NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 9,863
- 20,806
Wanabodi za asubuhi!naenda moja kwa moja kwenye mada.
Kwa wale makomredi wa chama tawala naombeni ufafanuzi wenu kuhusu lengo la kuua upinzani nchini linaisaidiaje CCM kama chama tawala? Upinzani si ndio kioo? kama kwa miaka mingi upinzani umekuja na ajenda nyingi za wananchi ambazo serekali imefanyia kazi kwanini mnauua? Ni kwa faida ya chama au mtu mmoja?
Wakati wa JK upinzani ulizuia nini? Ulizuia ujenzi wa miundo mbinu? Ulizuia uchumi? Mbona ulikuwepo na nchi ilisonga mbele? Ni nani huyu anaeuua? Ni CCM au mtu? Kama ni mtu ana ajenda gani binafsi ambazo chama tawala hakijui? MIMI TANGU NIPATE AKILI SIJAWAHI ONA UPINZANI UKIWA KIKWAZO CHA MAENDELEO
Mniambie ni maendeleo gani ambayo yamezuiwa na upinzani? Je ni stigglers gorge? Hawakusema taratibu za bajeti zifuatwe? Je ununuzi wa ndege? Hawakusema bunge ndio lenye idhini ya kupitisha bajeti ya manunuzi? Je ni elimu bure? Je hawakusema wao wanataka kuanzia msingi hadi chuo?
Makomredi naombeni majibu. Kuua upinzani je ndani ya ilani ya CCM imeidhinishwaje? Mkakati ndani ya ilani unasemaje? Ndio huku kukimbia kupokea fomu za wagombea wa upinzani? Ndio huku kununua wapinzani? Ndio ilani ya CCM imesema hayo? Huyo anaeua upinzani mnadhani ana malengo ya kutoka madarakani? Kama anaua upinzani ni kwa faida ya nani kama ataondoka madarakani? JIULIZENI UPINZANI UNAKUFA KWA FAIDA YA NANI? JE NI NCHI? MTU? AU CHAMA?
KARIBUNI MAKOMREDI WA KIJANI KWA MAJIBU MJARABU!!!