Dhambi ya kikokotoo cha wastaafu ni mbaya kuliko dhambi ya mauti

Inaumiza Sana
 
Hali ya mifuko kuwa mbaya sio tatizo kutoka kwa Mungu, ni watu waliolisababisha. Adhabu ya hilo haiwezi kulipwa na wastaafu waliotimiza wajibu wao kwa mifuko.
 
Wabunge wangeondolewa posho za vikao, kwa kuwa pale wawapo bungeni ndiyo huwa wanafanya kazi zao za msingi. Ulipwaji wa posho hii ndiyo sababu kubwa ambayo inapelekea kupatikana kwa wabunge wengi ambao hawana uwezo wa kuishauri, kuisimamia, na hata kuiwajibisha serikali.

Endapo kazi hii ingalikuwa na malupulupu ya kawaida, basi wengi wao wala wasingehangaika kupindisha taratibu, kuiba kura, kuhonga pesa nyingi, ku "lobby" au kufanya ushirikina ili kuipata.
Na pia ingekuwa fursa nzuri kwa watu wa kawaida na wenye sifa sahihi na uwezo kujitokeza ili kuigombea.

Mathalani kama wabunge wangeingia katika stahiki za mafao kama vile ilivyo kwa wafanyakazi wengine, sidhani kama wangalifanya mzaha katika suala la kikotoo. Ndiyo! Hiyo ni "agency problem"

It is agency problem because there is a conflict of interest inherent in any relationship where one party is expected to act in another's best interests.
Samahani kwa kuchapia lugha ya malkia, kwa kuwa sikutaka kupoteza maana ya msingi iliyopo nyuma ya tatizo hili la uwakala kama mgogoro wa maslahi.

Ni kweli kuna mgongano wa maslahi kati ya malupulupu ya wabunge yale ya watu wengine wanao wawakilisha. Linapokuja suala la suala la stahiki zao, basi hujitenga kabisa na za watu wengine, na wala hawataki kabisa wafanane na wale wanao wawakilisha.
 
Ukifa yanakoma mara moja
Serikali inayokula hela za marehemu imekosa radhi kwa Mwenyezimungu. Sababu wanazotoa kuhalalisha kikokotoo hazitokani na matakwa na maombi ya wastaafu wenyewe. Yaaani kosa la mtumishi ni kukubali kuwekewa fedha yake na wezi.
 
Hii ni njia ya sirikali kukwepa kuwalipa hela zao kwa kusaidiwa na kifo Chao[emoji3578]
 
Hii ni njia ya sirikali kukwepa kuwalipa hela zao kwa kusaidiwa na kifo Chao[emoji3578]
Hii ni dhambi kubwa kubaki na deni la mtu aliyekufa. Kwenye madodoso yako muhimu umeandika umri wa kuishi ni miaka 55 lakini mtumishi mwenye miaka 60 hutaki kumpa hela zake zote, hizo takwimu ni fake basi, not realistic,, mizi mtupu kuanzia ukusanyaji wa takwimu hadi kikokotoo.
 
nipo mbele mbele hapa yaani mm binafsi naona hili suala la kikokotoo ni wizi unaoishi.
 
Mchawi wa watumishi wa Tanzania hasa walimu wetu ni Cwt ambao waliiomba serikali siku ya sherehe za mei mosi zilizofanyika Mwembetogwa Iringa kwamba serikali ipunguze mafao ya mkupuo kutoka asilimia 50 hadi 25 ili mtumishi apate package kubwa ya hela ya mwezi huku bado akiwa amepanga nyumba au yuko nyumba ya makuti.Hakika vyama vya wafanyakazi Tanzania ni majanga .Sijui wanapata nini hao walimu wetu waliowachangia mamilioni kama ada ya uanachama wakiishi maisha mabovu?
 
Wakati mbunge anachukua million 270 akikosa ubunge kama kiinua mgongo na hyo ni baada ya miaka mitano tu halafu kwenye majukwaa wanahubiri uzalendo.
 
Linaonekana kana jambo la 'Ubunifu Uchwara'

Hata hivyo, serikali inapaswa kupunguza gharama, wanapaswa kujaribu njia kama hiyo, ikiwa wameshindwa kubuni na kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato. Wafunge mikanda.
Pesa za wastaafu si ndio zile watu wamepiga kwenye miradi hewa mifuko yote inapumulia mashine watu wamepiga hela.
 
Aliyeanzisha kikokotoo ni nani kwani
 
Kingetumika kwa Wabunge ndio wangewatetea wastaafu.
 
Narudia kuwausia wajukuu zangu
Hizi lawama, vilio na ngendembwe zitakoma pale mtakapoiweka CCM pembeni
 
Kwanza ututake radhi wakulima, wafugaji, wavuvi, wakwezi na wawindaji. Nasi tunastahili kuishi vizuri kama wazee wengine wowote walioitumikia nchi hii. Sisi kwa kuwa wakulima, wafugaji, wavuvi, wakwezi au wawindaji tunastahili sehemu ya keki ya nchi hii.
Mengine yote nakubaliana nawe.
1. Mifuko hii ni ya ajabu sana. Mfanyakazi katika mifuko hii ana kipato kizuri kuliko mchangiaji wa mfuko husika.

2. Mifuko hii imefanya uwekezaji wa hovyo sehemu nyingi. Mfano, PSSSF imejenga lijumba kubwaa (Ghorofa karibuni 32) Barabara ya Sam Nujoma, mkono wa kushoto ukitokea Mwenge kwenda Ubungo. Halafu haina mpangaji ukiondoa NHIF na wengine wachache sana. Kibali hicho cha uwekezaji wanatoa wapi bila kuwa na wataalamu wa kiuchumi?
 
Adui mkuu wa wastaafu ni CCM!
Angalia mafao ya wakubwa kama wabunge na mawaziri hawatumii kikokotoo hiki!
CCm wewe ni adui mkuu wa wananchi wako. shame on you
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…