Wonderful
JF-Expert Member
- Apr 8, 2015
- 7,347
- 5,986
Wachezaji hao sasa ni mali ya YANGA na wate wamemwaga wino kwa mkataba wa miaka 2.Niliwahi kutoa taarifa za Chanongo hapa takribani wiki moja iliyopita but nilikosea aka yake nikidhani ni Messi (RAMADHANI SINGANO)But alikua ni Chanongo na vikao vimeenda vema na atimae amesaini YANGA leo.YANGA MBELE DAIMA NYUMA MWIKO.-
UPDATES:KASEKE AKISAINI LEO ASUBUHI KUICHEZEA YANGA.
UPDATES:KASEKE AKABIDHIWA UZI No4 aliokua akiuvaa chuji.
=============================
=============================
UPDATES:KASEKE AKISAINI LEO ASUBUHI KUICHEZEA YANGA.
UPDATES:KASEKE AKABIDHIWA UZI No4 aliokua akiuvaa chuji.
=============================
=============================
KIRAKA mpya wa Yanga, Deus Kaseke, ametua klabuni hapo na mkwara wa mwaka.
Baada ya kutambulishwa tu, kiungo huyo akatamka mambo mawili. Kwanza, ametaka apewe jezi namba nne ambayo tayari Yanga wamempa, lakini pili anataka kocha amchezeshe winga wa kushoto, ili aweze kuifanyia makubwa klabu hiyo.
Habari za ndani ya Yanga awali zilisema kuwa Kaseke aliutaka uongozi umpe jezi hiyo kwani inampa nafasi ya kujisikia huru zaidi, lakini namba hiyo ilikuwa ikitumiwa na beki wa kati Rajab Zahir ambaye yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na Yanga ili kuongeza mkataba mpya.
"Mbali na kutaka apewe jezi namba 4 pia anasisitiza angependa kucheza winga wa kushoto akidai inamfanya ajiamini na kuisaidia timu kupata mabao kwani pia ni mfungaji mzuri," kilisema chanzo hicho.
"Katika suala hilo la jezi ndio utata zaidi kwani viongozi walimgomea kwa madai tayari inayo mtu ambaye ni Rajab Zahir, ambaye uongozi unaendelea kuzungumza naye kwa ajili ya usajili wa mkataba mpya."
Hata hivyo katika mkutano wao na wanahabari mchana wa jana, uongozi wa Yanga ulifichua kuwa umempa kiungo huyo mpya mkataba wa mwaka mmoja na kuridhia ombi lake la kutaka apewe jezi namba 4 kama alivyotaka.
"Kaseke atavaa jezi namba 4 na mkataba wake ni wa mwaka mmoja. Wengine ambao mpaka sasa tumewasajili ni kipa Deo Munishi ‘Dida' ambaye tumempa mktaba wa miaka miwili kama ilivyo kwa Haruna Niyonzima, huku Mbuyu Twite akipewa mkataba wa mwaka mmoja," alisema Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh.
Aidha menejja huyo aliweka bayana kwamba Yanga itaanza kambi ya mazoezi kujiandaa na msimu mpya Juni 8, ikiwa ni siku mbili tu tangu Kocha Mkuu, Hans Pluijm kurejea kutoka kwenye mapumziko nyumbani kwake Ghana.
Katika hatua nyingine, Yanga inajipanga kuhakikisha inafanya kweli katika mashindano ya Kombe la Kagame, ikipiga mahesabu ya kuzishusha timu tatu kubwa barani Afrika za Zesco ya Zambia, TP Mazembe na Mamelodi Sundwons ya Afrika Kusini, ili kufanya mashindano mafupi.
Chanzo: MwanaSpoti