Nadhani wakati umefika tupatiwe Kituo cha Benki Kuu. “Jana (juzi) tukiwa Chato, watu wa benki wale wanunuzi wa pamba walisema kuna tatizo la pesa. Mimi nalijua kwa muda mrefu, benki hizi nyingi zinapoagiza kutoka Mwanza (Tawi la Benki Kuu ya Tanzania) inachukua zaidi ya siku mbili kupata pesa. Tunaomba tupate kituo cha Benki Kuu kama ilivyo Shinyanga (Kahama) ili kurahisisha matumizi ya pesa katika mji huu. “Lakini pia kutokana na kustawi kwa mji huu, tumewasilisha mezani kwako ombi la kuwa Manispaa,” alisema.