Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Wakazi wa moja ya mitaa Mbagala Rangitatu hawana umeme tangu jana asubuhi mpaka muda huu ninapoandika hii Post. Wakazi hawa wapo mita mia tano toka ofisi ya Tanesco Mbagala na mita miambili toka Sub Station ya Mbagala, hata hivyo walishinda na walilala bila umeme kwa zaidi ya saa ishirini na nne japo kila wakipiga simu Tanesco jibu ni taarifa tunayo na mafundi wapo saiti!
Wakazi hawa wanapata umeme toka kwenye transifoma ambayo inasambaza umeme kwenye mitaa mingine ambayo imeendelea kupata umeme.
Wanaoishi pembeni mwa hiyo transifoma wana sema kuna kipande cha waya kilikatika asubuhi ya jana ndipo umeme ulipozima hata hivyo toka jana hakuna mafundi waliofika kutatua tatizo hilo toka jana mpaka leo licha ya kupewa taarifa mapema, hali hii ni ya kawaida kwa mafundi wa Tanesco kudharau taarifa za wananchi.