GPS ni hatua nzuri sana ya ku monitor utendani kazi wa Wagani."Namshangaa Hussein Bashe anataka pikipiki za maafisa Ugani zifungwe GPS, mbona wao kwenye V8 zao hawajafungiwa" Devotha Minja. Mbunge wa wananchi Jimbo la Morogoro Mjini.
Chanzo: Jambo TV
===
Devotha Minja, ambaye alikuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kwa tiketi ya CHADEMA amekosoa mapendekezo ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ya Kufunga GPS kwenye pikipiki za maafisa ugani akisema huo ni mradi wa mtu wa kupiga hela.
Amesema suala hilo halina msaada wowote wala tija. Ametolea mfano kuwa afisa ugani akiwa na mwenzi wake ambaye anaumwa atashindwa kutumia pikipiki hiyo kwa kuwa imefungwa vifaa hivyo hali ambayo itaondoa motisha kwa maafisa ugani.
Amesema mawaziri wana magari mazuri kwa matumizi yao binafsi na wanajaribu kuwabana maafisa ugani kwa masuala madogo.
Mbona ubishi huo hauna Tija?
By the way
Haikatazwi kufanya kazi nyingine lakini awe wazi na awe na Sababu!