Dhana ya kurudia kitu mara tatu na uumbaji wa roho

Dhana ya kurudia kitu mara tatu na uumbaji wa roho

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Tunajidili namba tatu kivingine leo... Sio tatu kama tatu la hasha bali mara tatu.

Tuangalie kwanza jinsi uhai unavyotengenezwa;
  • Makutano ya jinsia mbili tofauti
  • Kutungwa mimba
  • Kuzaa
Mfano huu ndio unaotumika kwingine kote kutengeneza roho ama kuumba. Kwenye kiapo cha ndoa unaapa mara tatu, kiapo cha urais pia na viapo vingine mbalimbali..

Kiapo cha kwanza ni makutano
Kiapo cha pili ni kutungwa mimba
Kiapo cha tatu ni kujifungua mtoto..

Hapo tayari unakuwa umeshaumba roho ya kitu husika.

Waganga wa kienyeji wanapokutuma kufanya kitu... Hukwambia kafanye mara tatu. Wachawi wanapotaka kutengeneza maroho yao baada ya kumaliza kutengeneza matanguli yao hughani mara tatu..

Ukisikia maneno huumba ndio hii. Lakini ni vema kutenganisha uumbaji wa Mungu na huu wa binadamu... Yeye alitamka mara moja tu na ikawa... Hata hiki tunachoita uumbaji wa roho za mapepo kichawi nk.. Si uumbaji hasa bali ni kutengeneza tu jumba linalofit jumba fulani bila kujali kama ni physical ama invisible...

Na katika uumbaji wote wa hizi roho hakuna uumbaji mbaya kama wa viapo kwakuwa hivi mwili wake ni invisible. Je, wewe umejihusisha na viapo!? Mara ngapi? Vinahusiana na nini!? Umetengeneza maroho bila kujijua..

Sasa tunaviua vipi hivi viapo!? Ili roho yake isiwe na nguvu ya kuleta madhara tena!?
Hakuna njia nyingine zaidi ya kurudia mchakato uleule.

Mfano kama mtu alijiapiza kukulaani maybe mzazi.. Ukitafuta suluhu naye akakubali yaishe ni lazima umuulize mara tatu;
Ni kweli umenisamehe?
Kwa roho moja?
Moja kwa moja!?

Huu ni mfano tu lakini ni lazima utafute njia ya kumfanya arudie mara tatu.. Iko hivyo!
 
Tunajidili namba tatu kivingine leo... Sio tatu kama tatu la hasha bali mara tatu
Tuangalie kwanza jinsi uhai unavyotengenezwa
.Makutano ya jinsia mbili tofauti
. kutungwa mimba
. kuzaa
Mfano huu ndio unaotumika kwingine kote kutengeneza roho ama kuumba.....
Kwenye kiapo cha ndoa unaapa mara tatu, kiapo cha urais pia na viapo vingine mbalimbali....
Kiapo cha kwanza ni makutano
Kiapo cha pili ni kutungwa mimba
Kiapo cha tatu ni kujifungua mtoto...
Hapo tayari unakuwa umeshaumba roho ya kitu husika
Waganga wa kienyeji wanapokutuma kufanya kitu... Hukwambia kafanye mara tatu
Wachawi wanapotaka kutengeneza maroho yao baada ya kumaliza kutengeneza matanguli yao hughani mara tatu... Ukisikia maneno huumba ndio hii
Lakini ni vema kutenganisha uumbaji wa Mungu na huu wa binadamu... Yeye alitamka mara moja tu na ikawa... Hata hiki tunachoita uumbaji wa roho za mapepo kichawi nk.. Si uumbaji hasa bali ni kutengeneza tu jumba linalofit jumba fulani bila kujali kama ni physical ama invisible...
Na katika uumbaji wote wa hizi roho hakuna uumbaji mbaya kama wa viapo kwakuwa hivi mwili wake ni invisible
Je wewe umejihusisha na viapo!? Mara ngapi? Vinahusiana na nini!? Umetengeneza maroho bila kujijua
Sasa tunaviua vipi hivi viapo!? Ili roho yake isiwe na nguvu ya kuleta madhara tena!?
Hakuna njia nyingine zaidi ya kurudia mchakato uleule
Mfano kama mtu alijiapiza kukulaani maybe mzazi.. Ukitafuta suluhu naye akakubali yaishe ni lazima umuulize mara tatu
Ni kweli umenisamehe?
Kwa roho moja?
Moja kwa moja!?
Huu ni mfano tu lakini ni lazima utafute njia ya kumfanya arudie mara tatu.....
Iko hivyo
Who is mshana Jr
 
No 3 is a sacred number just like 6 and 9. or angelic no. like 11.11.11 simply 11. Roman catholic believe on Holly Trinity.
Baba, Mwana na Roho mtakatifu. Number hii hutumiwa hata na wachawi kwa hiyo usishangae kwa kuwa kitu kitakatifu kinaweza kutumiwa kufanya just opposite yake. Let me say that instruments that are used to guard is the same instrument used to kill.
 
Leo sijaelewa vzr somo ....Je ikitokea mtu akakulaani mara moja Je iyo laana inaweza kikufikia.
Laana sio utani. Utani ndio huwezi kurudia rudia kwenye session moja ya utani. Laana ni kudhamiria, haitokei mara moja kama utani. Kabla laana haijatolewa mtoa laana alisha dhamiria na ikawa kweli ndani yake .. kwenye subconscious mind.
Ili subconscious mind ipokee hilo inapaswa kurudia rudia na minimum ni set ya ya tatu. Ukilaniiwa unajulishwa rasmi kuwa ulishalaaniwa!
 
Huwa nasoma nyuzi zako na kuzitafakari vyema sana,
Nataka nikuulize swali flani, Hivi we Mshana Jr :,
-mchawi
-mganga wa kienyeji
-muhenga
-jini
-mchungaji/shehe
-alien
-msukule
Ni hayo tu
 
Leo sijaelewa vzr somo ....Je ikitokea mtu akakulaani mara moja Je iyo laana inaweza kikufikia.
Yes laana hairudii mara 3kwakuwa yenyewe kiroho inajizidisha mara tatu lakini ni lazima anayekulaani awe na muunganiko nawe
Inajizidishaje mara 3?
Baba
Mama
Na wewe Mtoto
Kama ni mtu baki je? Uumbaji haudhihakiwi.. Hivyo kuna
Mungu katika utatu mtakatifu
 
Laana sio utani. Utani ndio huwezi kurudia rudia kwenye session moja ya utani. Laana ni kudhamiria, haitokei mara moja kama utani. Kabla laana haijatolewa mtoa allana alisha dhamiria na ikawa kweli ndani yake .. kwenye subconscious mind.
Ili subconscious mind ipokee hilo inapaswa kurudia rudia na minimum ni set ya ya tatu. Ukilaniiwa unajulishwa rasmi kuwa ulishalaaniwa!
Iko vizuri asante sana
 
NAMBA 3 INA MAMBO MENGI SANA KAMA HIVI PIA.
  1. Wagonjwa wengi hupewa dawa yenye dozi ya kutwa mara tatu.
  2. Kila mtu anatakiwa kujitambulisha kwa majina matatu.
  3. Waamini fulani wanaamini kuwa Mungu ana nafsi tatu.
  4. Wakati wa mateso ya Yesu, alianguka mara tatu.
  5. Yesu alisulubiwa na watu wengine wawili na hiyo kufanya idadi ya waliosulubiwa kuwa ni watatu.
  6. Imani hii inaendelea kwamba alifufuka siku ya tatu ilivyoandikwa.
  7. Jiko imara lina mawe au maegemeo matatu; angalia hata jiko la mchina na la gesi.
  8. Kabla ya kuanza riadha inahesabiwa moja mpaka tatu.
  9. Katika mashindano wanaong'ara ni mshindi wa kwanza, wapili na watatu.
  10. Waamini wengine kabla ya ibada lazima wajisafishe mara tatu.
  11. Mambo makuu kwa kila kiumbe hai ni kula, kuvaa na kulala
  12. Binadamu huzaliwa ,kuoa au kuolewa na kufa
 
Yes laana hairudii mara 3kwakuwa yenyewe kiroho inajizidisha mara tatu lakini ni lazima anayekulaani awe na muunganiko nawe
Inajizidishaje mara 3?
Baba
Mama
Na wewe Mtoto
Kama ni mtu baki je? Uumbaji haudhihakiwi.. Hivyo kuna
Mungu katika utatu mtakatifu
Kwaiyo mtoto anaweza kumlaani baba yake au mama yake kama wamemkosea.
 
Back
Top Bottom