Devotha Minja: Namshangaa Hussein Bashe kutaka Bodaboda za Maafisa Ugani zifungwe GPS

Devotha Minja: Namshangaa Hussein Bashe kutaka Bodaboda za Maafisa Ugani zifungwe GPS

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
"Namshangaa Hussein Bashe anataka pikipiki za maafisa Ugani zifungwe GPS, mbona wao kwenye V8 zao hawajafungiwa" Devotha Minja. Mbunge wa wananchi Jimbo la Morogoro Mjini.


Chanzo: Jambo TV

===
Devotha Minja, ambaye alikuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kwa tiketi ya CHADEMA amekosoa mapendekezo ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ya Kufunga GPS kwenye pikipiki za maafisa ugani akisema huo ni mradi wa mtu wa kupiga hela.

Amesema suala hilo halina msaada wowote wala tija. Ametolea mfano kuwa afisa ugani akiwa na mwenzi wake ambaye anaumwa atashindwa kutumia pikipiki hiyo kwa kuwa imefungwa vifaa hivyo hali ambayo itaondoa motisha kwa maafisa ugani.

Amesema mawaziri wana magari mazuri kwa matumizi yao binafsi na wanajaribu kuwabana maafisa ugani kwa masuala madogo.
 
Lazima uwe na pa kuanzia,

Tukianza na hao maafisa ugani tutakwenda kila sehemu mpaka kwa mawaziri,

Its a good idea, it only needs implementation
 
Sizan kama zinazuia kitu kadude kenyewe hakana kamera kapo tu kama kisikizo cha koti la suti unakanatisha sehem bas, sasa hako ndio kazuie mbona nakatoa nakaweka geto naendelea kula misele wao watajua chombo nimepaki
Inategemea umewekewa ipi,,,, ziko za aina tofauti,,, kuna nyingine kuitoa tu kwanza tayari inatoa taarifa
 
Huyo mama kaona mbali hapo aliposema itakua ni dili la mtu.kwasababu siku zote iko hivyo.kuna mavifaa mengi yanatengenezwa uko ulaya na china na soko lake kubwa liko afrika.Viongozi wanakuja kuvipigia debe vinanunuliwa kwa fujo ila baada ya miaka michache vinakua havina tena cha maana na wala hutasikia kikizungumziwa tena.watu wameshapiga ela yao wanawaangalia tu mmejazana na mavifaa yasiyo kazi stoo.mifano iko mingi sana.
 
Back
Top Bottom