Tume huru ni hitaji muhimu la Taifa. Kampeni ya kuidai ni muhimu.
Maandamano yanaweza kuwa sehemu ya kampeni hiyo.
Maaskofu waliovaa majoho wanaweza, na wanapaswa, kuwa sehemu ya maandamano hayo.
Lkn maandamano hayawezi, na hayapaswi, kuwa hatua ya kwanza.
Hatua ya kwani ni, na inapaswa kuwa, kujibu swali lifuatalo na kuhakikisha waandamanaji watarajiwa wanaelewa jawabu kwa swali:
TUME HURU INAYOTAKIWA TANZANIA NI KITU GANI NA SIO KITU GANI?
Nadharia kabla ya utekelezaji ni muhimu sana kwa kuwa itatuwezesha kufanya tathmini baada ya kutenda.