Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

Nilichogundua, wengi wanaenda church na Bado wanazini,

Na wanaamini, unaweza kuzini, Kisha ukatubu pekeako chumbani ukasamehewa,

Dhambi hiyo shetani anewekeza sana maana anajua ukitenda ,Utaratibu wa kumalizana nayo ni ngumu,

Umeoa au Kuolewa Kwa Mfano, ukaanguka katika UZINZI na mke wa Jirani au na kahaba,

Lazima utubu Kwa mkeo kama umezini na kahaba,

Kama umezini na mke wa mtu lazima itafutwe namna ya kumalizana na mume wa mke uliyezini naye, na hapo, mtumishi wa Mungu anahutajika Ili kusaidia mchakato kuisha Kwa Amani.

Wengi wanachukulia pia dhambi ya UZINZI, inapeleka wengi kuzimu na WA eokoka na hawajui chanzo.
 
Umenena vyema,

Kutubu inahitajika mwongozo wa watumishi,

Nikuulize,

Umeoa, ikitokea umezini na mke wa Jirani Yako,

Unaamini ukitubu sirini, na huyo mzinzi mwenzio akitubu sirini bila mkeo kujua, na bila mume wa uliyezini naye,

Unaamini Mungu atasamehe?
 
Tupe mfano wa category ya pili
Category ya pili ni mtu aliyepanda viwango vikubwa vya utumishi,

Mtu amefikia Hadi level ya uchungaji, au Nabii, amejazwa na kuongozwa na Roho mtakatifu, anaisikia sauti ya Mungu live,

Halafu mtu huyo aamue Kwa hiari yake kwenda Kwa Waganga atumie uchawi madhabahuni kujipatia kipato.

Kingine ni hivi,

Unakuta mtu anahubiri barabarani, wewe hujui na hujathibitisha kuwa Nia ni anahubiri INJILI ametumwa na Mungu au la, wewe inakwenda pembeni na kuanza kumsema live kuwa ni mwongo,

Au unamsema live na kumtukana Yeye na KAZI afanyazo, hapo unajiweka katika nafasi ya kumkufuru Roho mtakatifu.

Kwa ufupi, mtu aliyejazwa Roho mtakatifu, amepanda viwango Hadi kufikia kunena Kwa lugha, ana karama ya unabii na ana macho ya Rohoni,

Mtu huyo kuasi huasi Kwa kudhamiria Si kudanganywa na shetani maana Kwa viwango hivyo, mitego yote ya shetani Huwa unaiona hata kabla haijakufikia, na unakuwa unajua namna ya kuepuka.
 
Watumishi wa Mungu waadilifu wamebaki wachache siku hizi.
Wengi wanakwenda kimwili..hii inaondoa kuaminiwa na jamii.
Hili nalo hulioni?
Na Mtumishi naye akitenda dhambi,akatubie kwa nani?
Je,Biblia imeweka utaratibu gani katika Toba?
Kuasi Kwa watumishi, hakukupi fursa ya kutengeza Utaratibu wako,

Mwombe Roho mtakatifu akuonyeshe watumishi sahihi wankukusaidia. Wapo Bado wenye unyofu wa moyo.
 
Wamagharibi/uarabuni waliharibu sn ubongo wamwafrika kwa dini hii kitu kupona itachukua muda sn and possible isiwepo kabisa
 
....Nikuulize,

Umeoa, ikitokea umezini na mke wa Jirani Yako,

Unaamini ukitubu sirini, na huyo mzinzi mwenzio akitubu sirini bila mkeo kujua, na bila mume wa uliyezini naye,

Unaamini Mungu atasamehe?
Baada ya toba unafanya kitu kinaitwa jambo la kijamii ambalo linaitwa Malipizi ya ndoa. Hili siyo toba bali marekebisho baada ya kutengeneza na Mungu kwanza.
 
Baada ya toba unafanya kitu kinaitwa jambo la kijamii ambalo linaitwa Malipizi ya ndoa. Hili siyo toba bali marekebisho baada ya kutengeneza na Mungu kwanza.
Fafanua,

Hilo jambo la Kijamii linaloitwa malipizi ya NDOA ni lipi?

Una HAKIKA, BIBLIA kama Katiba, haijatoa mwongozo juu ya nini kifanyike baada ya mtu kuzini au kufanya uasherati nje ya NDOA takatifu?
 
Toba pekee ni ile unayouelekeza moyo wako kwa Mungu kuomba rehema zake.

Hiko ulichokitolea mfano ni matengenezo na siyo toba. Na hufanyika baada ya toba
 
Toba pekee ni ile unayouelekeza moyo wako kwa Mungu kuomba rehema zake.

Hiko ulichokitolea mfano ni matengenezo na siyo toba. Na hufanyika baada ya toba
Una andiko linaloshabiiana na usemacho kuwa hii ni TOBA na hii ni matengenezo?

Huoni wote wanaopinga wanaopinga hata huo Utaratibu unaouita matengenezo, sababu Yao kuu ni kuwa hata watumishi wanatenda dhambi kama hizo?

Nilichoandika ni Kweli tupu,

Kubalini UKWELI muwe huru.
 
Toba pekee ni ile unayouelekeza moyo wako kwa Mungu kuomba rehema zake.

Hiko ulichokitolea mfano ni matengenezo na siyo toba. Na hufanyika baada ya toba
Soma

(Mathayo 5:25)

Imetoa Utaratibu wazi, kabla ya kwenda kuomba msamaha Kwa Mungu, malizana na uliyemkosea kwanza,

Hata sadaka madhabahuni hupasi Kutoa ikiwa una tatizo na mtu hujamalizana nae.

Wengi mnalaaniwa sababu unakuta umezini Kwa Mfano, hujamalizana msamaha na mkeo, na mume wa uliyezini naye, unatubu kimya kimya Kisha inapeleka sadaka madhabahuni, sadaka hiyo hugeuka na kulaani KAZI zako ndomana hamfanikiwi katika KAZI mfanyazo na hamjui sababu ni nini!!

Mbinguni Si rahisi kama m avyodhani.
 
Fahamu hao wanakuwa hawajabadilishwa bado ni watoto wachanga kiroho,ndiyo
Mi misingi ya kutubia kazi zisizo na uh na uhai,Waebrania5:12-14)
Hii dhambi inaangusha sana watoto wengi wa Mungu! Mpaka baadhi ya Watumishi wa Mungu.
 
Mtumishi wa Mungu Kwa Mfano, azini na mke wa muumini,

Hivi atalimalizaje hili na kupata ujasiri wa kuendelea kusimama madhabahuni?

Njia ya Mbinguni ni nyembamba sana, halafu watu wananitukana kana kwamba niliyoandika nimetoa kichwani mwangu, wakati yote niliyoandika ni biblical.
 
Hukumu yake haiishi! Kwa Mtumishi wa Mungu,huko ndiyo kumkufuru Roho Mtakatifu! Ni gharama kuitubu.
 
Sahihi. Ni mtazamo wa mtu tu.
 
Hukumu yake haiishi! Kwa Mtumishi wa Mungu,huko ndiyo kumkufuru Roho Mtakatifu! Ni gharama kuitubu.
Hasa ndiyo dhambi ya kumkufuru Roho mtakatifu!!

Mungu atusaidie.
 
Kuwasaidia wanaojihusisha na hayo mambo ili iwe rahisi kuwatongoza.... Ni hayo tu kwa Sasa. Mungu hahitaji dalali ili akuondolee dhambi !!
 
Kuwasaidia wanaojihusisha na hayo mambo ili iwe rahisi kuwatongoza.... Ni hayo tu kwa Sasa. Mungu hahitaji dalali ili akuondolee dhambi !!
Ukizini na mke wa mtu unaingia chumbani, unapiga magoti na kutubu Kwa Mungu, Badala ya kutubu Kwa uliyemwibia mke?

Yaani uibe mke wa Juma, Badala ya kutubu Kwa juma, unatubu Kwa Mungu?

WANADAMU mna mapuuza!!
 
Kuasi Kwa watumishi, hakukupi fursa ya kutengeza Utaratibu wako,

Mwombe Roho mtakatifu akuonyeshe watumishi sahihi wankukusaidia. Wapo Bado wenye unyofu wa moyo.
Jibu na swali la pili,
Mtumishi akitenda dhambi naye aongozwe na nani kutubu?
Leta maandiko yenye utaratibu huo wa toba unaousema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…