Dhahama ya kuchakachua..

Dhahama ya kuchakachua..

Kama kawaida yako unapenda cha mwisho tu. Cha kwanza kwani hujakipenda? Au haraka haraka na papara zako?

cha kwanza chako kwani unachukuaga hata dk 2, vya kuendelea ndio unanigusa panapo.
 
Dada yangu aliandika hiviiiii
hicho kipengele cha mwisho MJ1 nimekipenda sana...

Nami nikamuuliza hiviiii
Kama kawaida yako unapenda cha mwisho tu. Cha kwanza kwani hujakipenda? Au haraka haraka na papara zako?

Sasa angalieni nilivyojibiwa sasaaaaaaa
cha kwanza chako kwani unachukuaga hata dk 2, vya kuendelea ndio unanigusa panapo.

Ndugu zangu njooni mniokoe kwenye makucha makali ya dada yangu! LOL
 
Mh huku nahisi kama nimepotea njia! :confused2::confused2:
Am sure MJ1 nimemuelewa vizuri lakini the rest mnanichanganya>>>:A S-confused1::A S-confused1::sleepy::sleepy:
you have put a smile on my face

thansk MM
 
Kwanza nakiri sikuwahi hata sikumoja kuhisi kuwa kamanda Acid na Babu yangu Asprin wanajua hata kutunga mstari mmoja... leo mmenishangaza wapenzi lol aksanteni sana.
 
binaadamu wanjanja, wazuri wa kuigiza
kitu kimoja kianza, vyengine vitamaliza,
mafuta yalivyofanzwa, mapenzi yaendeleza
mapenzi kuchakachua, ni ujuzi wa kuwaza.

sheria za ubunifu, chanzoni hazijatanzwa
iwe kwa muuza beef, au muokota chenza
utapita usanifu, mawazo kuendeleza
mapenzi kuchakachua, ni ujuzi wa kuwaza

maashallah dada G, tano pia nakupa
umechapa kama G, wala si tapatapa
kama spoti basi G, ndiyo uliyochapa
umenena neno jema, hakuna cha kuboresha

Nakupa gwara mazee
 
Mapenzi ya chakachua, sababuye wanawake,
Kujifanya wanajua, wachanganya na makeke,
Kisha waangukia pua, kila kitu mwakemwake,
Mapenzi ya chakachua, Hapa ni nyumbani kwake.

Babu yangu Sipirini, wote tuko lawamani
Hata si ya sirini, chakachua mapenzini
wote tuko kundini, si peke mke asilani
Kila wafanyacho wake, hujibu mapigo ya ngoma

Kama hakukuwa na wachakachuaji watu wasingechakachuliwa jamani babu au nakosea? Ni sawa na kuwaamuru mainfidelatees waache infedility wakati infidelators wapo! Bila Infidelators infidelatee atainfidelate na nani? Hapa nachokoza nyuki mamaa-naomba wasiione hii hawa memberz
 
Acid

lazima Mwanajamii1 akubaliane na sheria za ubunifu 🙂
 
kamanda wenda mrama, hii sasa nakujuza
tena chepuka mapema, kwani wewe si ajuza
pitia sheria mama, kile chama chapendeza
chakachua sio infi, na infi si chakachua

Hahahahaa naona nimekushika pabaya Kamanda...... nipe tofauti ya chakachua na infii tafadhali loh


chunguza sana kwa ndani, halafu pima imani
infi hurejesha amani, na pia huleta imani
infi ni jenuini, chakachua ina "lakini"
chakachua sio infi, na infi si chakachua

Infi huleta amani, kwao wasojua penzi
Sijaribu kwa fulani, anojua mapenzi
Hisia ikiwa moyoni, nataka penzi ulienzi
Infii ni chakachua, ni penzi liso hisia kamanda !!

Kiziangalia sheria, za infii zinavyosema
si kama penzi huria, infii hatakiwi sema
Hutakiwi fikiria, fidileta kwa mtima
Infii ni chakachua, ni penzi liso hisia kamanda!!

wa infi hutoa yote, chakachua haiwezi
chakachua ni kugeza, bali infi ni kuweza
hebu jaribu chakachua, halafu jaribu pia infi
chakachua sio infi, na infi si chakachua

Kamanda hapa napinga, kwa infii kutoa yote
kutoa yote ni kazi, yahusisha moyo wote
Kama hunayo hisia, huwezi toa yote kamanda.
 
Penzi la kuchakachua, ndilo lenye utamu,
Hutuchakachui kila siku, bali ni kwa hamu,
Mie nina uzoefu, wana JF mfahamu
Chakachua ni tamu, hasa akiwa binamu

Deodat karibu, ukaribie na kiti
unijuze kwa karibu, ngoja nibebe na kiti
Mzoefu na tabibu, utujuze kitikiti
Chakachua ya binamu, vipi ikawe ni tamu?


Hii haijaanza leo, bali tangu enzi za adamu,
Isipokuwa mambo yalifichwa, watoto wasifahamu,
Leo hii mambo hadharani, watu hawaogopi jehanamu
Chakachua ni tamu, hasa akiwa binamu

Hili nalo neno Deodat
 
Hongera MJ1 naona na wewe ni malenga mzuri sana Keep it up swirry
Aksante FirstLady nachangamsha akili hapa loh ..................Ila kusema kweli sikutegemea mpaka Acid na Asprin?? nimekubali JF ni kiboko.

Si ajabu tuna mpaka kina Masanja na Joti huku ndani... tuwape tu nafasi
 
hicho kipengele cha mwisho MJ1 nimekipenda sana...
Aksante nyamayao ..... mie nachanganyikiwa maana hata sioni tofauti ya Infidelity ya akina Baby yangu na Kamanda hapa na chakachua---- mpeka wanijuze
 
Babu yangu Sipirini, wote tuko lawamani
Hata si ya sirini, chakachua mapenzini
wote tuko kundini, si peke mke asilani
Kila wafanyacho wake, hujibu mapigo ya ngoma

Kama hakukuwa na wachakachuaji watu wasingechakachuliwa jamani babu au nakosea? Ni sawa na kuwaamuru mainfidelatees waache infedility wakati infidelators wapo! Bila Infidelators infidelatee atainfidelate na nani? Hapa nachokoza nyuki mamaa-naomba wasiione hii hawa memberz

Mjukuu mai dia, mimi siko lawamani,
Mila naizingatia, tangu enzi utotoni,
siwezi kuichenjia, nitakuwa matatani,
mwanaume kaumbiwa, kuishi na wake wengi.

Mwanaume kwa yakini, infi kwake asilia,
Acha mwanamke ndani, wa nje kuhudumia,
Kuweka sawa mizani, wanawake mezidia,
Mwanaume ameumbwa, kuishi na wake wengi.

Mwanamke kibishia, kisasi talipizia,
Hiyo ndio chakachua, mjukuu anasemea,
Infii haina nia, kuanzisha chakachua,
Mwanaeme kaumbiwa, kuishi na wake wengi!:welcome::welcome::welcome:
 
Sifaye binaaadamu, yeye si kama mnyama
amepewa ufahamu, ili siweze kukwama
akilize zi timamu, maisha kuyaandama
penzi kulichakachua, ni ujuzi wa kuwaza

mafuta wechakachua, ili kupata faida
mhudumu alijua, pesa singekuwa shida
mbaya kwake ilikuwa, sheria zikampiga
penzi kulichakachua, ni ujuzi wa kuwaza

inapokuja kwa penzi, mfumo ni ule ule
mkakati nguvu kazi, faida waweka mbele
kuchakachua si kazi, mafao yajaa tele
penzi kulichakachua, ni ujuzi wa kuwaza


(naomba ni eleweke kuwa sifagilii hii dhana ya uchakachuaji wa penzi, lakini i have to give to them, ni ubunifu wa hali ya juu) lol
 
haya, nimepita tu kuwasabahi!ntarudi mkiivisha chakula nikipendacho!
 
Acid

lazima Mwanajamii1 akubaliane na sheria za ubunifu 🙂
kweli kabisa... yani nnavyomuona... naona marinesheni imeshaanza kazi... katibu atakua keshampa kadi na katiba ya chama

MJ1 ananikumbusha mshairi bora --- AMIRI SUDI ANDANENGA [SAUTI YA KIZA]

i love JF
 
Back
Top Bottom