Baba_Enock
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 7,076
- 2,457
Je X-mass ni sherehe za kuzaliwa yesu kristo ? Nielewavyo gregorian calenda ilianza pale yesu alipozaliwa yaani tareh 01-januari - 01. Sasa ninapoambiwa tunasherehekea kuzaliwa yesu tar 25 -Dec, inachanganya kidogo.[au tarehe kamili ya kuzaliwa yesu haifahamiki ?] Wapendwa naomba msaada hapo na bwana asifiwe.
WANAJF;
Kwanza naomba nideclare kwamba mimi ni Mkristo tena anayejitahidi kwa nafasi yangu kuelewa vema kile ninachoamini. Nikiwa kama Mkristo, msingi wangu wa IMANI umejengwa katika MAANDIKO MATAKATIFU, yaani BIBLIA TAKATIFU. Hivyo, vyote ninavyofanya na maisha ninayoishi yanapaswa yaakisi kile nilichoelekezwa kwenye Biblia. Sasa ndugu zangu, hii Sikukuu ya Kristmas nimekuwa nikisherehekea toka nikiwa mdogo mpaka ukubwani lakni jambo moja ambalo liko wazi ni kwamba HAKUNA UKWELI WOWOTE KATIKA BIBLIA TAKATIFU KWAMBA YESU ALIZALIWA DESEMBA 25. Na kwasababu hii kitu inakosa support ya maandiko matakatifu, hivyo naamini wengi wetu tunaisheherekea tu kwasababu ya MKUMBO na MAZOEA TU. Kama kuna mtu yeyote, Mwanafunzi wa Biblia anayeweza kunisaidia na fungu lolote kwenye Biblia (toka Kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo) basi naomba anisaidie.
Zaidi ya kukosa suport ya Maandiko Matakatifu, lkn pia hata kipindi chote (Miaka 33) alichoishi Bwana Wetu YESU KRISTO hapa Duniani na hata kipindi cha Mitume, hatuoni kama kuna kipindi Bwana wetu Yesu au Mitume walishhiriki Birth-day ya BWANA WETU YESU KRISTO. Sasa hapo ndipo suali linakuja, je waanzilishi wa hii siku ya Kristmas walikuwa na kusudio gani? na ni kwa nini hii siku imekuwa na mwamko mkuu kiasi hiki katika IMANI YA KIKRISTO wakati hata kwenye BIBLIA TAKATIFU haijaonyeshwa kwamba tunapaswa kuisheherekea.
Nafahamu kwamba wapo wale watakaonibeza lkn hata Biblia inatuambia kwamba siku ile ATAKAPORUDI BWANA WETU YESU KRISTO KUWACHUKUA WATEULE WAKE kwenda nao MBINGUNI, hakutakuwa na sababu Ohooo mimi sikujua wala mimi nilikuwa naambiwa tu Viongozi wangu wa DINI (ambao naamini hata ukiwauliza kuhusu hii Kristmas watakosa Jibu la kukuambia, labda itakuwa ni Propaganda tu zisikokuwa na support ya kwenye Biblia Matakatifu). Na Biblia iko wazi zaidi kwa kusema; Watu wangu wanakufa kwa kukosa maarifa.
NB: Siamini kama ni makosa kujadili kitu muhimu kama hiki, kwani sioni tatizo la kueleweshana ktk suala ambalo lina mustakabali wa mambo yetu ya kiimani. Ndiyo maana hata katika baadhi ya Makanisa yetu kuna vipindi vya mjadala katika mambo mbalimbali ya kiimani.
Nawasilisha.
Mkristo wa 'KICHINA' 25th Dec SIO BIRTHDAY YA YESU acha kukariri mambo,ni siku ambayo wakristo hukumbuka kuzaliwa kwa Bwana YESU karibia miaka 2000 iliyopita.Ingekuwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa YESU isingetumika neno'karibia miaka...' ingekuwa unatajwa Umri husika wa YESU.Kama huamini kwamba YESU alizaliwa then huna sababu ya kukumbuka tendo hilo,pia unaweza kuchagua tarehe nyingine na mwezi mwingine kama unafikiri kweli Yesu alizaliwa nawe ufanye hiyo kumbukumbu.Wengi hawaelewi kuwa kesho sio bethdey ya yesu...
Sio mkristo wewe.,acha kupotosha watu! Kama huna kazi ya kufanya kalale
MIMI NI MKRISTO NINAYE-AMINI KWAMBA YESU ALIZALIWA NA BIKIRA MARIAM, AKAISHI DUNIANI KWA KIPINDI CHA MIAKA 33, AKAUAWA NA KUZIKWA NA ILIPOFIKA SIKU YA TATU ALIFUFUKA NA KWASASA YESU MBINGUNI NA ATAREJEA TENA KUWACHUKUA WALE WALIO WATEULE WAKE KWENDA NAO MBINGUNI KAMA BIBLIA INAVYOSEMA.
HII HABARI YA WEWE SIYO MKRISTO AU WA KICHINA KWASABABU YA SWALI AMBALO HATAHIVYO BADO HAMJALIJIBU; JE NI KWANINI TUNASHEHEREKEA KILA MWAKA 25 DESEMBA KAMA SIKU YESU ALIYOZALIWA? JE HAYA YANAPATA SUPPORT TOKA WAPI WKT KWENYE BIBLIA TAKATIFU HAYAPO? -ungenijibu katika hilo ungekuwa umenisaidia sana, kama una evidence ya kwenye Biblia, otherwise unajaribu kukwepa ukweli kwamba tunasheherekea Matakwa ya Kibinadamu na wala si mpango wa Mungu; kwani vipaumbele vyote muhimu katika ukombozi wa Mwadamu (kazi aliyokuja YESU Duniani kuifanya) vyote vipo kwenye BIBLIA TAKATIFU.
Nafahamu kuna watu hawapendi kujadili mambo ya kiimani kwasababu zao mbali mbali lkn lililojema ni lipi? na ni kwanini tunaruhusiwa kuwa na BIBLIA TAKATIFU na kushauriwa kukisoma? Je kama wote tungekuwa wavivu au kutopenda kusoma Biblia Takatifu, Je Waakristo Waprotestant wangekuwepo leo hii bila Martin Luther kufanya jitihada na Kusoma Biblia na kuelewa yaliyomo?
Mimi nafikiri tusibezane kwa maneno ya kejeli ktk mambo muhimu kama haya; wewe kama una facts za kutufanya tushehereke leo Desemba 25 kama sikukuu ya Kuzaliwa Yesu Kristo, tupe hizo facts zinazotoka kwenye BIBLIA TAKATIFU.
Halafu pia, neno la Mungu lina utaratibu, na hasa Ukristo, hivyo huwezi kunishawishi kwamba ni suala la mtu yeyote kujisikia ni lini na siku gani anasheherekea Kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Hiyo dhana ya uhuru huo unautoa wapi kwenye Biblia takatifu? Labda unishawishi kwamba wewe Biblia haikuhusu, na kama ndivyo basi hili swala nalo halikuhusu; kwani hili suala ni kwa wale WAKRISTO AMBAO BIBLIA TAKATIFU NDICHO KITABU KITAKATIFU na taratibu na Msingi wa Imani yao ipo kwenye Biblia Takatifu.
NB; H1N1 na Mwafrikahalisi; tafadhali rejea mada yangu hapo juu na uone kiini cha hoja yangu.
Mwanamke akishazaa atakuwaje bikira?
Kuna ushahidi gani kwamba Yesu aliishi actually na siyo a fictional character kama Willy Gamba au Superman?
Mkristo wa 'KICHINA' 25th Dec SIO BIRTHDAY YA YESU acha kukariri mambo,ni siku ambayo wakristo hukumbuka kuzaliwa kwa Bwana YESU karibia miaka 2000 iliyopita.Ingekuwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa YESU isingetumika neno'karibia miaka...' ingekuwa unatajwa Umri husika wa YESU.Kama huamini kwamba YESU alizaliwa then huna sababu ya kukumbuka tendo hilo,pia unaweza kuchagua tarehe nyingine na mwezi mwingine kama unafikiri kweli Yesu alizaliwa nawe ufanye hiyo kumbukumbu.Wengi hawaelewi kuwa kesho sio bethdey ya yesu...
Kuna ushahidi gani kwamba Yesu aliishi actually na siyo a fictional character kama Willy Gamba au Superman?
Ushaidi upo kwenye Biblia Takatifu. Manabii katika Agano la Kale wengi walitabiri kuzaliwa kwake na Katika Agano Jipya Vitabu vinne vya Injili (yaani Mathayo Mtakatifu, Marko Mtakatifu, Luka Mtakatifu na Yohana Mtakatifu) vyote vinaelezea Maisha ya Bwana wetu YESU KRISTO hapa Duniani. Na Vitabu vingine ambavyo vimeandikwa na Mitume kama Matendo ya Mitume, Warumi, Wakorintho, Wagalatia, n.k; vyote vinaelezea maisha ya YESU KRISTO NA MAMBO YOTE YANAYOHUSU UKOMBOZI WA MWANADAMU.