Dharau ya Waarabu kwa Waafrika Zanzibar, kumbe Mwalimu Nyerere 1957 aliwaonya kwanza kabla ya kuanzisha ASP

Dharau ya Waarabu kwa Waafrika Zanzibar, kumbe Mwalimu Nyerere 1957 aliwaonya kwanza kabla ya kuanzisha ASP

Zanzibar-Nyamwezi

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
1,244
Reaction score
766
1957 kabla ya kuunda chama cha ASP, Mwalimu Nyerere aliwasihi sana Waarabu Zanzibar wawaruhusu Waafrika kupiga kura, walipokataa aliwaonya kuwa that was the last chance.

Usiku huohuo akaanza vikao Rahaleo Mjini Zanzibar, kuanzisha ASP akiongozana na Mtemvu katibu wa TANU, Karume akakataa Uenyekiti wa ASP akiogopa kuuliwa na alidai ana mke na watoto wadogo, Mwalimu alimuweza alipomwambia chochote kitacho kutokea basi Mimi kama tulivyoshibana niamini wanao hawatopata shida nitawachukua.

Hapo ndio mwanzo wa Mapinduzi. Silaha alizileta mwalimu toka Algeria. (Simulizi za Sheikh Ali Muhsin Bin Barwani YouTube)
 
Usiseme dharau, sema kuwafanya watumwa, kuwabaka mama, mababa, watoto wadogo wawe wa kike au kiume, kuwauwa na kuwazika chini ya majengo, sasa linganisha na fadhila za vinyago..

Mbona hayo yanafanywa tokea siku ya uvamizi Januari 1964 mpaka hii leo au hao wanaookotwa kwenye plastiki Coco Beach wametoka mbinguni na hao wanaobambikiziwa kesi ZA kigaidi bila mpango na wengine kupigwa marisasi huyasikii.
 
Mbona hayo yanafanywa tokea siku ya uvamizi Januari 1964 mpaka hii leo au hao wanaookotwa kwenye plastiki Coco Beach wametoka mbinguni na hao wanaobambikiziwa kesi ZA kigaidi bila mpango na wengine kupigwa marisasi huyasikii
Mbona huzungumziii vifo vya Kibiti, wale wa CHADEMA waliouwawa kwa mazingira tata, huzungumzii hizo maiti kwanini ndugu wa marehemu hawajaja kusema wamepotelewa na ndugu zao, huzungumzii wale marehemu wahamiaji ambao hata madereva husika wamekiri kutupa maiti zao baharini kwenye mito n.k. Wala huzungumzii makada na viongozi wa chama tawala waliofariki kwa mazingira tata?! Tusiwe na double standard, kifo ni kifo.

Kuhusu kushambuliwa kwa marisasi, waliopatwa na haya majanga mpaka leo wamekataa kuleta wahusika ili upepelezi uwe kamilifu, tujiulize kwanini!
 
Kuhusu maandamano, sijasikia watu wakiandamana kwenye mambo muhimu kama ukosefu wa maji na umeme, miundombinu, afya, elimu, ustawi wa jamii, ukeketaji, mimba za utotoni, vyeti feki, rushwa, ufisadi n.k.
Kweli hayo ya juu siyo ya maana kuliko kusema unanyimwa uhuru wa habari wakati humu ndani tunajadili kila kitu?!
Maajabu ya Dunia kwa kweli
 
Nyerere hakuwa na mamlaka huko miaka hiyo
 
Mbona huzungmziii vifo vya Kibiti, wale wa CHADEMA waliouwawa kwa mazingira tata, huzungumzii hizo maiti kwanini ndugu wa marehemu hawajaja kusema wamepotelewa na ndugu zao, huzungumzii wale marehemu wahamiaji ambao hata madereva husika wamekiri kutupa maiti zao baharini kwenye mito n.k. Wala huzungumzii makada na viongozi wa chama tawala waliofariki kwa mazingira tata?! Tusiwe na double standard, kifo ni kifo...
Kuhusu kushambuliwa kwa marisasi, waliopatwa na haya majanga mpaka leo wamekataa kuleta wahusika ili upepelezi uwe kamilifu, tujiulize kwanini!

Wende ukadai maiti ya ndugu yako kwa watu wasiojulikana? 😛

Kuna watu wanawatafuta ndugu zao mpaka leo polisi iko kimya. Hivi unaweza kutwambia yuko wapi yule mwandishi wa habari alitaka kuchunguza mauwaji ya kibiti?? Ben Saanane yuko wapi?

Upelelezi kesi ya nyani umpelekee ngedere, kwanini kama mamlaka hawahusiki wanashindwa kuwaachia watu neutral wachunguze?
 
Kuhusu maandamano, sijasikia watu wakiandamana kwenye mambo muhimu kama ukosefu wa maji na umeme, miundombinu, afya, elimu, ustawi wa jamii, ukeketaji, mimba za utotoni, vyeti feki, rushwa, ufisadi n.k.
Kweli hayo ya juu siyo ya maana kuliko kusema unanyimwa uhuru wa habari wakati humu ndani tunajadili kila kitu?!
Maajabu ya Dunia kwa kweli
Hivi hayo yote uliyoyaandika source yake si huo utawala??

Humu ndani tunajadili huku mkiwashitaki wenye mtandao uhuru gani huo ??
 
Usiseme dharau, sema kuwafanya watumwa, kuwabaka mama, mababa, watoto wadogo wawe wa kike au kiume, kuwauwa na kuwazika chini ya majengo, sasa linganisha na fadhila za vinyago..
Hadithi za kutunga hizo! Hakuna Mzanzibari aliyefanywa mtumwa. Na kama ni biashara ya utumwa wenyewe walikuwa Wazungu ambao walitawala Tanganyika. Sijawahi kusikia CCM Tanganyika kuwatukana Wazungu.

Tujaalie Waarabu walifanya hivyo munavyosema walifanya, Shein juzi alikuweko Qatar kwa Waarabu, mbona hakuganya ziara ya Congo au Zambia kwa Waafrika wazalendo wenzetu waliotusaidia kujikomboa kuomba msaada.

Bob Marley alisema, " Tell the children the truth..."
 
Back
Top Bottom