Hivi unaelewa nini kusema kikosi kipana, mi ninavyoelewa ni kwamba tunaposema kikosi kipana manake kagere akiumia Boko anacheza, Husein akiumia Kwasi anacheza, ameumia kapombe Gyne anacheza.Kuna dhana kuwa Simba wana kikosi kipana , hii sio halisi. Matokeo ya finali ya Mapinduzi cup yanapingina na msemo huu. Ukweli ni kwamba Simba ni ya Okwi, kagere, bocco, mkude, shabalala, chama, Wawa, na manula. Wakikosekana hawa Simba haifanyi vizuri.
Wasio jua nini mana ya kikosi kipana wanafikiri tunasema simba ina vikosi viwili, hapana. Msilete tafsiri ya vikosi viwili na kikosi kipana.
Mwenye kuelewa atanielewa lakini Wenye kubadili mada hawawezi kuelewa.
Mfano hata man city ana kikosi kipana lakini hana vikosi viwili
Sent using Jamii Forums mobile app