Imeandikwa afichaye dhambi hatafanikiwa.Unaweza kutubu mwenyewe na ukiomba kwa nia utasamehewa, hakuna dhambi iliyo kubwa kuliko nyengine dhambi zote ni sawa
Hata biblia inaandika Baba yetu aonaye sirini atakujazi na kukulipa kadri ya mapenzi yake
Cha msingi ni kuomba kwa dhati kupitia kwa Kristo Yesu, Amen.
Unafanya KAZI ya Sauli, kuua na kupinga akina Petro ukiamini unamtetea Mungu kumbe unapotosha unamuudhi.Ndio inawezekana, kama akiinamisha kichwa chake, akatubu kwa kweli toka moyoni, Mungu huwa anaangalia moyo na anaweza kushuka na kumwokoa hata bila uwepo wa mtumishi. kwani Paulo alipokutana na Yesu na kupewa maelekezo aende kwa anania, alikuwa na mtumishi? si alikuwa ameshika upanga anaenda kukamata watu wa Mungu Damascus? kwani Yesu hakumwona. jua kuwa, hata ukiwa unatenda dhambi Mungu anakuona hadi moyo wako, ukiwa unaloga anakuona, ukiwa unauwa watu hata hao Hamas Mungu anawaona, ndio maana Mungu huwa anaweza kutuokoa toka mikononi mwa wabaya wetu kwasababu anatuona sisi na wabaya wetu pia, hivyo kwasababu anatuona hata ukipiga magoti na kutubu, anakuona na anaweza kukusikiliza.
kuendeleza kazi ya Mungu, shukran kwa Mungu, kumbariki mtu yeyote mwenye uhitaji, fungu la kumi,malimbuko, nakadhalika. umuhimu wake ni kuonyesha upendo wangu kwa Mungu, au kwa ndugu au kutii agizo la Mungu alilotuambia tutoe sadaka katika mazingira mbalimbali.Hebu niambie umuhimu/kazi sadaka unayoitoa wewe ukiondoa kwamba ni 'shukurani', umuhimu mwingine ni upi ?
Umetoa mfano mzuri sana, kwamba Yesu alimwambia Anania aende kwa Paulo ....... unadhani ni kwanini Yesu alimtuma tena Anania aende kwa Paulo wakati alishakutana nae njiani ?Ndio inawezekana, kama akiinamisha kichwa chake, akatubu kwa kweli toka moyoni, Mungu huwa anaangalia moyo na anaweza kushuka na kumwokoa hata bila uwepo wa mtumishi. kwani Paulo alipokutana na Yesu na kupewa maelekezo aende kwa anania, alikuwa na mtumishi? si alikuwa ameshika upanga anaenda kukamata watu wa Mungu Damascus? kwani Yesu hakumwona. jua kuwa, hata ukiwa unatenda dhambi Mungu anakuona hadi moyo wako, ukiwa unaloga anakuona, ukiwa unauwa watu hata hao Hamas Mungu anawaona, ndio maana Mungu huwa anaweza kutuokoa toka mikononi mwa wabaya wetu kwasababu anatuona sisi na wabaya wetu pia, hivyo kwasababu anatuona hata ukipiga magoti na kutubu, anakuona na anaweza kukusikiliza.
Tunasali Kanisa Gani??!!!hivi ninyi mnasali kanisa gani, mbona mnaficha kanisa lenu, au ni kanisa la uongo? tuambieni mnasali wapi tuwajue ili tujue kati yetu sisi na ninyi nani wa kusaidiwa kiroho. mpo nyuma sana kumjua Mungu na ninawaombea kwa Mungu awasaidie.
kinyume chake wewe ni ajenti wa shetani bila kujijua, na utahukumiwa kwa upotoshaji huu. unadhihaki sadaka ambayo Yesu Kristo aliitoa kwa machungu mengi, wewe unaona kama haikutosha?Unafanya KAZI ya Sauli, kuua na kupinga akina Petro ukiamini unamtetea Mungu kumbe unapotosha unamuudhi.
Mungu akusaidie.
hakuna aliyebisha kuombewa, tunachobisha hapa ni sadaka. hata mimi nilipookoka nilitubu kwa kuombewa, na ninawaombea watu kwa kuwawekea mikono wanapotubu waokoke au kuomba pamoja nao rehema kwa Mungu. lakini hawatakiwi kuja na sadaka. hoja hapa Ni SADAKA. sadaka sadaka.Umetoa mfano mzuri sana, kwamba Yesu alimwambia Anania aende kwa Paulo ....... unadhani ni kwanini Yesu alimtuma tena Anania aende kwa Paulo wakati alishakutana nae njiani ?
Swali zuri,Umetoa mfano mzuri sana, kwamba Yesu alimwambia Anania aende kwa Paulo ....... unadhani ni kwanini Yesu alimtuma tena Anania aende kwa Paulo wakati alishakutana nae njiani ?
basi inatosha, ninyi ni maajenti wa shetani. kwamwambieni shetani aliyewatuma mmekutana na watu wa Mungu huku wamejua njama zenu.Tunasali Kanisa Gani??!!!
1. Hekalu ni mwili wangu.
2. Madhabahu ni Moyo wangu.
3. KANISA ni Mimi mwenyewe.
Unataka tusali wapi?
Mungu anapenda Rehema kuliko sadaka.kuendeleza kazi ya Mungu, shukran kwa Mungu, kumbariki mtu yeyote mwenye uhitaji, fungu la kumi,malimbuko, nakadhalika. umuhimu wake ni kuonyesha upendo wangu kwa Mungu, au kwa ndugu au kutii agizo la Mungu alilotuambia tutoe sadaka katika mazingira mbalimbali.
hoja yetu sasa ni hii, unapoenda kutubu na umeshika sadaka, unashukuru nini tu? unashukuru kusamehewa hata kabla haujaomba msamaha? huoni kama unamhonga Mungu akusamehe? ninyi mnasali wapi? tuambieni hat akwenye DM tu.
Kwamfano kuvuta sigara ni dhambi au sio dhambi.Tatizo biblia imetaja uzinzi. Sasa uzinzi ufanyweje au kwa uchafu wa kiwango gani ni uzinzi.
Hakuna fungu la maandiko linaunga mkono unachofundisha. Mambo ya kiroho na imani lazima yawe na evidence angalau kwenye maandiko. Faith is evidence.
Ukristo wa kisasa unamapokeo mengi ambayo ni matokeo ya mawazo ya watu kwa mgongo wa mafunuo.
DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:Salaam shalom.
INTRODUCTON.
Imeandikwa, Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na haki, hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote.( 1 Yoh 1:9).
Dhambi ni kutotii, kwenda kinyume na maelekezo ya Mungu. Na Roho mtakatifu yupo kutukumbusha dhambi zetu Ili tuzitibie Ili tuendelee kuwa WATAKATIFU.
DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:
1. ZINAA NA UASHERATI.
UASHERATI ni kufanya Tendo la zinaa na mtu nje ya NDOA asiye mkeo au mumeo.
UZINZI ni kufanya tendo la uchafu, zinaa kabla ya Kuoa au Kuolewa.
Ukizini na mke wa mtu au mume wa Mtu, usijidanganye kuwa ukitubu sirini utasamehewa, HATIA itaendelea kuwepo Hadi uwatafute watumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi. Watumishi Wana BUSARA ya kusuluhisha dhambi hiyo pande zote mbili Ili ufunguliwe.
2. USHOGA.
Ikiwa uliwahi kuwa shoga, ukaamua kuacha, kamwe usitubu sirini na kuishiwa hapo, USHOGA huambatana na mapepo na kufungwa NAFSI, mfungwa kamwe hawezi jifunguanpingu mwenyewe, unawahutaji watumishi wa Kweli Ili UOMBEWE na kuwekwa huru, sadaka ni LAZIMA Ili itolewe huko.
3. USAGAJI.
Mwanamke pia aliyewa kufanya dhambi hiyo, huwezi kufunguliwa na Utumwa na HATIA hiyo pekeako Kwa kutubu sirini, nenda Kwa watumishi wa Kweli, Ukiwa na sadaka ya Ukombozi.
4. PUNYETO/ KUJICHUA.
Ikiwa uliwahi kujichua, ukaamua kuacha, unahitaji kwenda Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi Ili ufunguliwe, Mpiga PUNYETO ni mfungwa, ni mke au mume wa Roho chafu katika Ulimwengu wa Roho, hivyo kufunguliwa ni LAZIMA utoe sadaka, uvunje NDOA chafu hiyo ya kiroho na hati ya NDOA chafu ya kiroho iondolewe, usipofanya hivyo, unajidanganya. Mbinguni huingii ng'o!!
Neno Hilo hapo juu ni ROHO. Amen.
5.MWANAMKE KUOA MWANAMKE/MWANAUME KUOA MWANAUME MWENZIE.
Kutubu dhambi hii sirini bila watumishi wa Mungu ni kujidanganya. Chukua sadaka, nenda Kwa mtumishi, Sema Kweli Ili UOMBEWE na kufunguliwa, NDOA haramu ivunjwe na ufungwa wako kiroho uondolewe. Amen.
6. ORAL SEX.
Ikiwa uliwahi kushiriki oral sex, kunyonya au kuramba Kwa mdomo sehemu za Siri za mwanamke au Mwanaume na ukatambua ni DHAMBI, ukaacha, Bado u kifungoni.
Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli wa Mungu ufunguliwe na Mungu.
7. ABORTION./ UTOAJI MIMBA/ KUFUNGA UZAZI/ KUTUMIA VIDONGE VYA KUPANGA UZAZI.
Kimbia haraka Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli ,beba sadaka kulingana na uwezo wako, UOMBEWE ufunguliwe.
Ukipuuza Utakataliwa GETI la Mbinguni.
9. IKIWA ULIWAHI TUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME/ KIKE.
Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli UOMBEWE na kufunguliwa.
10. MAUAJI.
Ikiwa uliwahi kuua bila kukusudia ,ukahukumiwa JELA ukatoka, ikiwa uliua Kwa Siri na hukubainika, ikiwa ulishiriki kuua, usijidanganye kuwa unaweza kutubu sirini, HATIA Ili ikuondoke uwe na Amani, Tafuta kiongozi wa Mungu wa Kweli mwenye BUSARA za Mungu, akuongoze Cha kufanya, utoe pia sadaka ya Ukombozi.
11. IBADA ZA SANAMU, KUSHIRIKI IBADA ZA WAFU NA KUTOA SADAKA KWA MIZIMU KIMILA NK NK.
Kushiriki Ibada za KIMILA na Kutoa sadaka Kwa Roho za kishetani za Mababu, ni DHAMBI pia, ni kufungwa ni Utumwa ambao huwezi kujifungua pekeako.
Ukiamua kuacha na kuokoka, hatua inayofuata ni kushirikisha watumishi kukusaidia kukutenga na madhabahu hizo.
Sadaka ni LAZIMA, sababu, Ulimwengu wa Nuru na Giza sadaka ni inevitable. Amen
HITIMISHO.
Dhambi nilizotaja hapo juu, ni baadhi tu ya dhambi ambazo huwezi tubu pekeako, zimetajwa sawasawa na Ruhusa ya Roho mtakatifu Kwa mtumishi wake sawasawa na ufunuo wake apendavyo.
NB: Si DHAMBI zote zinahitaji kuona mtumishi wa Kweli kukusaidia kufunguliwa pingu za dhambi, ni baadhi ya dhambi ambazo Zina vifungo na attachment na maagano ya kipepo na kishetani.
Mungu awabariki.
Source: Nabii Justine Ibrahim.
Amen.
Upo sahihi kabisa, hapo kwenye kuvunja maagano ya giza kuna wakati tunahitaji watumishi wa Mungu watupe muongozo.Yesu alipokufa pale msalabani pazia la hekaru lilipasuka maana yake ametoa mpaka kati ya Mungu na mwanadamu hivyo tukiwa ba shida ikiwemo kutubu sio lazima kwenda kwa mchungaji sisi wenyewe anatusikia
Labda kuvunja maagano ya giza muda mwingine mtu peke yako huwezi! Inakubidi umuombe mchungaji msaada!
Rudi kusoma na uombe Mungu akusaidie kuelewa.basi inatosha, ninyi ni maajenti wa shetani. kwamwambieni shetani aliyewatuma mmekutana na watu wa Mungu huku wamejua njama zenu.
sasa umeelewa, ndicho nilichokuwa nasema.Mungu anapenda Rehema kuliko sadaka.
Mathayo 9:13
Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.
Na hatutoi sadaka ili tusamehewe dhambi, maana sadaka zetu haziwezi kufuta dhambi isipokuwa sadaka moja tu ambayo ni damu ya Yesu.
amri kutoka kifungu gani cha Biblia wewe kwamba twende kuomba rehema/msamaha kwa Mungu tukiwa na sadaka? unasema tuendapo nyumbani mwa Bwana tuwe na sadaka, nakubaliana na wewe, hoja tunayobishana hapa ni wakati ule wa kutubu, kwani kwenda kwa mtumishi wa Mungu utubu lazima iwe nyumbani mwa Bwana, huwezi kumfuata nyumbani kwake, kazini kwake au popote alipo uombe akuombee? manake hapo unaongelea kutoa sadaka kama kawaida uingiapo nyumbani mwa Bwana, hapo ndipo unapochanganya.Rudi kusoma na uombe Mungu akusaidie kuelewa.
Sadaka ni AMRI.
Ikiwa Mungu alimtoa mwanae wa pekee Yesu Kristo, sisi pia lazima tuendapo nyumbani mwa BWANA twende na sadaka,
Na sadaka hiyo Si mbadala wa Damu ya thamani ya Yesu,
Sadaka hiyo ni shukrani Kwa zawadi ya uhai na shukrani Kwa Yesu wetu.
Amen