BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
DHAMIRI YAMLAZIMISHA RAIS MAGUFULI KUKIRI UHARIBIFU KATIKA UCHAGUZI WA OKTOBA 2020!
Nilipokuwa nahojiwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, nililazimika kumueleza mmoja wa maofisa waliokuwa wananihoji nikasema kuwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 haukuwa Huru na wala haukuwa wa Haki. Aliponiuliza kama nilikuwa na ushahidi nilimjibu kuwa ndio ninao ushahidi!
Kama Madiwani waliopatikana katika Uchaguzi ule wamekataliwa na Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama chao kwa kuwaambia hadharani na ametamka kwa ujasiri kuwa hawakuchaguliwa na watu, je walichaguuliwa na nani? Jibu hapa rahisi na la wazi nalo ni kuwa walichaguliwa na Tume ya Uchaguzi!
Tunaweza kusema kuwa kwa maneno na kauli ya Rais Magufuli, Tume ya Taifa ya Uchaguzi haikutenda Haki na haijawa Huru machoni pa Watanzania na hata machoni pake yeye mwenyewe. Kama Madiwani wale hawakuchaguliwa na watu, sahihi kabisa pia kuwa Wabunge, na Rais nao hawakuchaguliwa na watu kwa kuwa wote walipatikana katika Uchaguzi mmoja uliosimamiwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo ndiyo inayolalamikiwa!
Tunawaalika Watanzania wote kujitokeza na kushiriki kwa kikamilifu katika kampeni za kuhamasisha umma wa Watanzania kuhusu umuhimu na uhitaji wa Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Nitakuwa nikingoza kampeni hizo katika nchi nzima nikiwa nimevalia majoho ya Kiaskofu!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfutate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula