Dhahabu kilo 53 yakamatwa uwanja wa ndege wa Mumbai kutoka kwa wasafiri waliotoka Tanzania

Dhahabu kilo 53 yakamatwa uwanja wa ndege wa Mumbai kutoka kwa wasafiri waliotoka Tanzania

Naomba uisome vizuri tena hii habari yako hapa juu ya usahihi wake.
Si jambo jema tuendelee kuzungushana hapa kwa kutafuta njia za kupotosha kilichoandikwa.

Hao wahindi "waliinunua hiyo dhahabu Doha"?
Sasa kama ilikuwa ni mali imenunuliwa kihalali, hao kwenye uwanja wa Mumbai walikuwa na taizo gani na mali halali?
Smuggling ni kuingiza Mali bila kui declare kwa kuepuka Kodi na vitu vingine kama hivyo..... Ila article hakuna mahala imesema Dhahabu ni ya Tanzania just take a screenshot uweke hapa mjadala uishe!!
 
Kupiga kelele kwenye TV Kuna impact Gani?

1. Nani aliyekamatwa kwa Wizi wa Makinikia Hadi Leo?

2. Mpaka anafariki mbona hakuwa amedai Trillion 450 zetu?

3. Mwanyika tuliyeambiwa ame facilitate wizi wa Makinikia alimpigia kampeni na pia kampa Ubunge wa Makambako.

4. Mpaka anafariki Makinikia yalikua Bado yanasafirishwa nje.

5. Mpaka anafariki Sheria yake ya permanent sovereignty ilishakua imefanyiwa ammendments kibao ikiwemo kuondoa kipengele Cha mashauri ya madai kusikilizwa na mahakama za humu ndani.

6. Licha ya kujenga ukuta tuliambiwa na ripoti ya ukaguzi huko Mererani kuwa madini yaliibwa chini ya ukuta JPM akiwa Rais.

7. Tunaambiwa kitalu Cha serikali kilivamiwa na watu binafsi kuchimba Tanzanite wakati ni reserve for future govt repository!!

Sasa Kama haya yote yamefanyika Kuna faida Gani ya kutoa mapovu kwenye TV huku reality ni tofauti? Au unaona Raha Mama Samia apinge ufisadi kwenye screen huku madini yanatoroshwa kwako wwe inakua enough?
Nimetokea kukuelewa kivingine kabisa leo kuliko nilivyowahi kukuelewa humu JF.

Unaponisoma naomba uwe unaelewa ninachoeleza. Nimeeleza wazi kuwa Magufuli pamoja na mambo yake mengi ya hovyo, lakini alionyesha nia na dhamira, na kwamba katika njia zake alizojaribu, nyingi zilikuwa na mapungufu. Lakini watu waliona dhamira ya alichonuia kukifanya, iwe kashindwa au vinginevyo, lakini alionyesha aliposimamia.

Kama alipiga kelele nyingi huku akiwa hana dhamira ya kuyaondoa hayo maovu, mimi sijui, lakini naona wewe unajua.
 
Nimesoma story yote, inaeleza kwamba mzigo walipewa doha wakati wa transit si kwamba walitoka nao Tanzania. Kwa TZ huwezi pita na gold airport kirahisi.

Gold na madini mengi ya tz yanatoroshwa nje kupitia njia ya maji na njia za boda (land)
Unajua kiingereza mkuu, rudia kusoma kwa makini,, jamaa wametokea nchini kwetu
 
Ari Mpya Nguvu mpya kazi iendelee ya upigaji wa Rasilimali zetu.
 
Smuggling ni kuingiza Mali bila kui declare kwa kuepuka Kodi na vitu vingine kama hivyo..... Ila article hakuna mahala imesema Dhahabu ni ya Tanzania just take a screenshot uweke hapa mjadala uishe!!
Na hiyo article haijasema popote kwamba ni kweli kwamba hao watu walinunua hiyo dhahabu huko Doha kabla ya kuisafirisha hadi India.Makala haijathibitisha mahali popote kwamba kuna mtu kutoka Sudan alieuza hiyo dhahabu.

Hiyo makala haijasema mahali popote kuwa hao watu hawakutoka na dhahabu toka Tanzania walikotokea.
 
ane hapa kwa jambo ambalo liko wazi.
Magufuli pamoja na ukichaa wake huwezi kumfananisha na Kikwete au huyu Samia katika eneo hili, na hata wewe hilo unalijuwa.
Sijui ni wapi umenisoma katika mistari hiyo hapo juu nikiitetea CCM.
Ila ninachokiona hapa kwa upande wako ni juhudi za kumtetea Samia katika madhaifu yake makubwa sana katika eneo hili na mengineyo.
Tutapata hasara sana chini ya utawala wake huu.
Nimtetee Samia kwa lipi? Mimi nachopinga ni kujifanya CCM imewahi kuwa safi.

Kipindi cha JPM unaweza nitajia nani alifungwa kwa wizi wa Makinikia au Tanzanite? Unaweza nieleza kwanini Mwanyika alipewa ubunge
 
Mkuu 'zitto junior', tusizungushane bure hapa. Unaponitaka mimi nitaje hayo unayoyasema hapa unanipa kazi ambayo siiwezi, nawe unaelewa hivyo.
Ninayoandika kuhusu Magufuli, ni juu ya swala hilo hilo moja ambalo niliona mwelekeo, hata kama matokeo yake hayakuwa kama yalivyotegemewa.
 
Na hiyo article haijasema popote kwamba ni kweli kwamba hao watu walinunua hiyo dhahabu huko Doha kabla ya kuisafirisha hadi India.Makala haijathibitisha mahali popote kwamba kuna mtu kutoka Sudan alieuza hiyo dhahabu.

Hiyo makala haijasema mahali popote kuwa hao watu hawakutoka na dhahabu toka Tanzania walikotokea.
We jamaa Nina wasiwasi na account Yako siku hizi!! Imekua hacked ama?

Screenshot_20221114_181824.jpg
 
Mkuu 'zitto junior', tusizungushane bure hapa. Unaponitaka mimi nitaje hayo unayoyasema hapa unanipa kazi ambayo siiwezi, nawe unaelewa hivyo.
Ninayoandika kuhusu Magufuli, ni juu ya swala hilo hilo moja ambalo niliona mwelekeo, hata kama matokeo yake hayakuwa kama yalivyotegemewa.
Nakuheshimu sana mkuu na ni mmoja ya watu wenye reasoning kubwa sana humu JF and u know that.... ila kwa hili naona umeteleza!! CCM Bado walikua wanaiba sana hivi umesahau Mbunge wa Kishapu si alikutwa na hatia ya ujangili How comes akarudishwa bungeni na JPM? Mwanyika ametusababishia hasara ya Trillion 450 kivipi apewe ubunge na JPM?!

Ukinijibu hayo ndio nitaamini JPM alizuia mafisadi ya CCM
 
Dhahabu toka Tanzania imekamatwa Ijumaa iliyopita toka kwa abiria wa kihindi aliyetoka Tanzania.

Dhahabu hiyo imenukuliwa kuwa kiasi cha kilo 61 toka kwa abiria wanne(sasa imeelezwa kuwa ni abiria saba).
Hii ni syndicate.

Maafisa wa Customs India waliwakamata wahindi hao na kiasi hicho cha dhahabu, sisi Customs wetu wanahongwa tu.

Mama Tanzania tumekwisha.

Sad
 
Nimetokea kukuelewa kivingine kabisa leo kuliko nilivyowahi kukuelewa humu JF.

Unaponisoma naomba uwe unaelewa ninachoeleza. Nimeeleza wazi kuwa Magufuli pamoja na mambo yake mengi ya hovyo, lakini alionyesha nia na dhamira, na kwamba katika njia zake alizojaribu, nyingi zilikuwa na mapungufu. Lakini watu waliona dhamira ya alichonuia kukifanya, iwe kashindwa au vinginevyo, lakini alionyesha aliposimamia.

Kama alipiga kelele nyingi huku akiwa hana dhamira ya kuyaondoa hayo maovu, mimi sijui, lakini naona wewe unajua.
Hakua na Nia yoyote ila ilikua ulaghai Ili ku create perception kwamba ni Mkombozi..... Hivi angekua na Nia njema angemuacha Mwanyika? Angemuacha Chenge? Angemuacha Kafumu ama Ngeleja uraiani?

Ni ajabu sana great thinker kuingizwa mkenge na wanasiasa na kibaya zaidi ukaamini Kulikua na Nia ya dhati kukomesha ufisadi!!!? Like seriously? Eti Tegeta Escrow walikamatwa Singh na Ruge ila HAKUNA hata mwana CCM mmoja aliyekutwa na hatia kwenye kashfa Ile!!! Eti nia ya dhati? Excuse me
 
We jamaa Nina wasiwasi na account Yako siku hizi!! Imekua hacked ama?
Hapana, haijawa 'hacked', ila unanisoma kivyako, pengine kutokana na misimamo yako mipya juu ya maswala kama haya.
Wewe na mimi hatujui/hatuna uhakika wa ilikotokea hiyo dhahabu. Hapo Arabuni hawana machimbo ya dhahabu. Wanachoweza wao ni kuisafisha iwe katika hali hiyo.
Makala haijaeleza zaidi ya kuripoti tu kilichoelezwa, pengine na hao hao wasafiri, kwa hiyo haitoi uhakika wa ilikotoka hiyo dhahabu.
 
Dhahabu toka Tanzania imekamatwa Ijumaa iliyopita toka kwa abiria wa kihindi aliyetoka Tanzania.

Dhahabu hiyo imenukuliwa kuwa kiasi cha kilo 61 toka kwa abiria wanne(sasa imeelezwa kuwa ni abiria saba).
Hii ni syndicate.

Maafisa wa Customs India waliwakamata wahindi hao na kiasi hicho cha dhahabu, sisi Customs wetu wanahongwa tu.

Mama Tanzania tumekwisha.

Zile scanner baada ya Jiwe kudancha nazo zikadancha

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 
Nimesoma story yote, inaeleza kwamba mzigo walipewa doha wakati wa transit si kwamba walitoka nao Tanzania. Kwa TZ huwezi pita na gold airport kirahisi.

Gold na madini mengi ya tz yanatoroshwa nje kupitia njia ya maji na njia za boda (land)
Mnengene, unatetea ama unafahamu unachokiandika kwa ufahamu? Mizigo inapitishwa bwa shee

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom