Usikurupuke kama hujaelewa uliza usiogope utaelimishwa.... Hebu niambie kwanini Mungu alimruhusu shetani amjaribu Ayubu.... Ukisoma kitabu cha Ayubu unaona kwamba shetani ana mawasiliano ya moja kwa moja na Mungu.. Na ni Mungu huyo huyo aliyempa shetani milki ya ulimwengu
Vipi ndugu maandiko huwa unasoma ana unasomewa? Je unaelewa? Nina mifano zaidi ya kumi kuthibitisha nilichoandika SIJAKURUPUKA
Bro kwanza asante kwa huko unakosema kusoma biblia,naomba Mungu akujalie sasa kuielewa maana hatua ya kwanza ya kuisoma yamkini umeiweza,
Skia nikuambie kitu mkuu,
Hiyo nukuu ya Ayoub haiongelei shetani kuwa na uungu,wala maana yake si kuonesha shetani ana uungu,ili kukusaidia kujua zaidi juu ya hili na maana yake tafuta vitabu rahisishi vya fafanuzi za biblia maana kuelewa we km ww inakutatiza,na si vibaya,
Halafu umeeleza jambo ambalo wala sikukataa,sikukataa mawasiliano ya Mungu na shetani,sijakataa juu ya nguvu zake,maana hata sasa wapo watu wana nguvu na hupata hata maono na mawasiliano na Mungu sasa nao unataka sema wana uungu?,
Kinachokusumbua unatumia maneno na ujuzi ule unaotumia kueleza mambo ya kidunia kueleza mambo ya MUNGU,
Lengo lako lilikuwa jema lakini namna na maneno ulotumia yamefanya iwe km unaongelea habari za ushirikina,
Narudia kusema shetani hana chembe chembe za UUNGU,nayasema haya kwa kuangalia asili yake,
Lkn km unataka tujadili kwa mapana kuhusu Shetani na Mungu sema,na leta vifungu toka BIBLIA tubadilishane elimu,
Nadhani ukae tu ujiulize kilichofanya useme shetani ana UUNGU,
Mi nadhani kurekebisha kauli haitakupunguzia sifa yako ya utaalamu,ujuzi nk mambo ambayo naona una hofu kuonekana hauna,
Hata wataalamu na wajuzi wanakosea pia
Shetani hana,hatakuwa na hajawahi kuwa na UUNGU,