Uchaguzi 2020 Devotha Minja afuata nyayo za Lema na Mdee, aweka clip ya Magufuli akimshambulia Abood Aziz

Uchaguzi 2020 Devotha Minja afuata nyayo za Lema na Mdee, aweka clip ya Magufuli akimshambulia Abood Aziz

Mgombea ubunge wa Morogoro mjini kupitia Chadema Mhe. Devotha Minja katika mikutano yake amekuwa akikatisha hotuba zake kwa kuweka clip ya sauti ya Magufuli. Katika clip hiyo anasikika Mhe. Rais Magufuli akimshambulia Abood mbunge wa CCM awamu iliyopita na aliyepitishwa tena na CCM akiomba miaka 5 tena.

Mhe. Magufuli akihutumbia wafanyabiashara wa stendi ya mabsi ya Msamvu alimshambulia Abood kwa kugeuza shughuli za viwanda alivyobinafishiwa na kugeuza kuwa mazizi ya mifugo yake huku Watanzania wakikosa ajira. Anasikika Magufuli akisema " kuna mbunge wa hapa wa CCM amegeuza kiwanda kuwa zizi huku akiwakosesha ajira". Mhe. Devotha Minja ambaye ni mtangazaji wa zamani wa ITV na mbunge wa viti maalum wa awamu iliyopita amerudishwa na NEC baada ya kukata rufaa kwani awali Mhe. Abood alishatangazwa kupita bila kupingwa.

Mchuano unaonekana kuwa mkali Kati ya wagombea hawa licha ya Abood kufanya kazi za ubunge kama mfadhili lakini hana uwezo wa kujenga hoja na ushawishi kwa wapiga kura awapo majukwani. Wafuatiliaji wa mchuano huu wanadai kuwa Devotha Minja anaweza shinda kutokana na kuungwa mkono na akina mama wengi na wafanyabiashara wengi Wa kichaga ambao ndiyo sehemu kubwa ya wafanyabiashara hapa Morogoro.

Sababu nyingine inayotajwa ni mgawanyiko mkubwa wa wana CCM, wale waliokosa kuwekwa kwenye kundi la kampeni wamekuwa wasaliti kwa kukosa pesa ya posho ya mfanyabiashara huyu wa mabasi na mafuta. WanaCCM wengi wamekuwa wakionekana kwenye mikutano ya Devotha Minja.
Sijui sisi watanzania tulikua wapi kudai tume ya Uchaguzi , majirani zetu Kenya wanashangaa, mgombea ndiye anayeteua wajumbe, wakurugenzi na makamishna wa tume kweli tutegemee mkurugenzi atamwangusha aliyempa ugali?? Tuamke tuamke
 
Huyo mama bora hiyo hela angewekeza kwenye biashar, Abood hawezi kumshinda, tena Morogoro kwa waluguru na wapogoro hahaha, anapoteza muda
Kwanini alienguliwa kama si tishio, huu ni upotolo
 
Sio ngumu tu, HAWEZI...

Uongozi sio mdomomdomo mtupu
Tangu CCM ilivyokutelekeza njaa imekufanya uwe na hoja duni sana ! sasa abood kuwapa magari mkazikie ndugu zenu waliokufa kwa umasikini ndio uongozi huo ?
 
Back
Top Bottom