Dhambi ya Zinaa, Ngono, Uzinzi na Uasherati

Uzinzi ni kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa, mtu ameoa/ameolewa akichepuka anafanya uzinzi.
Uasherati ni kufanya tendo la ndoa kabla ya kuingia kwenye ndoa.

Ninachoona, hakuna atakayebaki. Wote tumekwisha, japo Mungu nae atakuwa na mengi ya kutujibu hiyo siku.
 
Ni kawaida ya mwanadamu kutaka uhuru uliopitiliza.
Mathayo 5:28 Yesu alisema
" Lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake." Je kwa kumtazama na kumtamani mwanamke ni wapi unakuwa umeumiza hisia zake? Kuwa makini ndugu!
 
Tafsiri yako ipo kinyume
 
Watu wanampangia MUNGU namna ya kutafsiri dhambi na kutoa hukumu kwa maslahi binafsi.
Hakuna anayejua tafsiri halisi ya hukumu itakavyotolewa. Tenda mema na ishi kwa amani bila woga. Usitishike na matishio ya kilokole.
 
Sasa niambie katika amri 10 za Musa, ipi katika hizo ni kuvunja amri!?!

Mtoto ana balehe anaota wet dreams katenda dhambi!?

Beberu walituweza Sana kutujia na hizi dini, kila kitu dhambi. Ukiota dhambi!?
 
Wewe haya yote nani kakwambia kama siyo wazungu ambao kwa sasa hata wao hawaamini haya
 
Hii sadaka ya hatia imeandikwa kwenye kitabu Gani?

Kutumia njia za kuzuia mimba napo inaita dhambi, umerejea maandiko yapi?

Kutubu ni lazima uende mbele za watu?

Hapo kwenye ndoto nakubaliana na wewe kukemea, kuomba zisitokee lakini hauwezi kunishawishi ni dhambi Kwa kitu ambacho sio hiari Yako.
 
Najitahidi kuwa makini hapa. Kuna kupitiwa, kuna kukosea na kuna kufanya dhambi.

Halafu kama kitu hakimake sense huwa ninakuwa na walakini nacho automatically. Mi ntasema jamaa kapitiwa tu hapo. Simaanishi kuwa kupitiwapitiwa ni kuzuri lakini bado bhana, bado haijawa dhambi kwake. Ngoja tuone atakachokifanya next ndo tujue ni dhambi au la.....
.....
.....
Ona kageuka tu, kaangalia kalio, katikisa kichwa kuonesha kakubali, halafu kawasha bodaboda yake katembea😂😂.

Dhambi iko wapi hapo, japo sio vizuri angeweza kupata ajali huyu mwamba siku nyingine awe makini barabarani. So kwenye kupitiwa sawa amefanya, kwenye kosa sawa amefanya ila dhambi mmmh hapo bado bado kuna ukakasi

Kuhusu aliyowaza kichwani hatujui je;
A. Amewaza huyu mtoto nimvizie kichochoroni nimbake?
B. Huyu mtoto nimtafute kwao wapi nikatoe posa?
C. Hajawaza chochote zaidi. Hatujui
 
Namba 4 hujaielezea vizuri

Talaka haijawah kuwa mpango wa mbingu hilo ni lazima ujue,,
Talaka hutolewa kama mmoja wa wanandoa amecheat na huyo aliyecheat hatakiwi kuoa au kuolewa mathew 5:30-32
 
Sasa niambie katika amri 10 za Musa, ipi katika hizo ni kuvunja amri!?!

Mtoto ana balehe anaota wet dreams katenda dhambi!?

Beberu walituweza Sana kutujia na hizi dini, kila kitu dhambi. Ukiota dhambi!?
Ukiwauliza wanasayansi watakuambia "wet dreams"ni tendo la kibalojia. Lakini kiroho wet dreams ni matokeo ya jini mahaba ambae huja katika ndoto km msichana mrembo na kufanya tendo na kijana. Lengo ni kumchafua na kuvuna mbegu zinazohitajika katika ulimwengu wa kipepo kwa matumizi mbali mbali. Km kuna mganga au mchawi hapa atanielewa.

Mbegu za kiume ni bidhaa muhimu sana kwa majini hasa kwa vijana ambao hawajachafuliwa na wamebalehe punde.
 
We mpuuzi kweli eti wet dreams,, unaropoka tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…