Uchaguzi 2020 Devotha Minja afuata nyayo za Lema na Mdee, aweka clip ya Magufuli akimshambulia Abood Aziz

Uchaguzi 2020 Devotha Minja afuata nyayo za Lema na Mdee, aweka clip ya Magufuli akimshambulia Abood Aziz

DT125

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
437
Reaction score
637
Mgombea ubunge wa Morogoro mjini kupitia Chadema Mhe. Devotha Minja katika mikutano yake amekuwa akikatisha hotuba zake kwa kuweka clip ya sauti ya Magufuli. Katika clip hiyo anasikika Mhe. Rais Magufuli akimshambulia Abood mbunge wa CCM awamu iliyopita na aliyepitishwa tena na CCM akiomba miaka 5 tena.

Mhe. Magufuli akihutumbia wafanyabiashara wa stendi ya mabsi ya Msamvu alimshambulia Abood kwa kugeuza shughuli za viwanda alivyobinafishiwa na kugeuza kuwa mazizi ya mifugo yake huku Watanzania wakikosa ajira. Anasikika Magufuli akisema " kuna mbunge wa hapa wa CCM amegeuza kiwanda kuwa zizi huku akiwakosesha ajira". Mhe. Devotha Minja ambaye ni mtangazaji wa zamani wa ITV na mbunge wa viti maalum wa awamu iliyopita amerudishwa na NEC baada ya kukata rufaa kwani awali Mhe. Abood alishatangazwa kupita bila kupingwa.

Mchuano unaonekana kuwa mkali Kati ya wagombea hawa licha ya Abood kufanya kazi za ubunge kama mfadhili lakini hana uwezo wa kujenga hoja na ushawishi kwa wapiga kura awapo majukwani. Wafuatiliaji wa mchuano huu wanadai kuwa Devotha Minja anaweza shinda kutokana na kuungwa mkono na akina mama wengi na wafanyabiashara wengi Wa kichaga ambao ndiyo sehemu kubwa ya wafanyabiashara hapa Morogoro.

Sababu nyingine inayotajwa ni mgawanyiko mkubwa wa wana CCM, wale waliokosa kuwekwa kwenye kundi la kampeni wamekuwa wasaliti kwa kukosa pesa ya posho ya mfanyabiashara huyu wa mabasi na mafuta. WanaCCM wengi wamekuwa wakionekana kwenye mikutano ya Devotha Minja.
 
Go Devota, sijawahi kusikia sauti ya Abood mjengoni mbali ya kuona mikono akipiga meza. Wanamoro na Watanzania tunahitaji sauti ya Madam Devota mjengoni. Ushauri wangu kwa Abood na wengine wapiga makofi, wanaweza kutumikia jamii kwa kuanzisha NGOs, jifunzeni kwa Late mzee Mengi.
 
Huyo mama bora hiyo hela angewekeza kwenye biashar, Abood hawezi kumshinda, tena Morogoro kwa waluguru na wapogoro hahaha, anapoteza muda
 
Devota yuko vizuri kuliko Abood kwa hoja na sera ila kushinda kwa sasa ni ngumu
 
Kukata viuno majukwaani ndio Sera ya CCM?
Hizi ndiyo sera za CCM
JamiiForums-1343039852.jpg
 
Chadema chama cha Mbowe hovyo kabisa, wao wanadhani itasasaidia hiyo technique never. Watanzania hawawezi chagua manyumbu wanaoshikiwa akili na mwenyekiti.

Hivi wewe kiazi, kushikiliwa akili na mwenyekiti anayejitambua mbona ni nafuu kuliko baadhi ya tamthilia za vichekesho?
Kuna watu nikiambiwa huyu ni mwenyekiti wako naweza kuangua kilio.
 
Huyo mama bora hiyo hela angewekeza kwenye biashar, Abood hawezi kumshinda, tena morogoro kwa waluguru na wapogoro hahaha, anapoteza muda
Waluguru achana nao, wajumbe hata Al-Saedy walimpiga chini, kisa hawapi mabasi wakazikie, sasa Devo kiukweli anapoteza muda...atapata kura lakini hatoshinda!

Mpaka wananchi watakapoelimishwa, tofauti kati ya mfadhili na mbunge, wakapata ufunuo juu ya majukumu ya mbunge, mfadhili na wajibu wa serikali, yote ni ubatili.
Serikali haiwezi kuja na sensitization ya namna hiyo.
Ndiyo maana kina Gwaji wanakuja na sera jinga za kupeleka watu Marekani.

Everyday is Saturday.............................. 😎
 
Huyo mama bora hiyo hela angewekeza kwenye biashar, Abood hawezi kumshinda, tena morogoro kwa waluguru na wapogoro hahaha, anapoteza muda

Jimbo la Waluguru hilo, siyo Wapogoro.
 
majukwaani ndio Sera ya CCM?
CCM kupitia H. Polepole imesema wazi, kipindi cha kampeni, kwenye mikutano yake itakuwa inafanya mambo mawili. Moja kufanya sherehe ya kujipongeza kwa mafanikio makubwa iliyopata katika utekelezaji wa ilani yake ya 2015 (ni wakati huu wasanii mbali mbali ujumuika kutoa burudani kwa walioudhuria). Pili ni kutoa ufafanuzi wa ilani ya Chama ya mwaka huu na maono waliyonayo wagombea wa ngazi husika katika uchaguzi huu.

Leta hoja nyingine!
 
Back
Top Bottom