Francis, nataka nijibu hoja zako kama hapo juu.
1-Wafanyakazi, kuna nyongeza kama promotion uki badilishiwa majukumu hii huna shida nayo lakini kuna nyongeza ya madaraja mfano mwalimu wa mwaka wa kwanza hawezi kupokea sawa na mwalimu wa miaka 10 wakiwa na same qualifications, akianza kazi anaanza na Minimum mshahara katika grade ile ila kila akipata ujuzi anapanda level ili afike Max katika daraja lilelile ikitokea kapanda kuwa mwalimu mkuu hapo promotion anaanza katika grade mpya Min ataanza kupanda slowly kufika Max hii ni haki ya mfanyakazi kisheria.
2- Kuna hii kuongezwa mshahara kwa ujumla wafanyakazi wote kila mwaka hii inategemea na inflation na C.Bank wao wanatoa data hapo serikali ikiona kweli inflation ni kubwa inatoa kufidia na uwezo wa serikali, lakini ukiona inflation kubwa lakini serikali hawana pesa basi uchumi mbaya na kama wakitoa basi ni lazima wa manage inflation kuwa positive. Inflation inaongeza ukuwaji wa kiuchumi ni dalili watu wanaweza kufanya manunuzi wengi, tatizo kubwa ikiwa inflation ni over supply ya pesa kwa maana labda kuna pesa chafu watu wanapiga deal wanaiba pesa nyingi hawa wataleta inflation mbaya maana wataanza kununua vitu sio bei yake na kuwaumiza wengine kama ilivyokuwa miaka fulani Dar. nchi ikiwa haina inflation kabisa hiyo ni dalili ya uchumi kusinyaa na umaskini, inflation nzuri lakini kuwa managed.
3- Umeme watapunguza tu ili tufikie ushindani na nchi zingine sababu umeme wetu ni ghali ila kusema kuwa tuajiri tu wengine je una uhakika miaka 10 ijayo uchumi utakuwa endelevu na kuwalipa hawa wafanyakazi. chukuwa mfano una mfanyakazi nyumbani kwako unamlipa laki moja, kesho anakuja anakwambia naomba nyongeza maisha magumu utamwambia badala ya kukupa bora niongeze mfanyakazi mwingine nitakupunguzia kazi za kufanya, hapana utampa alfu 20 bora kuleta mwingine.