As long umeweka alama ya kuuliza yote yatajulikana muda ukifika lakini yaliyo dhahiri kubaki madarakani kwa hii dola (Samia/Ccm) bado ni tatizo kwa demokrasia ya kweli lkn kuondoka kwake pia kunaweza kuleta changamoto nyingine za muda mfupi na mrefu na kwa mtizamo wangu ni hizi hapa
Kuondoka kwa hii dola kunaweza kuleta makundi mengi yanayotaka powers na yanayotaka kuwa ndani ya unufaika toka mwanzo na hapa kuna vyama vya siasa, makundi ya kiraia na kiharakati bila kusahau taasisi za dini na tusipoangalia tunaweza tengeneza tena makundi hatari na umwagaji damu endelevu kwa yale makundi yatakayoona hayaendi kunufaika , unaweza pata picha hapa kwa yule Shehe na maneno yake
Mfano tuseme jeshi lichukue Nchi na kwa mazingira haya ninayo yaona inaweza pia kuleta mpasuko wa makundi kwenye hiyo taasisi wako watakao taka na kupambania mamlaka wao kwa wao na wengine wapo watakao ona himaya ya zamani imehujumiwa nalo ni tatizo jingine isije tukazisha Sudan nyingine
Mwananchi dhidi ya mwananchi huku napo kuna migawanyiko wapo wanona kuutoa huu utawala ndo mwanzo wa ukombozi halisi na uhuru lkn wapo wengi wanaona ni hujuma inafanywa kwa sababu za vikundi vichache kwa msukumo pia wa kutoka nje ili kuvuruga amani na mawakala hapa ni vyama vya siasa na hasa Chadema, wana harakati na wengi wao hao wenye ushawishi wapo nje ya Nchi na kuna taasisi za kidini hasa wanao toa waraka
Muungano pia utakuwa kwenye wakati mgumu kama dola hii itaanguka sasa ndo tujiulize zile sababu za kuwa na muungano za mwanzo bado zipo au hazipo , kuanzia za kiusalama wa eneo hili na mengineyo?
Muda ndo utaamua lkn yote kwa yote mambo hayatakuwa sawa kwa muda huu kwa kutoka madarakani na kubaki na kubwa ni ku calculate hizo risks na matokeo yake na sio kuendeshwa kwa mihemko tu
Na kwa sie tunaotaka amani tu tunabebwa bebwa tu na hatujui cha kufanya kwa makundi haya na wengine kwa kutaka kwetu amani wana tu label kama wasaliti na tunaishia kutukanwa tu bila sababu lakini tunashauri watu waweke silaha zao chini wakae kutafuta muafaka na maridhiano vinginevyo hakuna salama kwa wote sie na mtaichoma nchi yenu hii nzuri, ni ushauri tu