Dhambi ya Zinaa, Ngono, Uzinzi na Uasherati

Tumehubiriwa sana kuhusu dhambi ya zinaa,ngono uzinzi,na uasherati.Wachungaji wengi hawafundishi kwa kina dhambi hii kwa sababu wao wenyewe inawagusa. Matokeo yake Wakristo hupata ufahamu mdogo na wa juu juu na kujiona wako salama na kumbe wamepotea km watu wa mataifa. Ndio maana kuna msemo " Garbage in garbage out". Injili ikihubiriwa vizuri bila kupindisha au kuficha ficha wengi hatuko salama.

Dhambi ya zinaa ni dhambi iliyofunga na kuwapoteza watu wengi bila kujali umri,cheo au jinsi.Shetani ameificha dhambi hii kwa kuifanyia "camouflage", kwa namna mbali mbali mfano kutoa tafisiri za uongo na kufanya kampeni za kuhalalisha ngono na kuonekana ni kitu cha kawaida watu kufanya bila utaratibu.

Yafuatayo ni matendo( dhambi za kingono)ambazo km ulifanya/unafanya ukifa bila kutubu adhabu yake ni jehanamu kwenye chumba cha uzinzi,uasherati na ngono.

1.Kufanya ngono kabla ya ndoa.Hata km mlikuja kuoana baadae km hamjatubu dhambi mliyoifanya adhabu yenu ipo pale pale na mtahukumiwa wote 2 baada ya kifo. Mpango wa Mungu si watu kufanya tendo kabla ya ndoa.Hivyo mnapofunga ndoa baadae, je mlitubu kosa lenu mbele ya mtumishi wa Mungu na kutoa sadaka ya hatia?

2.Kufanya ngono nje ya ndoa. Kwasasa hili nalo ni janga.

3.Kuzaa kabla ya ndoa. Hata km mlikuja kuoana baadae km hamkutubu kupitia maombi ya utakaso, dhambi hiyo ipo pale pale.Ndoa yenu haihalalishi zinaa mliyoifanya hapo kabla.

4.Kuoa au kuolewa ukaachika/ kuacha na kuoa/ kuolewa tena.

5.Kuwa na wapenzi/wake wengi.

6. Kufanya mapenzi katika ndoto. Watu wengi wameweza kuishinda zinaa ya mwili ya kawaida. Lakini Shetani amewafata na kuzini nao katika ndoto na hata kufunga ndoa za kijini na jini mahaba. Kiroho hii ni zinaa km zinaa zingine. Tuwe macho hasa kufanya maombi kabla ya kulala.

7.Kumtamani mwanamke kwa kumtazama
8.Kuwaza waza kufanya ngono( Kuwaka tamaa ovyo)

9.Kuongea maneno ya kushabikia ngono.Matendo 4:23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima".

10.Kujichua (Masterbation)
11.Mapenzi ya jinsia moja. Walawi 20:10-21
12.Kufanya mapenzi kinyume na maumbile hata km ni kwa mkeo. Walawi 20:10-21
13.Kufanya mapenzi na mnyama. Walawi 20:15-16
14.Kufanya ngono na ndugu yako. Walawi 20:17-21

15.Kuangalia picha za ngono.Hata km umeacha je umetubu? Lazima ufanye maombi ya toba yaliyoambatana na sadaka ya hatia.

16.Wanaotumia kondom hata km wameoana bado ni dhambi.

17.Kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo.
18.Kuchezea utupu wako au wa mtu mwingine kwa vidole. Ni chukizo mbele za Mungu.

19.Wanaotumia vidonge au vijiti vya kuzuia mimba
20. Kutoa mimba.

Nb. Kila tendo tunalolifanya linarekodiwa katika ulimwengu wa roho( Kuzimu na mbinguni). Ukifa kuzimu wanatoa hesabu ya matendo yako. Km ulifanya dhambi na ukatubu rekodi ya mbinguni itaonyesha na utawekwa huru na kwenda kwenye umilele wa mbinguni. Kinyume chake ni kwenda kwenye umilele wa Jehanamu.

Km umefanya zambi hizo au moja ya dhambi hizo inabidi utubu na kufanya maombi ya kukombolewa ukiambatanisha na sadaka ya hatia.

Neno la Mungu linasema:-
"Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako".Matendo 8:22.

Mungu awabariki na atusamehe makosa yetu. Nawatakia Jumapili njema yenye baraka tele.
Hayo ni kwa mujibu wa IMANI ya Kikristo
 
Kabsa yaan anasahau kuwa chanzo kingn ukiachana na tamaa cha wanandoa kusalitian na kuchepuka nikuwa huwa hawaridhishwi nawenza.mfn mwanamke kutofrahia tendo kiujumla.akijaribu kwa wengne tyr anasalit maan anakutana navitu hajawah fanyia ikiwepo kuandaliwa vzur kabla ya tendo, kuandaliwa kwnyewe ndo jamaa anadai ni dhambi.sohata waliooa wanadhambi kumbe.#Makubwa#
Hajui matatizo mengi kwenye ndoa siyo fedha na magari ni SEXUAL FRUSTRATIONS!
Hili ndilo analopaswa kuhubiri, namna gani bora wenza wanaweza kuridhishana kitandani mpaka zinaa sijui uasherati isiwe dhambi!

Hawa ni wale wanaotembea na Spika njoo Kwa Yesu kuna uzima kisha anaomba sadaka papo kwa papo apate hela ya Kula. Kasahau kwa Yesu kuna uzima!
 
Sometimes hawa wahubiri wana exaggerate mambo..
Kuna mmoja aliwahi kusema hata kunywa kahawa, chai, soda.. ni dhambi. Sasa unajiuliza, enzi za maandiko hivyo vinywaji havikuwepo, na havikuandikwa, na havileweshi, amejuaje kama vina dhambi?!!!
 
Tumehubiriwa sana kuhusu dhambi ya zinaa,ngono uzinzi,na uasherati.Wachungaji wengi hawafundishi kwa kina dhambi hii kwa sababu wao wenyewe inawagusa. Matokeo yake Wakristo hupata ufahamu mdogo na wa juu juu na kujiona wako salama na kumbe wamepotea km watu wa mataifa. Ndio maana kuna msemo " Garbage in garbage out". Injili ikihubiriwa vizuri bila kupindisha au kuficha ficha wengi hatuko salama.

Dhambi ya zinaa ni dhambi iliyofunga na kuwapoteza watu wengi bila kujali umri,cheo au jinsi.Shetani ameificha dhambi hii kwa kuifanyia "camouflage", kwa namna mbali mbali mfano kutoa tafisiri za uongo na kufanya kampeni za kuhalalisha ngono na kuonekana ni kitu cha kawaida watu kufanya bila utaratibu.

Yafuatayo ni matendo( dhambi za kingono)ambazo km ulifanya/unafanya ukifa bila kutubu adhabu yake ni jehanamu kwenye chumba cha uzinzi,uasherati na ngono.

1.Kufanya ngono kabla ya ndoa.Hata km mlikuja kuoana baadae km hamjatubu dhambi mliyoifanya adhabu yenu ipo pale pale na mtahukumiwa wote 2 baada ya kifo. Mpango wa Mungu si watu kufanya tendo kabla ya ndoa.Hivyo mnapofunga ndoa baadae, je mlitubu kosa lenu mbele ya mtumishi wa Mungu na kutoa sadaka ya hatia?

2.Kufanya ngono nje ya ndoa. Kwasasa hili nalo ni janga.

3.Kuzaa kabla ya ndoa. Hata km mlikuja kuoana baadae km hamkutubu kupitia maombi ya utakaso, dhambi hiyo ipo pale pale.Ndoa yenu haihalalishi zinaa mliyoifanya hapo kabla.

4.Kuoa au kuolewa ukaachika/ kuacha na kuoa/ kuolewa tena.

5.Kuwa na wapenzi/wake wengi.

6. Kufanya mapenzi katika ndoto. Watu wengi wameweza kuishinda zinaa ya mwili ya kawaida. Lakini Shetani amewafata na kuzini nao katika ndoto na hata kufunga ndoa za kijini na jini mahaba. Kiroho hii ni zinaa km zinaa zingine. Tuwe macho hasa kufanya maombi kabla ya kulala.

7.Kumtamani mwanamke kwa kumtazama
8.Kuwaza waza kufanya ngono( Kuwaka tamaa ovyo)

9.Kuongea maneno ya kushabikia ngono.Matendo 4:23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima".

10.Kujichua (Masterbation)
11.Mapenzi ya jinsia moja. Walawi 20:10-21
12.Kufanya mapenzi kinyume na maumbile hata km ni kwa mkeo. Walawi 20:10-21
13.Kufanya mapenzi na mnyama. Walawi 20:15-16
14.Kufanya ngono na ndugu yako. Walawi 20:17-21

15.Kuangalia picha za ngono.Hata km umeacha je umetubu? Lazima ufanye maombi ya toba yaliyoambatana na sadaka ya hatia.

16.Wanaotumia kondom hata km wameoana bado ni dhambi.

17.Kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo.
18.Kuchezea utupu wako au wa mtu mwingine kwa vidole. Ni chukizo mbele za Mungu.

19.Wanaotumia vidonge au vijiti vya kuzuia mimba
20. Kutoa mimba.

Nb. Kila tendo tunalolifanya linarekodiwa katika ulimwengu wa roho( Kuzimu na mbinguni). Ukifa kuzimu wanatoa hesabu ya matendo yako. Km ulifanya dhambi na ukatubu rekodi ya mbinguni itaonyesha na utawekwa huru na kwenda kwenye umilele wa mbinguni. Kinyume chake ni kwenda kwenye umilele wa Jehanamu.

Km umefanya zambi hizo au moja ya dhambi hizo inabidi utubu na kufanya maombi ya kukombolewa ukiambatanisha na sadaka ya hatia.

Neno la Mungu linasema:-
"Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako".Matendo 8:22.

Mungu awabariki na atusamehe makosa yetu. Nawatakia Jumapili njema yenye baraka tele.
Wewe mwenyewe huchomoi hapa, kwa kuwa umewaza ukaandika.
 
1Yohana1:9-10 inasema:-
9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
10 Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.
 
Mmmhhh. Kwan lazima kuambatana na sadaka ya Toba. Na sadaka ya Toba ni Nini? Ebu fafanua kidogo hapo.

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Kuna dhambi nyingi tunafanya, watu tunachukulia poa. Sio Wakristo wala Waislamu na Wapagani wanazini mno. Mungu aturehemu na kutupa nguvu ya kuachana na dhambi.
 
Mmmhhh. Kwan lazima kuambatana na sadaka ya Toba. Na sadaka ya Toba ni Nini? Ebu fafanua kidogo hapo.

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
Sadaka ya toba na sadaka ya hatia hakuna tofauti kubwa sana. Tofauti ni aina ya tendo ulilotenda. Mfano unapotembea na mke wa mtu au kuiba mali ya mtu, hayo ni matendo ya hatia na utatakiwa utoe sadaka ya hatia.Soma Walawi19: 21.

Dhambi tunazozifanya kwa kutojua mfano mawazo mabaya,hasira,kijicho,kulaumu n.k tunakiwa kuambatisha sadaka ya toba ili tusamehewe. Pia kuna sadaka ya kukombolewa. Hii ni sadaka ya kumuomba Mungu kufungua vifungo vya kiroho km utasa,kuolewa,kukataliwa na mabalaa mengine.
 
3044120_16FF8E59-2C1F-46CB-8A7D-E4D34E6651E7.jpeg
 
Ngoja nikuambie kitu hakuna sehemu ambayo watu tunaharibiwa km kupitia ndoto.
Kupitia ndoto watu wanafanywa kuwa tasa,kufungwa kuolewa au kuoa,kuibwa nyota na kunajisiwa. Shetani anajua Biblia zaidi ya mimi na na wewe na anafahamu wapi pa kutukamata. Kwanini ndoto chafu za usku ni dhambi. Biblia inasema

Yoshua 1:8
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

Mtu anaechezewa na mapepo au wachawi usiku, Biblia haipo kichwani mwake. Na mtu asiyesoma Biblia hana roho mtakatifu maana ni kwa kusoma na kufakari neno la Mungu na kuliishi ndo tutamwita Roho Mtakatifu. Pasipo na roho mtk basi pana roho mchafu. Na ukishakuwa na roho mchafu wewe ni mdhambi with "no excuse".

Aaah wapi! Ni wapi imeandikwa ndoto inaelekea dhambi? Hiyo mistari umeweka inaelekea umuhimu wa kushuka na kuliweka neno la Mungu moyoni. Elezea hapa ndoto inavyokuwa dhambi, kumbuka ndoto sio kitu Cha hiari.
 
Jamaa kaokoka juzi ana amsha amsha!
Anataka kuokoa nyoyo za JF,
Wala tunda kimasihara wameonekana wapo wengi humu!
Na ana moto hatari! hadi wakristu wenzake tunashtuka! 'Nini hicho kilichotupiga kwa ghafla!? Jamaa kaja ghafla sana daah!😂😂.

Wazungu nao wanasemaga 'whaat hit me!!?
 
Na mtu asiyesoma Biblia hana roho mtakatifu maana ni kwa kusoma na kufakari neno la Mungu na kuliishi ndo tutamwita Roho Mtakatifu. Pasipo na roho mtk basi pana roho mchafu
Mtu yeyote anayetenda mema ako na roho wa Mungu, haijalishi alishawahi kuiona wala kiushika biblia au hata hajawahi kuiwazia. Mtu anaweza kumjua Mungu kupitia vyanzo vyake vingine saafi kabisa.

Moja kati ya mkanganyiko wa kimantiki walioupata mafarisayo ni pale waliposema ati 'Yesu anatoa pepo na kuponya kwa nguvu za kishetani' Wakati inayakinika kwamba mema hutoka kwa Mungu. Kwa nini ilibidi waseme hivyo? Ni kwa sababu alifanya baadhi ya vitu ambavyo wao waliona sio vyema mfano kuponya siku ya sabato.

Lakini ndugu nikwambie popote penye logical contradiction ujue tu sikuzote ni kwa sababu kuna kimoja ni kweli kingine kimepotoshwa. Japo maandishi yao yalisema usifanye kazi siku ya sabato iliwabidi watumie akili kujua kuwa kuna kitu hakiko sawa lazima. Huu ni wito kwako kuhusisha akili penye utata wowote.
 
Barikiwa mtumishi ila hisi pisi kali mbn zinakuwa nyingi Sana tunawafadisha Sasa ningekuwa muslamu ningeoa wanna yaani mnk Ni wengi Sana na Ni wazuri na wamaume Ni wachache Sana
 
Back
Top Bottom