Gari limeshikiliwa na hao Wasudani mkuu.Akitoka auze hilo gari apate mtaji wa kuanzia maisha
Huku za Sudani ni Bora zaidi kuliko za Bongo.Awali, familia ya dereva huyo iliyopo Tanzania ilieleza kuwa walijulishwa kutoka Sudan kuwa aliyegongwa alikuwa akiendesha pikipiki na kupoteza maisha papohapo ambapo Familia ya marehemu na kwamba imesema ili Mtanzania huyo aachiwe pamoja na gari inatakiwa ilipwe faini ya Tsh. Milioni 72.
Mmezoea kugonga gonga watu bongo hamjali maisha ya wengineTraffic case ngumu kiasi hicho!
Huko hakufai kupeleka gari yako.
😂🤣🤣 Hakikisha ukipata bahati ya kuendesha gari kubwa hapa TZ na ukakutana na gari ina STL , SU ......... Zichakate haswaaaaHuku za Sudani ni Bora zaidi kuliko za Bongo.
Huku ukigonga na kuua unatamba mtaani tu ila ukisema No reform unanyea debe
Alafu usilo lijua ni kwamba hata leo hii Mganda , Mrundi , Mkongo ......n.k wakiingia bongo kama ni dereva wa roli huwa makini sana kwani nao husema serikali ya Tanzania huwabana sana hususani pale wanapo sababisha ajari .Bongo madereva wanadekezwa sana, ndio maana mnaona sawa tu kugonga mtu na kuua ..eti traffc case. Hata kama ni traffic case kinachoangaliwa ni mazingira ya ajali.Huwezi kusababisha ajali na kifo kwa ulevi halafu uepuke jela.Au uendeshe bila kufuata sheria za barabarani usababishe maafa halafu useme ni traffic case.Watu wanaovertake hovyo hovyo kama wendawazimu sehemu isiyofaa ku overtake. Nchi nyingine kosa la kuendesha ukiwa umelewa (driving under the influence - DUI) ukikamatwa unaweza kwenda jela hata kama hujasababisha ajali, kiasi cha pombe mwilini kinaweza kuamua uende jela au la. Hivyo madereva wa kibongo laima wajue si nchi zote wanacheka na madereva wazembe.
Mahakama imetoa kifungo cha miaka mi 3 ila ndugu mwanzo mwanzo walitaka 100m baada ya kukutana na mwanasheria wa dereva wamepunguza mpaka 30m mahakama ya wapi unafanya kazi namna hiyo?Kila nchi ina sheria zake ukikosea huko utahukumiwa huko huko kwa sheria zao
Kazi ya serikali sio kutetea wahalifu wiofanya uhalifu nje ya nchi
Kokote nchi yeyote unatakiwa kutii sheria bila shuruti
Isije ikawa dereva kashikiliwa na wale jamaa wa " Tuma Kwa namba hii?"Swali ni kwanini ndugu wa.marehemu ndio.wenye maamuzi? ina maana south sudani hakuna mahakama? nadhani kuna kitu hakijakaa sawa katika hii issue.
Gari yoyote iwe ya mizigo au private cars kabla ya kuingia nchi nyingine nisemee hizi ambazo ni majirani zetu huwa lazima uikatie bima hapo boda kabla ya kyingia nchi husika na nadhani mojawapo ya kazi ya hiyo bima ni pamoja na ajali kama hizoNilidhani gari ikiingia nchi nyingine hulipiwa bima kubwa ya nchi ile - hivyo bima hiyo ndio ingehusika kuwalipa ndugu wa aliyegongwa!
Roving Journalist unaweza kufuatilia tena hii ishu kujua imefikia wapi?Dereva Mtanzania aliyekuwa akiendesha lori, Juma Ally Maganga (45) ambaye alikuwa akishikiliwa na Mamlaka za kiusalama nchini Sudan Kusini kwa tuhuma za kugonga mtu na kusababisha kifo cha mtu huyo, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani.
Taarifa kutoka kwa mmiliki wa Lori alilokuwa akiendesha Gabriel John Kiliki ameonesha nyaraka inayoonesha hukumu ya Maganga imeanza 14/02/2025 pamoja na kwamba anatakiwa kulipa faini mbalimbali ambapo kama hatafanikiwa kuzilipa ndani ya siku 14 kuna uwezekano wa adhabu ya kifungo kuongezwa.
Awali, familia ya dereva huyo iliyopo Tanzania ilieleza kuwa walijulishwa kutoka Sudan kuwa aliyegongwa alikuwa akiendesha pikipiki na kupoteza maisha papohapo ambapo Familia ya marehemu na kwamba imesema ili Mtanzania huyo aachiwe pamoja na gari inatakiwa ilipwe faini ya Tsh. Milioni 72.
Mke wa dereva huyo, Rehema Godfrey Mongi (38) alinukuliwa akisema awali Familia ya marehemu ilitaka faini ya zaidi ya Tsh. Milioni 100 lakini baada ya kuombwa na Mwanasheria wamekubali kupunguza, na kwamba kama itapatikana Tsh. milioni 36 wapo tayari kumuachia Maganga bila gari “Mmiliki wa gari yeye amesema hana hela kwa sasa yupo tayari kusamehe gari.”
Ilivyokuwa awali:
~ Dereva Mtanzania anashikiliwa Sudan Kusini baada ya kugonga mtu, inadaiwa Polisi wagoma kumuachia wanataka hela
~ Dereva Mtanzania anayeshikiliwa Sudani Kusini kwa kugonga mtu aendelea kusota gerezani, familia ya aliyegonjwa yataka fidia
Proud Muslim?Nimewahi kuishi Sudan Kusini, niwaambie tu, huyu dereva ana bahati sana hajauawa, wale watu ni makatili, lipeni hizo hela aondoke salama.
Na inaonekana ni kweli, kwa sababu nimesikiliza story hii youtube, mke alihojiwa na Millard, anasema walijadiliana na ile familia ya huyo marehemu kwa simu, walifikia hatua wakasema wao wanatamani kama vipi hata huyo dereva apigwe tu risasi, afe wamalizane nae kihivyo wote wawe wamekosa.Nimewahi kuishi Sudan Kusini, niwaambie tu, huyu dereva ana bahati sana hajauawa, wale watu ni makatili, lipeni hizo hela aondoke salama.
NCHI HII IMEJAWA NA MATAPELI NA WATU WANAOTAKA MADARAKA KWA FAIDA YAO NA FAMILIA ZAOHivi ni kweli kabisa hao viongozi wa wizara ya mambo ya nje walishindwa kufatilia tokea hiyo February mpaka mtu anahukumiwa April 23?
Kuna haja gani sasa kuwa na watu wazembe namna hiyo hapo wizarani?
Huo ubalozi wa hapo Kampala nao umeshindwa kuwa na muwakilishi kwenye jambo hilo?
Hivi hii nchi si ndio ipo kwenye jumuiya ya Africa mashariki?
Vipi hii jumuia haina kupeana taarifa za kina juu ya matatizo kama haya kwa kila raia anayeenda huko au anayekuja huku?
Na vipi kwenye mipaka yetu watu wanavyotoka huwa hawaelekezwi namna ya kuwasiliana na balozi iwapo anapata tatizo huko aendako?.
Nina jamaa ni wakenya huwa wananieleza wao wakivuka tuu mpaka tayari line zao zinawapa ujumbe wa kuwasiliana na balozi kwa nchi husika anapoelekea kwa nini na sisi hawa services provide wasipewe huu utaratibu angalau maderva na wananchi wanaoenda nchi nbali mbali wakawa wanapta taarifa kama hizi.
Mwisho ni bora watanzania tukamchangia huyu ndugu maana wahusika kamili mpaka sasa naona hawajaamua kwa dhati kumsaidia huyu dereva, cha msingi mwanafamilia ajitokeze na aende eneo husika watu tujitolee chochote kitu, hii ndio suluhisho hakuna kingine kwa sasa
Hivi vikampuni uchwara mabosi wengi ni roho mbaya ya huyo tajiri yaani kweli unatoa milioni 1 unaona ni msaada kwa dereva wako na mali yako?
Hiyo dola 3500 angetoa hali hii isingefikia hapo ilipo una truck zaidi ya moja halafu unaona hizo dola ni nyingi kuliko thamani ya gari lako kweli???