Mchambuzi wa masuala ya Siasa Deus Kibamba amesema kwa mazingira ya sasa, ni ngumu kupata mchunguzi wa ndani atakayeaminika na pande zote, isipokuwa ni busara pande zote zikaridhia kupata mchunguzi huru kutoka nje ya nchi huku akirejelea hotuba ya Rais Samia siku chache zilizopita akieleza kuunda Tume itakayofanya uchunguzi kwa matukio na vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025
Amesema kwa sasa kumekuwa na tatizo la kutoaminiana kwa wadau mbalimbali, na kwamba katika mazingira ya aina hiyo ili kupata muafaka wa Kitaifa na kupata taarifa zaidi za kiuchunguzi ni vyema taasisi huru ya nje ya nchi ikafanya kazi hiyo
Kibamba ameeleza hayo leo Novemba 18, 2025 akiwa katika mahojiano na Jambo TV