KING KIGODA
JF-Expert Member
- Dec 28, 2018
- 3,893
- 3,145
Huyu anampaka chemchem za juu!.[emoji23][emoji23][emoji23]Chemchem ndio spring
Sasa ona Muhammad alivyo patia kuelezea Koran , nyie mnaweka mapicha ya bahari
I was sitting behind the Messenger of Allah (ﷺ) who was riding a donkey while the sun was setting. He asked: Do you know where this sets ? I replied: Allah and his Apostle know best. He said: It sets in a spring of warm water (Hamiyah) Sunan Abi Dawud 4002
TAYARI UMEMKALISHA SASA KWA AIBU KUBWA ANAJICHEKESHA.[emoji16][emoji23][emoji2]Ayoub34:16
Je! Umeziingia chemchemi za bahari, Au umetembea mahali pa siri pa vilindi?
Unajichekesha
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hapa nilipo kila siku jua linazama mlimani.Muhammad ameweka wazi ndipo Jua linapozama
I was sitting behind the Messenger of Allah (ﷺ) who was riding a donkey while the sun was setting. He asked: Do you know where this sets ? I replied: Allah and his Apostle know best. He said: It sets in a spring of warm water (Hamiyah) Sunan Abi Dawud 4002
Matendo ya Yesu ni yapi?.Ebu yaweke hapa.Nyie wavaa kobaaz okokeni mufuate matendo ya kristo achacheni na mudy yule ni agent wa shetani
Prove kwamba hayupo.common sense inanileta kuelewa kuwa daku ni kujiandaa masaa mengi kuhimili njaa! Unakula /inakunywa saa kumi hayo maji/uji ili ikusaidie kufika saa 12 , maana si rahisi/ni mateso kuhimili njaa,, kiu etc kwa saa zaisi ya 12 kesho yake.
Hivi tabu yote ya nini? Unatafuta nini? Bada? Kwani lazima ujitese? Ili iweje? Kuingia mbinguni? Who knows kama kuna Mungu? IMANI, IMANI IMANI
Mimi ni muislamu na sikubaliani na wanayofanya zanzibar ya kuzuia watu kuuza migahawa mchana wa ramadhani maana hakuna dalili yoyote kidini katika kwamba nabii muhammad (radhi za Allah ziwe juu yake) aliwahi kufanya hayo.Swali zuri Sana madam Numbisa
Kama nilivyoeleza awali maana halisi ya Daku,pamoja na mambo mengine ni kumuwezesha mfungaji kuwa na stamina ili apate kuendelea na majukumu yake kama kawaida pasina kuwa na uchovu mwingi
Sasa,
Dhana nzima ya kuwazuia watu Kula chakula hadharani au kuuza vyakula ni Kwa Nia moja Tu kuheshimu mwezi mtukufu WA ramadhani na kuwahimiza watu wafunge au watekeleze ibada ya funga.
Na utaratibu huo hufanywa kwenye maeneo yenye waislamu wengi kama Zanzibar Kwa maana wengi wao ni waumini WA kiislamu hivyo hawana budi kufunga,na si rahisi kukuta huku bara kuna mambo kama hayo.
Lakini hata Kwa utashi WA kawaida Tu Kwa ibada kama ya mwezi wa ramadhani ambayo ni maarufu Sana na waislamu wengi wanafunga je si Busara basi kutokula hovyo hovyo hadharani?
Ebu chukulia wewe Numbisa let's say upo na wapangaji wenzako karibia wote wamefunga je itakuwa Busara ukiwa nao barazani mnabadilishana mawili matatu basi ukawa na msosi wako unakula mbele yao je ni Sawa?
Ni sawa kula mbele ya aliyefunga maana funga ni ya kwake yeye na Allah( subhanna huwataala) mbona mimi nikiwa na swaum nakaa na rafiki zangu na wengi huwa wanakula kawaida tu na wala sitamani wala nini maana nimefunga .Swali zuri Sana madam Numbisa
Kama nilivyoeleza awali maana halisi ya Daku,pamoja na mambo mengine ni kumuwezesha mfungaji kuwa na stamina ili apate kuendelea na majukumu yake kama kawaida pasina kuwa na uchovu mwingi
Sasa,
Dhana nzima ya kuwazuia watu Kula chakula hadharani au kuuza vyakula ni Kwa Nia moja Tu kuheshimu mwezi mtukufu WA ramadhani na kuwahimiza watu wafunge au watekeleze ibada ya funga.
Na utaratibu huo hufanywa kwenye maeneo yenye waislamu wengi kama Zanzibar Kwa maana wengi wao ni waumini WA kiislamu hivyo hawana budi kufunga,na si rahisi kukuta huku bara kuna mambo kama hayo.
Lakini hata Kwa utashi WA kawaida Tu Kwa ibada kama ya mwezi wa ramadhani ambayo ni maarufu Sana na waislamu wengi wanafunga je si Busara basi kutokula hovyo hovyo hadharani?
Ebu chukulia wewe Numbisa let's say upo na wapangaji wenzako karibia wote wamefunga je itakuwa Busara ukiwa nao barazani mnabadilishana mawili matatu basi ukawa na msosi wako unakula mbele yao je ni Sawa?
Negative is incapable of proofProve kwamba hayupo.
Hawa jamaa basi tu wanakaza fuvu lakini hawana dini kwa kweliKWA USHAHIDI KABISA,NYINYI MUANGALIZI WENU NA MCHUNGAJI WENU NI SHETANI.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
AYUBU 2
1Tena ilitukia siku moja hao wana wa Mungu walipokwenda kujiweka mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao, ili kujiweka mbele za BWANA.2BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi? Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. 3 BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ijapokuwa ulinichochea juu yake, ili nimwangamize pasipokuwa na sababu.
What is negative? And why can't it be proven and what is the link between existance of the almighty God and negative?Negative is incapable of proof
Mungu tu ndie anaaamehe dhambi ili jiwe nguvu ya kusamehe dhambi za waislamu limetoa wapi , kitu kinacho kusamehe ndio ibada yenyewe
- Sanamu jiwe unalolisujudi kila siku lisome kazi zake, kALIGUSE jiwe likusamehe dhambi 😂😂😂
- Jiwe jeusi lina fyonza dhambiza waislamu
- Ibn Abbas alisisitiza kwamba: Muhammad alisema: "Jiwe jeusi liliteremka kutoka Peponi, na lilikuwa jeupe zaidi kuliko maziwa, kisha likatiwa weusi na dhambi za watoto wa Adamu. Jami` at-Tirmidhi 877
- Jiwe jeusi kutoa hukumu siku ya mwisho
- Imesimuliwa kwamba Ibn 'Abbaas alisema: Muhammad alisema juu ya Jiwe: "Na Allaah, Allaah Atalileta jiwe hiyo Siku ya Kiyama, na jiwe litakuwa na macho mawili na ambayo yanaona na mdomo ambao utaongea , na jiwe litashuhudia kwa wale walioigusa kwa moyo wa kweli. "Jami` at-Tirmidhi 961
- Jiwe linafuta dhambi likiguswa kwa moyo wa kweli
- Imesimuliwa kutoka kwa Abdullah bin Ubaid bin Umair kwamba: "Ewe Abu abdur-Rahman, kwanini nikuone tu ukigusa hizi pembe mbili?" Alisema: "Muhammad alisema: Kuzigusa zinafuta dhambi." Sunan an-Nasa'i 2919
Ayo maandiko ni yenu wala hayanihusuACHA UPOTOSHAJI!!!
Ivi Kwanini mnabishia mtume pedophile MuhammadHapa nilipo kila siku jua linazama mlimani.
Kama unabisha nakuwekia picha hapa.
Embu kataa Aya maandiko ya wabusu jiweACHA UPOTOSHAJI!!!
Naomba nikupe Elimu kuhusu jiwe jeusi kwa kifupi sana;
Alkaaba ilijengwa na Ibrahim na mwanae Ismail kwa maelekezo ya Mungu ili wanadamu wapate pa kuelekea wakati wanafanya Ibada. Jiwe alilotumia Ibrahim (kama ngazi) kusimama ili ajenge sehemu ya juu ya Alkaaba lipo hadi leo hapo pembeni ya alkaaba (kwa nje) na lina alama ya Unyayo wake (usiniulize aliwezaje kubonyeza jiwe kwa miguu yake)
Kuhusu jiwe jeusi; Baada ya Ibrahim kukamilisha ujenzi wa alkaaba, alisema aweke alama hata huko baadae kama alkaaba itajengwa upya watu wajue eneo halisi ilipo jengwa; Ili kuweka alama ndio akatafuta jiwe la tofauti na yaliyokuwepo eneo hilo akapata jiwe la tofauti akaliweka (ndilo watu huita jiwe jeusi)
Kwa maelezo hayo; hilo jiwe liliwekwa kama alama ya kuonesha alkaaba ilipojengwa na sio vinginevyo...
Kwa kifupi sana hayo ndio maelezo yake wala hakuna mtu anaye abudu jiwe jeusi; ni UPOTOSHAJI !!!
Usikubali kudanganywa na wasio na Elimu huko mtaani au wanaopotosha uislam kwa manufaa yao binafsi...
Aise karibu kwangu bro napenda wageni kipindi hiki.Daku inaambata na Vigoma siku hizi ukifika mwezi wa Ramadhan vile Vigoma vya Kula Kula Daku Mpemba na kinyago anaecheza Vigoma hakuna tena, sijui nani alieua vile Vigoma vya Daku siku hizi hakuna watu wanawaza kula tu na kula kwenyewe wanakula kiuchoyo zamani ukifika mda wa futari unachagua Baraza la kwenda kula na hufukuzwi na kingine utakuta umeletewa nyumbani ule,
Yaan zamani mwezi wa Ramadhani waislamu walikua wakalimu sana nazungumzia waislamu wote sio wahisani Ila siku hizi sijui njaa imezidi Ramadhan waislamu wanakula wenyewe ule utaratibu wa kula kibarazani umekufa hakuna kukaribisha mtu na hakuna kumpelekea mtu (jirani) chakula,
sababu kubwa kisayansi kwanini watu wapendelea kula mihogo,viazi,magimbi na uji ni sababu vina starch kubwa hivyo ni kurudisha nguvu mwilini iliyopotea maana sukari ndio mafuta ya mwili.Kuna post moja nimeiyona ingawa ilikuwa inazungumzia kwaresma lakini mwandishi wa post hiyo alikuwa na lengo la kukashifu dhana nzima ya Futari na Daku.
Kwake yeye Kwa mujibu wa Imani yao wanakula chakula chochote kile tofauti na watu wa Imani nyingine ambayo pasina kuficha na Imani hii ni Uislamu.
Kwa uelewa wa mwandishi anachoelewa yeye kuhusu Futari cha kwanza kinachomjia kichwani kwake ni uji, viazi au mihogo na tambi, kwake yeye hiyo ndio Futari.
Na Daku ni chakula ambacho kinaliwa usiku sana kama ugali, wali na ndizi na kadhalika, kwahiyo kana kwamba anaona fahari kwamba wao hawana mambo hayo kwahiyo mambo yao yapo super.
Ningependa nimpe elimu juu ya mambo haya ili ukungu umtoke katika ubongo wake na apate kujua usahihi wa dhana ya Futari na Daku ili kesho na kesho kutwa asirudie tena kuongea huo upuuzi.
Futari imetokana na neno kufuturu kwa Kiswahili chepesi ni mlo wa kwanza baada ya kufunga swaumu, kwahiyo kile chakula cha kwanza kukila baada ya kufungua ndio huitwa Futari, na yaweza kuwa tende au maji, ukipata kimoja kati ya hicho hapo tunasema umefuturu, na chakula kingine ni ziada tu kwa maana kinahesabika kama chakula kingine tu.
Tofauti na watu wa Imani nyingine, Futari au kufuturu ni ibada na ina utaratibu wake, miongoni mwa mambo muhimu ya kufanya kwa mwenye kufunga ni kutakiwa kufuturu mapema au haraka mara baada tu ya kuingia Magharibi baada ya jua kuzama.
Hapo hutakiwa kupata tende au maji kwani hivyo ndio vitu ambavyo ni Sunna kutoka kwa Mtume wetu, lakini hata hivyo hakuna aweza kufuturu Kwa biskuti, matunda, karanga au na chochote kile ambacho anaweza kuipata Kwa wakati huo, hapo ndio tunasema kufuturu.
Kwahiyo funga ya muislamu au mwezi wa Ramadhani unaweza kufungwa hata bila ya uwepo wa uji, au viazi, ndizi, magimbi na kadhalika, hivyo ni vyakula tu ambavyo vimezoeleka lakini sio kwamba bila hivyo haipatikani funga, mtu anaweza kufuturu kwa chai na mkate au chapati na hiyo ndo ikawa Futari yake.
Daku ni chakula ambacho huliwa usiku Sana na inashauriwa kuanzia saa nane, tisa mpaka saa kumi usiku, lakini hii nayo ni ibada pia, kwa maana ni bora zaidi kuchelewa kula Daku kama ambavyo ni bora zaidi kuwahi kufuturu, na unapata thawabu kwa kufanya haya.
Daku ni chakula kilicho barikiwa na ndio maana waislamu wanasisitizwa sana mwezi wa Ramadhani wajitahidi Kula Daku, lakini ifahamike kwamba Daku inaweza kuwa glasi moja ya maji au maziwa, au chai na andazi au chapati, ili mradi tu upate chochote kidogo cha kula usiku huo, na hiyo ndio Daku.
Kwa mfano unaweza kula wali wako au ugali saa tano usiku halafu usiku ukaamka kunywa chai tupu au juisi au maziwa ndio ikawa Daku yako, hapo unapata baraka.
Na haya mambo ya kudhani Futari ni viazi, mihogo, ndizi, magimbi na uji au chai huwa tatiza hata baadhi ya waislamu kwa kusema hawana hela ya Futari na hivyo kushindwa kufunga swaumu, huo ni uelewa mbaya sana na ni kukosa maarifa kabisa.
Tupende kujifunza na kupata elimu ili tufanye mambo sahihi kwa wakati sahihi kabisa.
Natumaini wale ambao walikuwa na uelewa mbaya kuhusu Futari na Daku walau kwa uchache watakuwa wamepata maarifa na kutoa ukungu katika vichwa vyao.
Ni hayo tu!
johnthebaptist
Numbisa
Shukrani chiefsababu kubwa kisayansi kwanini watu wapendelea kula mihogo,viazi,magimbi na uji ni sababu vina starch kubwa hivyo ni kurudisha nguvu mwilini iliyopotea maana sukari ndio mafuta ya mwili.