Swali zuri Sana madam
Numbisa
Kama nilivyoeleza awali maana halisi ya Daku,pamoja na mambo mengine ni kumuwezesha mfungaji kuwa na stamina ili apate kuendelea na majukumu yake kama kawaida pasina kuwa na uchovu mwingi
Sasa,
Dhana nzima ya kuwazuia watu Kula chakula hadharani au kuuza vyakula ni Kwa Nia moja Tu kuheshimu mwezi mtukufu WA ramadhani na kuwahimiza watu wafunge au watekeleze ibada ya funga.
Na utaratibu huo hufanywa kwenye maeneo yenye waislamu wengi kama Zanzibar Kwa maana wengi wao ni waumini WA kiislamu hivyo hawana budi kufunga,na si rahisi kukuta huku bara kuna mambo kama hayo.
Lakini hata Kwa utashi WA kawaida Tu Kwa ibada kama ya mwezi wa ramadhani ambayo ni maarufu Sana na waislamu wengi wanafunga je si Busara basi kutokula hovyo hovyo hadharani?
Ebu chukulia wewe
Numbisa let's say upo na wapangaji wenzako karibia wote wamefunga je itakuwa Busara ukiwa nao barazani mnabadilishana mawili matatu basi ukawa na msosi wako unakula mbele yao je ni Sawa?