Deus Kaseke na Haruna Chanongo watua Yanga SC

Deus Kaseke na Haruna Chanongo watua Yanga SC

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
Wachezaji hao sasa ni mali ya YANGA na wate wamemwaga wino kwa mkataba wa miaka 2.Niliwahi kutoa taarifa za Chanongo hapa takribani wiki moja iliyopita but nilikosea aka yake nikidhani ni Messi (RAMADHANI SINGANO)But alikua ni Chanongo na vikao vimeenda vema na atimae amesaini YANGA leo.YANGA MBELE DAIMA NYUMA MWIKO.-


UPDATES:KASEKE AKISAINI LEO ASUBUHI KUICHEZEA YANGA.

UPDATES:KASEKE AKABIDHIWA UZI No4 aliokua akiuvaa chuji.

=============================
=============================


KIRAKA mpya wa Yanga, Deus Kaseke, ametua klabuni hapo na mkwara wa mwaka.

Baada ya kutambulishwa tu, kiungo huyo akatamka mambo mawili. Kwanza, ametaka apewe jezi namba nne ambayo tayari Yanga wamempa, lakini pili anataka kocha amchezeshe winga wa kushoto, ili aweze kuifanyia makubwa klabu hiyo.

Habari za ndani ya Yanga awali zilisema kuwa Kaseke aliutaka uongozi umpe jezi hiyo kwani inampa nafasi ya kujisikia huru zaidi, lakini namba hiyo ilikuwa ikitumiwa na beki wa kati Rajab Zahir ambaye yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na Yanga ili kuongeza mkataba mpya.

"Mbali na kutaka apewe jezi namba 4 pia anasisitiza angependa kucheza winga wa kushoto akidai inamfanya ajiamini na kuisaidia timu kupata mabao kwani pia ni mfungaji mzuri," kilisema chanzo hicho.

"Katika suala hilo la jezi ndio utata zaidi kwani viongozi walimgomea kwa madai tayari inayo mtu ambaye ni Rajab Zahir, ambaye uongozi unaendelea kuzungumza naye kwa ajili ya usajili wa mkataba mpya."

Hata hivyo katika mkutano wao na wanahabari mchana wa jana, uongozi wa Yanga ulifichua kuwa umempa kiungo huyo mpya mkataba wa mwaka mmoja na kuridhia ombi lake la kutaka apewe jezi namba 4 kama alivyotaka.

"Kaseke atavaa jezi namba 4 na mkataba wake ni wa mwaka mmoja. Wengine ambao mpaka sasa tumewasajili ni kipa Deo Munishi ‘Dida' ambaye tumempa mktaba wa miaka miwili kama ilivyo kwa Haruna Niyonzima, huku Mbuyu Twite akipewa mkataba wa mwaka mmoja," alisema Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh.

Aidha menejja huyo aliweka bayana kwamba Yanga itaanza kambi ya mazoezi kujiandaa na msimu mpya Juni 8, ikiwa ni siku mbili tu tangu Kocha Mkuu, Hans Pluijm kurejea kutoka kwenye mapumziko nyumbani kwake Ghana.

Katika hatua nyingine, Yanga inajipanga kuhakikisha inafanya kweli katika mashindano ya Kombe la Kagame, ikipiga mahesabu ya kuzishusha timu tatu kubwa barani Afrika za Zesco ya Zambia, TP Mazembe na Mamelodi Sundwons ya Afrika Kusini, ili kufanya mashindano mafupi.

Chanzo: MwanaSpoti
 

Attachments

  • images-1.jpeg
    images-1.jpeg
    9.4 KB · Views: 1,020
  • images-20.jpeg
    images-20.jpeg
    5.7 KB · Views: 2,807
  • kaseke.jpg
    kaseke.jpg
    7.5 KB · Views: 2,610
  • kaseke+tambulishwa+2.jpg
    kaseke+tambulishwa+2.jpg
    6.8 KB · Views: 1,472
Karibuni jangwani madogo mufanye kaz iliyowaleta.
 
Kwan dirisha c hua waz lig ikiisha tu,au tz tofaut
 
SO WHAT?.....Wachezaji wenyewe mnawakopa hamna uwezo wa kuwalipa mishahara
 
chanongo Simba wamemkataa hata bure, Ni mchezaji ambaye hajitambui anaweka ushabiki wake kwa yanga mbele kama mliangalia mechi kati ya stand united dakika ya 92 alishndwa kufunga akiwa yeye na goli maana kipa alishaenda malikiti...
 
pole sana!!

Sawa endelea na updates zako kwanza mi sio mshabiki wa mikia kama kweli yanga wamechukua hao vilaza wamenikera bado hawajafikia hadhi ya yanga tuko na hitaji la wachezaji lakini sio kama hao
 
Yanga inasajili kwa ajili ya ligi yetu ya kombe la mbuzi au kushindana na timu kama Tp Mazembe na Zamalek?
 
Kuhusu haruna chanongo yanga wamelamba dume coz ni mchezaji mwenye kasi kama ya kina msuva na ngasa,so ni mchezaji anaeendana na falsafa yetu..
 
chanongo Simba wamemkataa hata bure, Ni mchezaji ambaye hajitambui anaweka ushabiki wake kwa yanga mbele kama mliangalia mechi kati ya stand united dakika ya 92 alishndwa kufunga akiwa yeye na goli maana kipa alishaenda malikiti...

lakini mbona ashawahi kuifunga yanga huyu?
 
Lakini hao wachezaji ni mahitaji ya kocha au ya viongozi,
kwa maana Deus Kaseke na huyo Peter Mwalyanzi aliyesaini simba walikuwa kama mpira wa kona kwa Yanga na Simba,
Ngoja tusubili kama watatusaidia.
 
Lakini hao wachezaji ni mahitaji ya kocha au ya viongozi,
kwa maana Deus Kaseke na huyo Peter Mwalyanzi aliyesaini simba walikuwa kama mpira wa kona kwa Yanga na Simba,
Ngoja tusubili kama watatusaidia.

Simba wamesajili kwa fasion kwa sabb midfield wanao wengi na wazuri but yanga wameshugulika na kuziba pengo la ngasa
 
Simba wamesajili kwa fasion kwa sabb midfield wanao wengi na wazuri but yanga wameshugulika na kuziba pengo la ngasa


Mkuu kama ni mahitaji ya mwalimu hakuna shida kwani ndo anajua mchezaji yupi anafaa nafasi ipi?
 
Sawa endelea na updates zako kwanza mi sio mshabiki wa mikia kama kweli yanga wamechukua hao vilaza wamenikera bado hawajafikia hadhi ya yanga tuko na hitaji la wachezaji lakini sio kama hao

kwa mfano mchezaji gani wa nchi hii anafaa kusajiliwa yanga?.
 
Back
Top Bottom