Dhana ya maisha

Dhana ya maisha

Ryan The King

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
2,788
Reaction score
2,690
Nawasalimu kwa lugha zenu, ishara na mitindo mbalimbali ya salamu zenu kwa kuzingatia umri, elimu, tamaduni mitazamo, falsafa na Itikadi Zenu.
Nafurahishwa na uwepo wenu katika jukwaa hili, basi na iwe furaha kwenu kama ilivyokuwa desturi kwangu.

Nikirudi kwenye Mada;

Maisha ni uwepo wa ukinzani baina ya mambo mawili yasiyofanana. Huu ni mtazamo wangu kulingana na jinsi nilivyotafakari. Bila kuwa na ukinzani basi ni wazi hakuna maisha.

Ukinzani ni kitendo cha mambo mawili kutokubaliana katika jambo moja. Ukinzani huu umenifanya nitoe kanuni ambayo nimeiita "UWILI".

Bila kuathiri kanuni za asili na zile za kibinadamu, kanuni hii ya Uwili ndio inafanya maisha yaweze kuendelea.

Je kuna wakati ulijiuliza moja ya maswali yafuatayo:-
1- kwa nini kuna nyuma na mbele, Juu na chini, mashariki na Magharibi, Jinsia ya kike na kiume, Wema na ubaya nakadhalika.

2- Je kungekuwaje ikiwa kanuni hizi za Uwili zisingekuwapo?

Ukweli ni kuwa hakuna maisha bila Kanuni ya Uwili.

Kanuni hii ndio huleta maana kamili ya dhana nzima ya Maisha. Kanuni hii ndio humfanya kiumbe katika ulimwengu wa nje kuwa jinsi alivyo japokuwa katika Ulimwengu wa ndani yaani wa kiroho kanuni hii hafanyi kazi.

Maisha ni vile mtu alivyo, ajionavyo, alivyonavyo, Pamoja na vile na wale wanaomzunguka. Hii huweza kuwa maana kamili ya dhana ya Maisha.

Hakuna maisha zaidi ya jinsi mtu alivyo, ajionavyo na mazingira yake.
Hivyo hatuwezi kutamani au kutafuta mambo yaliyo nje ya uwezo wetu.

Ikiwa mtu atataka mambo yaliyo nje ya uwezo wake basi hujitafutia matatizo yake mwenyewe katika Ulimwengu huu unaoonekana, hivyo kuathiri baadhi ya Elementi za Ulimwengu wa ndani kama Furaha, amani, na Upendo(Kanuni chanya za rohoni). Na Elementi hizi zikiharibiwa mtu huyo hujikuta katika maradhi ya mwili ambayo huweza kudhani amelogwa.

Pia kama mtu atafanya mambo chini ya kiwango chake basi matokeo huweza kuwa mabaya kuliko ya yule aliyetenda juu/nje ya uwezo wake.

MAISHA NI MTAZAMO, NJIA, MATOKEO

Mtu huweza kuwa na mtazamo Chanya lakini hutumia njia hasi hivyo hupata matokeo mabaya.

Mtu fulani ataungana na Mimi kuwa, watu wengi ukiwauliza jambo lolote katika kufanikiwa katika maisha, huwa mawazo mazuri, maono, na mitazamo ya faida lakini ukiyaangalia maisha yao utashindwa kushangaa jinsi Ufukara ulivyowapiga.

Pia Mtu huweza kuwa na mitazamo hasi lakini hutumia njia Chanya na mwishowe kupata matokeo mazuri.

Ikumbukwe kwamba Mitazamo huathiri Njia au mbinu, na hakuna mahusiano ya moja kwa moja baina ya Mitazamo ya Maisha na Matokeo yake katika Maisha. Bali kuna uhusiano wa njia na Matokeo.

Maisha huongozwa na kanuni ya UWILI.
 
Utanisamehe mi mgumu kuelewa!!

ni ukinzani upi na upi uliosababisha maisha..?
 
Utanisamehe mi mgumu kuelewa!!

ni ukinzani upi na upi uliosababisha maisha..?

Wala usijali Mkuu, wewe wala si mgumu wa kuelewa. Bali unahitaji uchambuzi yakinifu ili uweze kujiamini kwa kile ulichokuwa unataka kukijua.

Ni kwamba Ukinzani ni Uvutano baina ya mambo au vitu viwili visivyofanana.
Vitu hivyo ndio huleta kanuni ambayo nimeipa jina la "UWILI".

Ukinzani unaosababisha maisha ni pamoja na uwepo wa Jinsia ya kike na kiume ambayo ndio huleta ongezeko la viumbe duniani.

Ukinzani wa Wema na Ubaya, mwanga na Giza, Mauti na Uzima.

kumbuka kanuni hii hutumika katika ulimwengu huu unaoonekana.
 
Wewe binafsi unaelewa maisha ni nini...?
 
sijakataa kwamba huelewi we niambie maisha ni nini..?
 
"Maisha ni vile mtu alivyo, ajionavyo,
alivyonavyo, Pamoja na vile na wale
wanaomzunguka. Hii huweza kuwa
maana kamili ya dhana ya Maisha."
Soma vizuri kwenye posti mbona maaana ipo mkuu
nielewavyo mimi maisha ni uhai hayo uloyataja hapo ni vitu ambavyo kiumbe hai huanavyo/huvitenda baada ya kuwa hai,
unapokuwa hai unaweza kutenda vitu tofautitofauti so hiyo ni mienendo ya maisha.
 
Ukinzani upo hata kabla ya viumbe kuwako, hata wewe kuja kwako ni kutokana na Uvutano wa jinsia ya kike na kiume. Ndio maana Hata Mungu akasema sio vyema huyu mtu(Adam) awe peke yake. Unadhani ni kwa nini Mungu hakuumba mwanaume wa pili ili amsaidie Adamu?

Unaweza kunipa majibu kwa nini kuna usiku na Mchana?

Je kuna ulazima gani wa kuwa na Juu na Chini?

Ni wazi Maisha ni Ukinzani wa kanuni za Uwili ili yaweze kuendelea.

Bila Uwili hakuna Maisha mkuu
 
When people see some things as beautiful, other things become ugly.
When people see some things as good, other things become bad.
Being and non-being create each other.
Difficult and easy support each other. Long and short define each other.
High and low depend on each other.
Before and after follow each other.

Lao Tsu.

Mimi naweza kuongezea kuwa uwili unaletwa na perception.
 
hiyo ni kweli, ndio maana nikasema kwa nionavyo, kumaanisha mwingine anaweza kuona tofauti na Mimi na huo ndio ukinzani.
 
hiyo ni kweli, ndio maana nikasema kwa nionavyo, kumaanisha mwingine anaweza kuona tofauti na Mimi na huo ndio ukinzani.

Sizingumzii perceptions kati ya anayeamini mtazamo huo na asiye amini. Nazungumzia perceptions in our minds.
 
Back
Top Bottom