Dereva Mtanzania Juma Ally Maganga aliyeshikiliwa Sudan amehukumiwa miaka mitatu jela

Dereva Mtanzania aliyekuwa akiendesha lori, Juma Ally Maganga (45) ambaye alikuwa akishikiliwa na Mamlaka za kiusalama nchini Sudan Kusini kwa tuhuma za kugonga mtu na kusababisha kifo cha mtu huyo, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani.

Taarifa kutoka kwa mmiliki wa Lori alilokuwa akiendesha Gabriel John Kiliki ameonesha nyaraka inayoonesha hukumu ya Maganga imeanza 14/02/2025 pamoja na kwamba anatakiwa kulipa faini mbalimbali.

Awali, familia ya dereva huyo iliyopo Tanzania ilieleza kuwa walijulishwa kutoka Sudan kuwa aliyegongwa alikuwa akiendesha pikipiki na kupoteza maisha papohapo ambapo Familia ya marehemu na kwamba imesema ili Mtanzania huyo aachiwe pamoja na gari inatakiwa ilipwe faini ya Tsh. Milioni 72.

Mke wa dereva huyo, Rehema Godfrey Mongi (38) alinukuliwa akisema awali Familia ya marehemu ilitaka faini ya zaidi ya Tsh. milioni 100 lakini baada ya kuombwa na Mwanasheria wamekubali kupunguza, na kwamba kama itapatikana Tsh. milioni 36 wapo tayari kumuachia Maganga bila gari “Mmiliki wa gari yeye amesema hana hela kwa sasa yupo tayari kusamehe gari.”
​

Ilivyokuwa awali:
~
Dereva Mtanzania anashikiliwa Sudan Kusini baada ya kugonga mtu, inadaiwa Polisi wagoma kumuachia wanataka hela

~ Dereva Mtanzania anayeshikiliwa Sudani Kusini kwa kugonga mtu aendelea kusota gerezani, familia ya aliyegonjwa yataka fidia
Mbona ni uhuni tu hapo kwani huko sudani watu wakigonga ndiyo wote wana hukumiana hivyo au kuna janja ya ufisafi usikute ni mchezo baina ya mmiliki wa gari na dereva na ndugu kupata pesa ...hakuna sheria kama hiyo popote duniani ...sasa hiyo sudani ambayo watu wanauana kama kuku ndiyo dhamani ya mtu iwe hivyo hata ulaya hakuna sheria ya hivyo hapo kuna mchezo
 
niliiona hii habari kwa Millard Ayo instagram. Nilichanga elfu 30 kwa mke wa jamaa. iliwekwa namba yake.
 
Upumbavu mtupu sudani magari ya kenya yanagonga na kuua kila siku na hakuna hukumu ya hivyo .
 
Akikaa miaka 3 ndo anatoka ye na gari akaze tu miaka 3 sio mingi ela ipewe familia yake
 
Mke wa dereva huyo, Rehema Godfrey Mongi (38) alinukuliwa akisema awali Familia ya marehemu ilitaka faini ya zaidi ya Tsh. milioni 100 lakini baada ya kuombwa na Mwanasheria wamekubali kupunguza, na kwamba kama itapatikana Tsh. milioni 36 wapo tayari kumuachia Maganga bila gari “Mmiliki wa gari yeye amesema hana hela kwa sasa yupo tayari kusamehe gari.”
Mmhhh. Pazitoo 😪
 
Angekua mzanzibari angesaidiwa ila kwakua n mtanganyika na sio chawa w CHURA.pole yake na familia na watanganyika kwa ujumla.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Basi buana kama serikali haina ubalozi inaruhusu vp watu wake waende Sudan Kusini ?
Mjinga wewe huna exposure ya maisha

Kutafuta fursa ni popote duniani

Sio kazi ya serikali kumpangia mtu akatafute riziki wapi

Utakufa maskini shauri yako
 
Huku kwetu madereva ya kirwanda wanauwa raia wetu sana barabarani niliwah kushuhudia gari la mizigo lime over take sehemu isiyo ruhusiwa likasababisha basi kupinduka na kuuwa watu umo,sina hakika kama lile gari kesi ilifikia kama ya uko sudan,wamegonga watoto sana wa shule barabara ya dom morogoro,ila raia wetu uko wanakwenda kula miaka,,hii inchi hiii ni upuuzi sana.
Ajali ina mambo mengi,lakini nanyi madereva tujitaidi kuongeza umakini,uhai ni mzuri sana.
Sijui ile kesi ya dereva ya kirwanda alichoma kisu mtanzania mwenzetu ilifika wapi??
Ziko sheria za barabarani kila nchi ukikosea kuna adhabu zake za kisheria
 
Sasa hizo mahakama gani mpaka raia wanaingilia kuamua wanachotaka?. Mahakama haina sheria yake iliyonyooka kwa ajili ya kosa la kama hilo la kugonga mtu?. Iweje ndugu ndio wanapanga adhabu?
 
Angekua mzanzibari angesaidiwa ila kwakua n mtanganyika na sio chawa w CHURA.pole yake na familia na watanganyika kwa ujumla.
KAZI ni kipimo cha utu
Kila nchi ina sheria zake ukikosea huko utahukumiwa huko huko kwa sheria zao

Kazi ya serikali sio kutetea wahalifu wiofanya uhalifu nje ya nchi

Kokote nchi yeyote unatakiwa kutii sheria bila shuruti
 
Dereva Mtanzania aliyekuwa akiendesha lori, Juma Ally Maganga (45) ambaye alikuwa akishikiliwa na Mamlaka za kiusalama nchini Sudan Kusini kwa tuhuma za kugonga mtu na kusababisha kifo cha mtu huyo, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani.

Taarifa kutoka kwa mmiliki wa Lori alilokuwa akiendesha Gabriel John Kiliki ameonesha nyaraka inayoonesha hukumu ya Maganga imeanza 14/02/2025 pamoja na kwamba anatakiwa kulipa faini mbalimbali.

Awali, familia ya dereva huyo iliyopo Tanzania ilieleza kuwa walijulishwa kutoka Sudan kuwa aliyegongwa alikuwa akiendesha pikipiki na kupoteza maisha papohapo ambapo Familia ya marehemu na kwamba imesema ili Mtanzania huyo aachiwe pamoja na gari inatakiwa ilipwe faini ya Tsh. Milioni 72.

Mke wa dereva huyo, Rehema Godfrey Mongi (38) alinukuliwa akisema awali Familia ya marehemu ilitaka faini ya zaidi ya Tsh. milioni 100 lakini baada ya kuombwa na Mwanasheria wamekubali kupunguza, na kwamba kama itapatikana Tsh. milioni 36 wapo tayari kumuachia Maganga bila gari “Mmiliki wa gari yeye amesema hana hela kwa sasa yupo tayari kusamehe gari.”
​

Ilivyokuwa awali:
~
Dereva Mtanzania anashikiliwa Sudan Kusini baada ya kugonga mtu, inadaiwa Polisi wagoma kumuachia wanataka hela

~ Dereva Mtanzania anayeshikiliwa Sudani Kusini kwa kugonga mtu aendelea kusota gerezani, familia ya aliyegonjwa yataka fidia
Hilo suala lipelekwe wizara ya mambo ya nje kuna utaratibu fulani huwa wanafanya ili mtu aachiwe
 
Serekali ya Tz hainaga msaada kwa raia wake
sio kama Kenya. Kenya pamoja na ukabila wana umoja sana.
Tz tunaonekana ni wamoja kumbe hatujaliani
Umoja wa tz ni wa kinafki. Ni facade imetengenezwa kufunika kpasuko uliopo ili wageni wasijue
 
Back
Top Bottom