Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
DHAMIRA YA SERIKALI NI KUJENGA BARABARA YA NDALA - MWAWAZA KWA KIWANGO CHA LAMI
"Barabara inayotoka Ndala kwenda Mwawaza Manispaa ya Shinyanga palipo na Hospitali ya Rufaa ipo kwenye Ilani ya CCM 2020-2025 lakini Makamu wa Rais alikuja Shinyanga akatoa ahadi. Ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami?" - Mhe. Dkt. Christina Christopher Mnzava, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga
"Naomba nimuhakikishie Mbunge Christina Christopher Mnzava kuwa barabara hii ipo kwenye Mpango na fedha zikipatikana dhamira ya Serikali ni kuhakikisha barabara inajengwa kwa kiwango cha lami ili iweze kuwanufaisha wananchi" - Mhe. Zainab Katimba, Naibu Waziri TAMISEMI