Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

Hakuna bunadamu ambaye ni mtumishi wa Mungu; binadamu wote ni waja wake kwa haki sawa.
 
Kuna jamaa aliiba spika za kanisani siku alipoenda kutubu wakamuitia polisi
 
Jibu na swali la pili,
Mtumishi akitenda dhambi naye aongozwe na nani kutubu?
Leta maandiko yenye utaratibu huo wa toba unaousema.
Soma (Kutoka 22:16, )
Mtu akimshawishi bikra ambaye hajaposwa Bado na akambikiri, atatoa Mahari Kisha atamwoa Binti huyo,

Likewise, mtu akizini na mke wa mtu, yampasa kulipa Mahari ambayo mume alimtolea mke na hiyo ndiyo adhabu yake, Kisha atasamehewa dhambi hiyo.

(Mathayo 5:25)

Patana na mshitaki wako mkiwa njiani kabla hajakufikisha Kwa kadhi, kadhi akakupeleka Kwa liwali ukatupwa GEREZANI,

Ukizini na mke wa mtu, unatakiwa kupatama na mshitaki wako ambaye ni mume wa uliyezini naye.

Ukizini na kahaba, mshitaki wako ni mkeo, mkiyamaliza ndipo unaenda kutubu Kwa Mungu.

Siku hizi vijana hamfundishwi adabu na wakubwa, mnajiendea tu!!

Umeelewa?
 
Sawa bwana mkubwa
 
Wachungaji wenyewe wambea usiku tu kashamtangazia mama Mchungaji ..... Jumapili unaona unaangaliwa kichini chini kumbe mama Mchungaji kashatangaza Kwa Fulani .... Fulani kwa Fulani .... Me na Mungu nitubu sirini na Mungu aone nimedhamiria kwl imeisha hiyo.
 

Hiyo ni imani ya kiyahudi au ukristo? Kama Yesu ni kuhani mkuu kwanini niende kwa mtumishi mwingine?

Ingekua dhambi zetu zinamzuia kutusamehe asingekubali kufa msalabani.

Kwani watumishi hawatendi dhambi?, kama wanatenda kwanini niende kwao nikawaambie nimezini? usikute na yeye katoka kuzini mda huo!!
 
Mtumishi umeanzia mbali sana. Ungesema tu tulete sadaka
 
1&5 wamejaaaa humuu ndani waanze kuombewa wajitaje kwanza
 
Kiboko ya wachawi arudi kutujibu haya
 
 
Hapo unatubu kwa Mungu au kwa mchungaji?
Mtu aliyekuwa baba wa mtoto ambaye sasa ni yatima,

Akitaka kutubu, kipi sahihi,

1. Kutubu kimya kimya sirini.

2. Kumtafuta mtoto wa mzazi aliyekuwa Kisha kutafuta Amani naye Kwa msaada wa Mtumishi wa Mungu,Kisha ndipo uombe msamaha Kwa Mungu?
 
Mtumishi umeanzia mbali sana. Ungesema tu tulete sadaka
Sadaka ya mbwa HAIPOKELEWI.

Sadaka ya damu HAIPOKELEWI,

NB: Usipotoa sadaka ,unaweza kufanyika sadaka ya kuteketezwa mfano mzuri ni Isaka mwana wa Ibrahimu.

Sina haja na sadaka Yako ndio maana hata PM Iko blocked, nimedirect utafute mtumishi wa Mungu karibu Yako asaidie.
 
Ok, basi nenda PEKEAKO Kwa mume wa mke uliyezini naye bila kumtumia mtumishi wa Mungu uone kama utarudi na shingo Yako ikiwa kichwani mwako!
 
Nimesema Mtumishi wa Mungu wa Kweli. Si mtumishi yeyote.

Msisitizo uko hapo.
 
Watumishi wenyewe akina Lusekelo na wale wengine waliopokea mgao wa ESCROW au watumishi gani
 
Watumishi wenyewe akina Lusekelo na wale wengine waliopokea mgao wa ESCROW au watumishi gani
Tafuta watumishi wa Mungu wa Kweli,

Achana na matapeli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…