Design ya Sebule kuwa Chini halafu Vyumbani na Sehemu ya Chakula kuwa Juu

Ndugu wanamajilisi, hiyo "design" tajwa hapo Juu ndio Ujenzi wa Kisasa?
Au ni kipi hasa kinapelekea Mafundi wengi kushauri Ujenzi wa namna hiyo?
Halafu jiko liko chini au juu pia? Je nyumba ina family room pia au ni sitting room tu?

Ni vizuri sana iwapo juu itakuwa ni sehemu ya family tu, yaani bedrooms, family room, na bathrooms at least mbili: moja ndani ya master, na nyingine inayokuwa shared na vyumba vingine. Halafu floor ya chini inakuwa na garage, jiko,storage, laundry, dining, living room, guest room na public bathroom.
 
Hazungumzii gorofa.
 
Yeah ni nzuri ila hapa kwangu sio ngazi mbili ni moja tu, na naona panapendeza nikijenga kwangu ntaweka pia...au ishakua old fashion?
Nope...nilikuwekea picha nimeifuta kwangu iko hio two steps. Living room iko chini inakupa high ceiling
 
But watoto kama wamezaliwa hapo, wala hakuna shida. Wanazoea tu.

Kwa mijini (kama Dar, Arusha nk), kujenga nyumba isiyo ya ghorofa ni "ufisadi" wa ardhi. No?

Kwa sebule/dining kuwa same floor but levels tofauti nakubaliana na hoja lakini kwa sababu tofauti....inapunguza flexibility ya floor space husika. Zikiwa level moja, kunakuwa na flexibility kubwa zaidi kwenye matumizi.
 
Huo ni ujenzi wa kijadi wa nyumba za tembe za Wagogo nilioukuta maeneo mengi Dodoma. Unapoingia ndani ya nyumba unashuka sebuleni na kupata ubaridi. Pia dari liko karibu sana na usawa wa ardhi. Kwahiyo ukiichimbia sebule chini, dari linakuwa juu kidogo.

Kuna changamoto kubwa ya kuyatoa maji yakiingia sebuleni, panageuka dimbwi! Hata wanaopiga deki wanapata shida sana kukausha maji.

Labda pawepo namna ya kutoboa shimo la kutolea maji nje, lakini pia liwe linazibwa. La sivyo utakaribisha vyura, mijusi na hata nyoka!
 
Ndugu wanamajilisi, hiyo "design" tajwa hapo Juu ndio Ujenzi wa Kisasa?
Au ni kipi hasa kinapelekea Mafundi wengi kushauri Ujenzi wa namna hiyo?
Hii design ina leta sense au feeling ya ukubwa...hata eneo kama ni dogo..yaan sebule kama ndongo bas itaonekana kubwa...na nyumba itaonekana kubwa

Ni nzur sana ukiidesign ..angalia nyumba ya zamarad kwaa ndan..safi kabisa
 

Hizo ngazi tatu ndo ziwe tishio kwa watu hao, kwahiyo ghorofa ndo kabisa tujiepushe!
 

Bado kuna watu wanadeki kwa kusukuma maji mengi! Au unaongelea maji gani, mafuriko?[emoji16]

Siku hizi neno 'kupiga deki' limebadilishiwa maana, sebleni ni mwendo wa kufuta na kukausha tu.
 
Bado kuna watu wanadeki kwa kusukuma maji mengi! Au unaongelea maji gani, mafuriko?[emoji16]

Siku hizi neno 'kupiga deki' limebadilishiwa maana, sebleni ni mwendo wa kufuta na kukausha tu.
Kama umewahi kuziona hizo sebule za kigogo huwezi kuongelea kukausha maji unakokufikiria! Nazungumzia nyumba za tembe za kigogo ambazo hata paa si la bati, na sakafu ni udongo. Siyo nyumba unazofikiria wewe!

Kwa kukusaidia tu, jaribu kutembelea nyumba yenye sakafu ya udongo na sebule iwe chini, halafu imwagie maji, ndipo utaelewa changamoto niliyoiainisha
 

Basi mfano wako ni mzuri ila umeupachika pasipostahili, hoja mezani sio nyumba za tembe…. hata hizo za tembe hazina sakafu hivyo hazipigwi deki.

Ikiwa zimeingia maji (tuseme mafuriko), wenyewe wana namna yao ya kuyaondoa…. ndio maana wanajenga hivyo.
 
Kama ningazi moja ni nch 6

Sent from my TECNO WX4 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo watu wanalazimisha ile inataka nyumba yenye nafasi halafu pia mafundi wanakosea unakuta mtu ile step ameweka cm zaidi ya 15 lazima iwe hatari maana kitalam ngazi ni cm 15

Sent from my TECNO WX4 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…