo, mara hayupo zamu mara kaenda likizo.

Lakini pia kuna utata juu ya tukio hilo kwa kuwa wao wanasema ajali ilimhusisha Mwanaume lakini kwenye taarifa ya Polisi inadaiwa wameandika aliyekufa ni Mwanamke.

Tunaomba msaada Serikali itusaidie kumuokoa Mtanzania mwenzetu, nimeambiwa ana kidonda kikubwa, anaumwa sana lakini bado wamemuweka ndani.

WIZARA YA MAMBO YA NJE
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga anasema "Nimewasilisha taarifa hii Idara ya Afrika leo asubuhi (Februari 20, 2025) tulipoipokea. Wanafuatilia kwenye ofisi zetu za Ubalozi. Naomba nikupe majibu pindi nitakapoyapata. Nashukuru kwa ushirikiano wako."
WhatsApp Image 2025-02-20 at 19.11.18_e665533a.jpg

================
WhatsApp Image 2025-02-21 at 06.22.23_c5d4c12e.jpg
WIZARA: KUNA MAENDELEO KATIKA UFUATILIAJI
Wizara ya Mambo ya Nje imesema inaendelea kufuatili suala la Mtanzania Juma Ally Maganga (45) kushikiliwa Nchini Sudan Kusini kwa tuhumza za kugonga mtu na kusababisha kifo chake.

Inadaiwa tukio hilo lilitokea Februari 14, 2025 alipokuwa akiendesha Gari (T931 CYS) mali ya Kiliki Company, akiwa na msaidizi wake ambaye pia ni mwanaye, baada ya hapo walishambuliwa na raia, Askari Polisi walipofika wakawaokoa na kuwapeleka kutibiwa na baadaye Kituo cha Polisi Malikia.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje, Mindi Kasiga, amesema “Mkurugenzi Idara ya Afrika anafuatilia kwa karibu na Ubalozi wetu Kampala. Inavyoonekana kuna mwendelezo mzuri, wamefanikiwa kuwasiliana na utingo. Kwakuwa hatuna Ubalozi Sudan Kusini mawasiliano yamekuwa shida kidogo. Lakini Nimeomba wakipata chochote watuambie.”

Pia soma ~ Mtanzania anayeshikiliwa Sudani Kusini aendelea kusota, familia ya aliyegonjwa yataka fidia
 
Inauma s
Kuna Mtanzania mwenzetu anaitwa Juma Ally Maganga ambaye ni dereva wa magari makubwa, inadaiwa anashikiliwa na Watu ambao wanadai wao ni Askari Polisi Nchini Sudan Kusini, sababu ya kumshika ni kwamba wanamtuhumua amemgonga mtu na kusababisha kifo wakati alipokuwa katika safari zake akipita nchini humo.

Vyanzo vya taarifa zinaeleza kuwa bosi wa Mtanzania huyo anaitwa Gabriel John Kiliki ni bosi wa Kampuni inaitwa Kiliki Company.

Juma akiwa anaendesha gari lenye namba za usajili T 931 CWS alisafiri kwenda Sudan Kusini eneo la Juba ambapo ndipo ajali ilitokea, akapalekwa Kituo cha Polisi cha Nimule.

Baadaye akahamishwa na kupelekwa Kituo cha Polisi Malikia Police Station.

Siku ya tukio la ajali ilikuwa Februari 14, 2025, baada ya kushikiliwa, akapewa nafasi ya kutoa taarifa kwa ndugu zake ambapo inadaiwa Polisi waliomshikilia walianza kutoa maelekezo kuwa watumiwe fedha.

Taarifa zaidi zitafuata kujua kinachoendelea…

==========================

JamiiForums imefanya jitihada za kuwasiliana na mmiliki wa gari alilokuwa akiendesha Juma Ally Maganga, mke wa dereva huyo na pamoja na upande wa Wizara ya Mambo ya Nje

Mmiliki wa gari, Gabriel John Kiliki
Ni kweli dereva wangu Juma Ally Maganga ameshikiliwa tangu Februari 14, 2025, tumeshatuma hela zaidi ya Tsh. Milioni 1 kwa Askari waliomshikilia ili wamuachie lakini mpaka sasa bado kashikiliwa.

Kila tunapowasiliana na hao Askari Polisi wa huko wanakuwa wanataka hela lakini hawakamilishi tunachokubaliana, baadaye wakataka tuwatumie Dola 3,500 ambazo lakini hatujatuma mpaka sasa.

Pia, tunaendelea kuwasiliana na Mwenyekiti wa Madereva wa Malori wa Afrika Mashariki anaitwa Sudi, anasaidia kuwasiliana na Polisi wa hapo.

Wakati huohuo, kuna madereva wangu wengine wa nne ambao nao wapo huko wanashughulikia, gari pia alilopata nalo hiyo ajali wamelizuia mpaka sasa na nimejulishwa dereva wangu huyo hali yake kiafya siyo nzuri kwa kuwa anaumwa, alipigwa sana na Wananchi baada ya tukio kutokea.

Mke wa dereva, Rehema Godfrey Mongi
Wakati mume wangu anasafiri alikuwa na msaidizi wake ambaye ni mtoto wangu pia, anaitwa Hassan Juma Maganga, baada ya tukio waliwapiga sana, walipofika Polisi wakawapeleka kwenye kituo cha Afya baadaye wakawapeleka gerezani.

Walimuachia mwanangu ili apate nafasi ya kutoa taarifa kwetu, wamekuwa wakitaka hela huko, tunatuma lakini hawamtoi.

Hela inapotumwa mwanangu akienda Kituo cha Polisi waliposhikiliwa awali, wanaambiwa Askari aliyepokea fedha hayupo, mara hayupo zamu mara kaenda likizo.

Lakini pia kuna utata juu ya tukio hilo kwa kuwa wao wanasema ajali ilimhusisha Mwanaume lakini kwenye taarifa ya Polisi inadaiwa wameandika aliyekufa ni Mwanamke.

Tunaomba msaada Serikali itusaidie kumuokoa Mtanzania mwenzetu, nimeambiwa ana kidonda kikubwa, anaumwa sana lakini bado wamemuweka ndani.

WIZARA YA MAMBO YA NJE
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga anasema "Nimewasilisha taarifa hii Idara ya Afrika leo asubuhi (Februari 20, 2025) tulipoipokea. Wanafuatilia kwenye ofisi zetu za Ubalozi. Naomba nikupe majibu pindi nitakapoyapata. Nashukuru kwa ushirikiano wako."
Inauma sana..
Boss yeye atakomboa gari lake haangaiki na wewe dereva.
Hii hata rwanda jamaa yangu aligonga akakamagwa eti anaambiwa "usingeuja kwetu huyuasinge kufa"basi raia walitaka kumuua sema polisi yao iliwahi ilikua chupu chupu wamalize
 
Back
Top Bottom